Mtake msitake, CHADEMA kuweni makini na Marando

Msanii

Platinum Member
Jul 4, 2007
22,540
29,596
Wakati anahamia CHADEMA kutoka chama kingine cha siasa, niliweka maoni yangu wazi kwamba SIJAWAHI kumuamini na anapaswa kuogopwa katika siasa za vyama.

Anguko la Mrema na NCCR-Mageuzi ilikuwa ni sehemu ya kazi yake,
Kinacholeta ukakasi ni kwamba, wanasiasa wote waliotoka CCM kwa minajili ya kutoa upinzani wa dhati waliishia kutiwa misukosuko na hata kufilisiwa na hatimaye kulazimishwa kufa kisiasa na kurejea CCM. Pia ikumbukwe kwamba Tangu aibukie upinzani, Mwanasiasa huyu hajawahi kupata misukosuko na kizuri zaidi anafanikiwa sana ktk nyanja zote kimaisha.

Turudi kwenye random info
Alijitetea kwenye majukwaa ya siasa kwamba kuwatetea kwake mafisadi wa EPA mahakamani hakuhusiani na siasa za chama chake ktk kupambana na ufisadi, Na akasema yeye ni kama daktari hivyo hakatai mgonjwa. Ikumbukwe kwamba kesi za Mahakama kuu pekee ndizo ambazo WAKILI hana hiyari endapo atapangiwa kumtetea mtuhumiwa wa Jamhuri, Lakini kwenye mahakama za chini hakuna ULAZIMA wa wakili kusimama na kumkingia kifua public enemy ambaye yeye anahusika na presha zilizosukuma dola kuchukua hatua dhidi ya mtuhumiwa.

Twende sasa, majuzi hapa alifanya kosa ambalo mtu wa kawaida hajuzu kufanya, yaani kureveal majina ya UwT ambao wanatuhumiwa kufanikisha deal la Lwakatare, na serikali ikatishia kuchukua hatua na mpaka sasa hakuna lililotokea.

Siri nyingi za CCM na serikali yake zinavuja kwa mpangilio maalum, na ikumbukwe kwamba hata Dr. Slaa alishawahi kukiri kuwa sehemu kubwa ya UWT wanapeleka taarifa kwake, lakini kiuhalisia ni kwamba huyu bwana yupo nyuma ya haya yote. Na hata mipango mingi ya CHADEMA yenye manufaa kwa taifa imekuwa inavuja kwa CCM ambapo wanaidaka hoja hewani na kujimilikisha ili kupata reputation mbele ya jamii.

Nikiongelea tukio la hivi majuzi la kifo cha kutatanisha cha afisa UWT ambapo in connection kifo cha Imran Kombe kinahusika ktk utata huo pia, ni wazi kwamba kuna ujumbe mahususi [kwa mujibu wa watoa maoni] unatumwa kwa wanaovujisha siri MFU za serikali, hasa zile zinazohusu namna taifa linavyotafunwa kisawasawa na watu wachache. Ninapata nguvu ya kuamini kwamba huyu bwana yupo behind all these, yaani to unmask Romans.

Simsemi mwingine bali Mabere Marando. Ni hatari kwa afya ya siasa za vyama vingi.

NIMESEMA
 
Nadhani jambo la msingi ni kumtafakari kwa makini sana. Lakini CHADEMA wenzangu tunatakiwa kuwa makini sana na hizi post zinazoletwa huku.
 
Kama ni thread ya kipuuzi, hebu eleza ukweli wako unaoujua
Labda uanze kutueleza wewe huko Usalama wa Taifa alikuwa Department gani? na je una uwelewa wowote kuhusu idara ya Usalama wa Taifa au wewe ni mpiga tarumbeta tu.
 
We unafikiri CDM ni NCCR? muulize naibu katibu wako mkuu anavyohaha kuua soo la Lwakatare.
 
kwani umeambiwa chadema ni mtu mmoja?...pia ukumbuke wengi wa wanasia wakubwa unaowajua nchi hii ni UWT! ,ogopa wanasiasa wote basi,.
 
kwani umeambiwa chadema ni mtu mmoja?...pia ukumbuke wengi wa wanasia wakubwa unaowajua nchi hii ni UWT! ,ogopa wanasiasa wote basi,.
Kuna mijitu humu ni mijinga sana....

Laurence Gama ndio mkurugenzi wa kwanza wa Usalama wa Taifa lakini alipigwa chini ubunhe na mtoto mdogo kabisa Emanuel Nchimbi je hiyo system ilikuwa wapi isimsaidie former boss?

Kila mtu anamjuwa Hans Kitine naye alikuwa Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa lakini mtu mdogo ndani ya Usalama wa Taifa kama Bernad Membe akaweza kumshughulikia kwa sababu alikuwa ameshastaafu kazi, sasa hawa wanaomlazimisha Marando kwamba bado ni Ofisa wa usalama wa Taifa simply wana upeo finyu na upungufu wa busara. Hata Mizengo Pinda alikuwa Ofisa Usalama wa Taifa lakinio hayupo kule tena.

Nina rafiki yanguwa karibu sana amepata kazi kwenye international organization na offer ya mshahara wamempa nzuri, ameamuwa kuwaandikia wakubwa zake Usalama wa Taifa kuacha kazi na wamemkubalia na sasa anapiga pesa ndefu sana. ni ujinga tu kudhani Usalama wa Taifa ni kazi to the grave yard.
 
Hujui unachoongea wewe...
Once ukiwa snake hauwezi kubadilika na kuwa kenge tena...

Ila kitu kimoja ni kwamba, rushwa ya utajirisho na uongozi ndiyo inayotumika kuwabana wanausalama na kuitumikia CCM kwa gharama ya damu zao. Kama ninaongopa, basi hesabu za MEREMETA zingekaguliwa na CAG, na hata Deep Green ingelikuwa kwenye orodha ya waliofikishwa mahakamani kwa wizi wa mabilion ya hazina.

Visiki vilivyowekwa kwenye vyama vya siasa ndivyo vinavyotumika kuvunja nguvu za upinzani nchini.
 
Back
Top Bottom