Mtaji wa Milioni 5-10 (TZS): Biashara gani unaweza kufanya?

Kuna thread moja ya kilimo cha green house humu nadhani huyo mama aliyeanzisha thread ile anaweza kukusaidia, umeshawahi iona? Nadhani pia wataalam wengine kama kina Zanzibar Spices watakuja kukusaidia.....Mimi nazidi kukuombea ufanikiwe katika kila jambo.

Pamoja mkuu ngoja niitafute nione,
 
Last edited by a moderator:
Mkuu tupo hapa kwa lengo la kushauri na kiasi flani kukuonesha njia ipi upitie na magumu yapi utakutana nayo katika safari yako ya uboreshaji wa maisha yako.
Umefanya la maana sana kuleta wazo lako JF kabla hujaitumia hiyo hela.
Leo nimejitokeza kwa mara nyingine tena kukupa ushauri wangu make nilikaa kimya kuona uelekeo wako. Kwakuwa umeegemea kwenye kilimo, nimeona ni vyema nikashare nawe pamoja na wana JF wote uzoefu wangu kwenye zao la Tikiti maji.

Kwanza kabisa nakuomba uende taratibu, mdogomdogo malengo yako yatatimia tu. Lengo nataka uokoe huo mkopo-kumbuka unadaiwa zaidi ya hiyo 7M.
Usikimbilie kununua Drip Lines kwa sasa ni ghari mno na pesa yako ni ndogo sana. Kilimo ni patapotea haijarishi umejipanga vipi, utalima au kimekuingia damuni kiasi gani! Tafta namna nyepesi kwako ili ikitokea kwamba umeanguka basi uwe na capital ambayo itabackup maumivu ya awali na wakati huo tayari utakuwa ushasoma mchezo kwauzuri.

Sasa basi zingatia haya yafuatayo;

Mhimu zingatia maji, dawa,
mbolea na huduma iliyojitosheleza.
Naimani ushapata soko la uhakika. Epuka kulima kabla hujafanya utafiti wa soko/mlaji.
Pata wafanyakazi wa uhakika na waaminifu. Simamia mradi wako muda wote.
Pata mshauri mtaalam mwandamizi wa hiki kilimo ambaye atakuwa na wepesi wa kuhudhuria/fika shamba pindi utakapo mhitaji.
Jenga mazoea ya kujifunza tabia na mwenendo wa zao husika kila siku hapo utaongeza ubunifu na kuepuka makosa mbele ya safari.
Kwa kilimo cha Matikiti yafuatayo ni mhimu kuzingatiwa;
Epuka kulowanisha majani ya tikiti
Epuka kumwagilia mida ya jioni sana ili yasilale/kae na unyevu muda mrefu.
Epuka kugeuza geuza shina/majani kusiko kwa lazima.
Epuka kupiga dawa mida ya asubuhi utafukuza wadudu marafiki wa uchavishaji.
Hakikisha unadhibiti wadudu waharibifu km panya make hula sana bulbs ktk nursery stage na tafadhari sana usilowanishe wala kugusa tunda changa na ikibidi weka matandiko ya nyasi au kibao chini ya tunda.
Zidisha huduma na akili yako ifocus kwenye huduma bila kuwaza kitakachotokea...
Weka vivutio vya nyuki shambani kwa kutupia nta au vipande vya tunda la fenesi ili uchavishaji ufanyike kwa mkupuo.
Kipindi cha maua maji yawe ya wastani ila ya uhakika.
Kujua kama tunda limekomaa, angalia kijikamba kimezunguka kama coil au spring karibu kabisa na tunda lenyewe. Ikiwa kimeanza au kinaonesha dalili ya kukauka basi ujue tunda lipo tayari kuvunwa.
Usivune mpaka uwasiliane na mteja wako aje ashuhudie mwenyewe ukomavu au dalili za kukomaa.

