Mtaji wa Sh. Mil 5 unafaa kwa biashara gani?

WATANZANIA TUNAPENDA SANA BIASHARA RAHISI NA ZISIZO HITAJI AKILI KABISA, BIASHARA YA BODABODA INAFANYWA NA WATU AMBAO WAMEFIKIA MWISHO WA KUFIKILIA NA AMBAO NA WAVIVU WAKUTUMIA AKILI

- Kwa magreat thinker kuja na wazo la Bodaboda ni kitu cha ajabu sana, ni kwa nini tusipende kuwekeza katika miradi yenye tija kwa taifa hili

1. Kwa nini si miradi yenye tija kwa taifa hili?

2. Kwa nini si uwekezaji ambao hata watu wa nje watatamani kufanya na wewe kazi?

3. Hii biashara si sustainable hata kidogo na sijui mtu mwenye hii biashara huwa anaplani niniu mbeleni

- Anzisha biashara ambayo miika kumi ijayo itakuwa ni biashara kubwa sana ndani na nje ya nchi hii,

- Watanzania utakuta mtu ana gest house moja ana Bodaboda tatu, ana kibanda cha simu na vocha, sasa mtu kama huyi sijui huwa anataget nini kuja kuwa vipi,

-HII DUNIA NI YA USHINDANI MKUBWA SANA NA KWA SASA ATAKAYE SAVAVIVE NI MTU ANAYE KUWA NA IDEA ILIYO ENDA SHULE, JARIBUNI KUTEMBELEA African Report muone vijana wa nchi zingine mawazo yao ya biashara, huwezi kuta vuijana kama wakule NIGERIA WANAPEANA USHAURI WA BODABODA HATA SIKU MOJA,

Nilizama Aidea ambayo hata ukiitwa kwenda kupresent mahali watu wanakuna vichwa na kukuona wewe ni mtu mwingine kabisa, sasa unaitwa unaenda kupresent Bajaji na Bodaboda utaonekana wa ajabu sana


Mbwembwe kibao, na umemalza pasipo kutoa ushauri zaid ya lawana

Nngekuona zimo kama ungehitimisha kwa kutoa ushauri.
 
hiyo ni kweli kabisa. Tujifunze kuwa na idea mpya ili tutamaniwe siyo kutamani. Kaka hapo juu umenikuna.....
Wenzenu wenye idea mnazosema hawawazi kuhusu kula. Kumbuka, sisi inabidi ufanye chochote ilimradi mkono uende kinywani. Hatuna suport labda kwa watoto wa kishua. Ndio maana tunaishia kushauriana vitu vya kutupatia chochote kitu na sio kuendeleza hicho kitu kikakua
 
Mi ni mwanafunzi wa mwaka wa pili nachukua shahada ya uhasibu. Wana JF nina mtaji sh. Million 5. Je naweza kuwekeza katika aina gani ya biashara na iweze kunilipa vizuri kwa miaka 2. Naombeni mnisadie kwa hili.
Nenda kusini ndani ndani huko ununue heka 30 za shamba upande korosho, tafuta hati na kila kitu baada ya miaka miwili peleka hati benki uombe mkopo MIL 190
 
Kama upo maeneo mazuri anzisha huduma ya MPSA inalipa sana kama ukishindwa MPSA anzisha duka la kuuza mitungi ya gesi nayo inalipa but depending with your location kama upo kwetu mkoa mpya wa Katavi biashara ya mitungi ya gesi hapo haina nafasi maana bado tuna misitu minene kwa hiyo tunatumia mkaa kwa sana
Nina idea y kuuza mitungi y gasi je inalipa dear npo interested San n hii kitu
 
tunataka wajasiriamali wenye financial stability kama kina Aliko Dangote, sasa bodaboda sioni kama kuna nafasi ya kukua zaidi ya kupata hela ya kula tu.
Yeah hasa ukizngatia n kwamb faida yke et mpka uwait kW muda w two years ,khaa Mimi Dada angu alijuta baada y mkopo wake wote kununulia Boda ...
 
Usiulize ni biashara ipi ya kufanya. Fanya kwanza utafiti ujue ni vitu gani vinahitajika hapo ulipo. Ukeshajua kuna soko ya hivyo vitu na faida yake kwa siku tafuta pia kujua kama upatikanaji wa malighafi ni rahisi. Kama soko, malighafi na eneo la biashara lipo, tafuta basi wahudumu wenye weledi. Hakikisha ni biashara ambayo unaweza kuifuatilia kwa karibu kila siku. Ukichukua bodaboda, utaweza kupata vijana waaminifu watakaokutunzia bodaboda zako? Maana unaweza kufanya mwaka ukute zote zimekongoroka.

