Mtake msitake wadada mashindano ya u-miss ni chanzo cha uhuni na mmomonyoko wa maadili | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtake msitake wadada mashindano ya u-miss ni chanzo cha uhuni na mmomonyoko wa maadili

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by gango2, May 9, 2012.

 1. gango2

  gango2 JF-Expert Member

  #1
  May 9, 2012
  Joined: Aug 31, 2011
  Messages: 1,237
  Likes Received: 453
  Trophy Points: 180
  Habari zenu wanandugu,

  Pamoja na kwamba taasisi na wadau mbali mbali wa tasnia ya urembo wanajaribu kuielemisha jamii kuwa mashindano ya umiss au umiss sio uhuni lakini nadhani mtakubaliana nami kuwa kwa kiasi kikubwa mashindano haya yamekuwa ni chanzo kikubwa cha mmomonyoko wa maadili na uvunjwaji wa utamaduni halisi wa mtanzania.

  siku hizi ili uwe miss au ushiriki mashindano ya umiss ni lazima ujiandae Kuvaa vichupi ili nawe uonekane vyema mbele ya wenzio. yaani vichupi ndo mavazi ya kimiss eti. Ndio najua uhuni ni tabia ya mtu na mtu anaweza kuvaa kichupi na asiwe muhuni lakini naamini ya kwamba pamoja ya kwamba utavaa kichupi na kutokuwa muhuni lakini kwa kiasi fulani utachangia kuharibu watoto wakike wengine kwani nao wanaweza kusema mbona fulani alikuwa anavaa kichupi lakini hakuwa muhuni.

  chonde chonde wadada naomba muwe makini sana, kama fedha zipo zipo tuu, sio mpaka mjidharirishe mbele ya watu, namna hiyo. miili yenu ni hadhina kubwa sana mbele ya jamii, hebu kabla hujafanya jambo lolote jaribu kutafakari kuwa linamanufaa gani kwako na kwa taifa.

  ndio wapo wachache ambao umiss umewafanya watambulike katika jamii, na wamekuwa mfano mzuri wa kuigwa but asilimia kubwa ya hawa watu wanaishia kuharibika,


  MAMIS WA KIBONGO.jpg

  hebu tazama picha hiyo hapo juu, pamoja ya kuwa wapo nusu uchi lakini wao wanaona furaha sana na wanachekelea,
   
 2. Kisusi Mohammed

  Kisusi Mohammed JF-Expert Member

  #2
  May 9, 2012
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 442
  Likes Received: 80
  Trophy Points: 45
  Ukweli mtupu, wasiokubaliana na Ukweli huo basically watakuwa na matatizo makubwa!
   
Loading...