Lima kwa njia ya furrow(FARO) ya mifereji.
Mfereji wa kusukuma maji uwe 30cm (MAIN TRUNK) na utapanda matikiti kwenye mifereji ya 60cm (DISTRIBUTARIES) ambayo itakuwa na urefu wa 8metres. Panda zigzag kila upande.
Mifereji ya 60cms utaipishanisha kwa 2metres na huo upandaji wa zigzag kwenye fereji panda punje mbili kila shimo kwa umbali wa angalau 1metre.
Matunda yakishaanza kutambaa yalazie kwenye tuta/kingo (ulilopishanisha kwa 2metres) kila shina na upande wake huku ukiacha uwazi kwenye huo mfereji wa 60cm kuruhusu maji yatembee bila shida.
Utapiga dawa kwa kusimama juu ya matuta/jamvi kabla matikiti hayaja tambaa na yakishatambaa pita kwenye mifereji.
Palizi ifanyike kabla shina halijatambaa na baada ya hapo dhibiti magugu kwa kung'olea hasa kipindi cha maua. Usipalilie tena baada ya kujotokeza kwa matunda.
Tumia mbegu ya SUGAR BABY(ROYAL) au SUKAR F1 (HYBRID japo hii haizai sana)

Tumia BLAST kama kiuatirifu kwaajili ya wadudu km amphids na viroboto wa kijani na wadudu wengine wanao shambulia majani,maua na tunda
Tumia BLUE Copper, Ridomil au Ivory kwaajili ya kuvu/ukungu.
Mbolea nayo ni mhimu sana AGROVET watakushauri ni mbolea ipi inafaa pande hizo kwajili ya kukuzia na kuzalishia plus booster.

Makisio kwa ekari1 ni kama ifuatavyo:
Kawaida ekari1 ni 4000m²
upandaji ni 1m each na 2m apart.
kila shimo miche2
kila shina matunda2 ya nguvu
Bei ya shamba sh 1000@
Hapa nimefanya roughly kwa kuondoa baadhi ya vipimo lakini hesabu zinalalia hukohuko.
Hivyo basi ekari1 itacontain mashina
4000m²/(1m×2m)×2miche= 4000
Number ya matunda 4000×2=8000
Makisio ya kipato bila gharama 8000×1000= sh8,000,000/=
Hesabu siku zote huwa haidanganyi. Ila juhudi zetu ndo mchawi wa kuyafikia malengo.
Nakushauri uanze na eneo dogo ili uweze kujifunza vizuri na kumudu changamoto.
Kikwazo kikuu ni wasaidizi. Uwe makini nao hasa kwenye upigaji dawa na mbolea.
Jingine kubwa ambalo nilisahau kukuelekeza ni umakini mkubwa utahitajika karibu na mavuno kuanzia siku ya 65-70 baada ya kupanda usiendelee kumwagilia kuruhusu sukari ijenge zaidi na kuepuka yasijaze maji mengi yakapasuka. Na katika siku 15 za mwisho omba Mungu matikiti yasinyeshewe mvua. Kama ni hybrid basi utahesabu maumivu make huwa yanabadilika na kuchora vidoadoa vyeupe ikifuatiwa na uozo wa haja!!!(usiogope)

Ndiyo hayo mkuu nimetumia muda mwingi sana kuandika haya maelekezo km kuna sehemu nimeruka basi usisite kuuliza na pia kuna wadau wengine watajazia mwanya!
KILA LA KHERI MKUU.
 
Usimwigize mwenzio Jehannam... RIBA ya aina yoyote ni haram soma hapa... nimeweka hii maana sijui wewe ni dini gani ila kama wewe ni muislam kama mimi basi huu ndio usia wangu kwako... Ya Allah nimewasilisha