Nakushauri fungua biashara ya vyakula - viwe vya kupika na kuuza au kununua jumla na kuuza rejareja ukiweza kupata source na wanunuzi kuna faida nzuri na hakuna headache.
 
Mi ni mwanafunzi wa mwaka wa pili nachukua shahada ya uhasibu. Wana JF nina mtaji sh. Million 5. Je naweza kuwekeza katika aina gani ya biashara na iweze kunilipa vizuri kwa miaka 2. Naombeni mnisadie kwa hili.
Mrejesho mkuu
 
Nikupongeze kijana kwa kuwa na pesa na kuamua ikusaidie kutafuta pesa zaidi
Unapaswa kutambua hakuna biashara isiyokosa changamoto, iwe ndogo au kubwa
Kadiri biashara inavyokuwa kubwa, na changamoto nazo huongezeka

1. Bodaboda
Hakikisha unaandikishiana mkataba na dereva
Hakikisha kunakuwepo na daftari la malipo, kila siku akileta hela anasaini
Hakikisha mkataba unatamka kuwa amalizapo mkataba, pikipiki itakuwa yake, hii huchochea ari ya yeye kuitunza
Hakikisha asipoleta hela hadi ikafika elfu 50, unamnyang'anya pikipiki, zaidi ya hapo huwa hawana uwezo wa kulipa
Usijenge urafiki na dereva, hata akufurahishe vipi, baki kuwa kauzu
Epuka kumtumia yeye akupeleke sehemu za starehe, au akamchukue demu wako au bwana wako mahali
Mahusiano yenu yawe ya kazi tu.

2. Mobile money
Wapo watu wanaouza hizo laini kwa bei chee, nunua hizo, utaelekezwa namna ya kutoa pesa yako kwa urahisi
Uombe mungu usipate tatizo litakalokulazimu uende kwenye kampuni za simu, kwakuwa laini si zako, hutopata msaada isipokuwa mwenye jina lake
Ueke mtu aliyetulia kichwani, anaweza akatumiwa meseji ya kawaida inasomeka mteja katoa hela, kumbe chenga. Yeye akajikuta katoa cash halafu float haijaongezeka. Ndivyo wanavyopigwaga. Awe makini
Anza na mitandao mitatu mikubwa unayoiamini wewe
Usisahau vocha za kurusha na kamashine kaluku
Si lazima fremu hata vile vibox mwake tu au meza na mwamvuli, shega pia
Hakikisha mnaona na huyu mtu kila siku, tena kwa nyakati tofauti, asijue utamuibukia saa ngapi

3. Mitungi ya gas
Ukipata fremu ukaamua kufanya biashara namba 2, basi hata hii utafanya hapohapo
Faida ya mtungi ule mdogo, huwa ni elfu 5, kwa mpya na ule wa kujaza, kama zitapishana si sana, inategemea na kampuni
Unaweza anza na michache, na ukakua polepole
Mtaji wa milioni 2 na nusu unaweza ukakutoa mazima
Eneo lazima liwe ni la makazi ya watu
Weka namba ya simu, wateja wengine wanapenda kupelekewa, akikupigia, unampa bodaboda na namba ya simu ya mteja waelekezane mpaka mtungi umfikie
Hakikisha hakopeshi mtungi
Hakikisha unakaba hadi penati, wanakawaida ya kuongeza mitungi yao, yako hawauzi
Weka namna nzuri ya usimamizi

4.Biashara ya vinywaji baridi
Kama unaweza kupata fremu maeneo kama ya ubungo
Basi nunua freezer, weka maji na soda
Tafuta vijana watakouza kwenye foleni
Utahitaji vijana kama sita, watano wanaizunguka kwenye foleni, na mmoja anaetunza mahesabu

Usisahau kuleta mrejesho kwakile utakachoona ni sawa.
Meflo Mswahili
 
Sikushauri ununue bodaboda. utapata presha bure. nimeshaifanya inausumbufu sana. Nenda kibaigwa nunua alizeti kwa sasa gunia ni elfu 35 , kaifadhi kwenye mashine za kukamulia ,kaa miezi mi4 uza gunia kwa elfu 55. Ushauri zaidi ni pm
Kwenye hii on average atapata 700,000 per month I'm gross income but subject to changes in demand and supply so it is equally likely that the price can also drop from 35,000 to 25,000 in four months
 
Back
Top Bottom