RIBA NI DHAMBI KUBWA; YAINGIZA MOTONI
Katika Qur’ani Mola amesema :
( الَّذِينَ يَأْكُلُونَ الرِّبَا لاَ يَقُومُونَ إِلاَّ كَمَا يَقُومُ الَّذِي يَتَخَبَّطُهُ الشَّيْطَانُ مِنَ الْمَسِّ ذَلِكَ بِأَنَّهُمْ قَالُواْ إِنَّمَا الْبَيْعُ مِثْلُ الرِّبَا وَأَحَلَّ اللّهُ الْبَيْعَ وَحَرَّمَ الرِّبَا فَمَن جَاءهُ مَوْعِظَةٌ مِّن رَّبِّهِ فَانتَهَىَ فَلَهُ مَا سَلَفَ وَأَمْرُهُ إِلَى اللّهِ وَمَنْ عَادَ فَأُوْلَـئِكَ أَصْحَابُ النَّارِ هُمْ فِيهَا خَالِدُونَ)
“Wale wanaokula riba hawasimami ila kama anavyosimama aliye pandwa na Shet’ani kwa wazimu. Hayo ni kwa kuwa wamesema: ‘Biashara ni kama riba tu’, wakati Mwenyezi Mungu ameihalalisha biashara na kaiharamisha riba. Hivyo aliyefikiwa na mawaidha kutoka kwa Mola wake akaacha [kula riba], basi ni chake kilichotangulia, na hukumu yake iko kwa Mwenyezi Mungu. Ama wenye kurudia basi hao ndio watu wa Motoni, humo watadumu” (Albaqara, aya-275)
Wenye ilmu wanasema aya inatupa taswira ya wanaokula riba watapokuwa wanatoka makaburini mwao siku ya kiyama ya kwamba watakuwa wakitapatapa, wanasimama wakianguka kama mtu aliyeingiwa na shetani.
MLA RIBA HAWI MUUMINI :
Mwenyezi Mungu amebainisha kuwa kula riba na imani hayakubaliani:
(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اتَّقُواْ اللّهَ وَذَرُواْ مَا بَقِيَ مِنَ الرِّبَا إِن كُنتُم مُّؤْمِنِينَ)
”Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu, na acheni kilichobaki katika riba, ikiwa nyinyi ni Waumini” (Albaqara, aya-278)
Kwa hivyo ikiwa sisi ni waumini kweli basi tumche¹ Mwenyezi Mungu na tuache riba.
SIYEACHA RIBA KATANGAZIWA VITA NA MWENYEZI MUNGU :
Mwenyezi Mungu amesema baada ya aya iliyotangulia:

.( فَإِن لَّمْ تَفْعَلُواْ فَأْذَنُواْ بِحَرْبٍ مِّنَ اللّهِ وَرَسُولِهِ وَإِن تُبْتُمْ فَلَكُمْ رُؤُوسُ أَمْوَالِكُمْ لاَ تَظْلِمُونَ وَلاَ تُظْلَمُونَ)
“Na kama hamtafanya [hivyo], basi jueni kwamba mtakuwa na vita na Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Na mkitubu, basi haki yenu ni rasilmali zenu. Msidhulumu wala msidhulumiwe” (Albaqara, aya-279)
Vita vya Mwenyezi Mungu si vya risasi au mabomu, lakini vita vya Mwenyezi Mungu hapana mtu ambaye anaweza kuvikimbia. Miongoni mwa vita vya Mwenyezi Mungu ni kupatwa na maafa mengi kama vile dhiki au mtu kutokuwa na raha katika maisha yake hata akiwa na mali nyingi. Kwani Mwenyezi Mungu huondoa baraka katika mali ya riba::
(يَمْحَقُ اللّهُ الْرِّبَا وَيُرْبِي الصَّدَقَاتِ وَاللّهُ لاَ يُحِبُّ كُلَّ كَفَّارٍ أَثِيمٍ)…
“Mwenyezi Mungu huifutia baraka [mali ya] riba, na huzibariki [mali zinazotolewa] sadaka. Na Mwenyezi Mungu hampendi kila mwenye kukana [amri Zake], mtenda dhambi” (Albaqara, aya-276)
Huwenda ukamuona mtu masikini lakini akawa yumo katika furaha kuliko huyo anayekula riba. Sababu ya huyu kuwemo katika furaha ni ahadi ya Mwenyezi Mungu aliyoahidi ya kuwa Mu’umini yeyote atakaetenda mema (mke au mume) basi atamhuisha maisha mazuri na atamlipa malipo mazuri akhera:
(مَنْ عَمِلَ صَالِحاً مِّن ذَكَرٍ أَوْ أُنثَى وَهُوَ مُؤْمِنٌ فَلَنُحْيِيَنَّهُ حَيَاةً طَيِّبَةً وَلَنَجْزِيَنَّهُمْ أَجْرَهُم بِأَحْسَنِ مَا كَانُواْ يَعْمَلُونَ)
“Mwenye kutenda mema, mwanamume au mwanamke, naye akawa ni Muumini, tutamhuisha maisha mema; na tutawapa ujira wao kwa bora ya waliyo kuwa wakiyatenda” (An Nah’l, aya-97)

Lakini atakae pinga amri za Mwenyezi Mungu basi atakuwa na dhiki hapa duniani na siku ya kiyama atafufuliwa kipofu:

(وَمَنْ أَعْرَضَ عَن ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنكاً وَنَحْشُرُه يَوْمَ الْقِيَامَةِأَعْمَى)
“Na atakayeacha kufuata mawaidha yangu, basi kwa yakini atakuwa na maisha ya dhiki, na Siku ya Kiyama tutamfufua hali ya kuwa kipofu” (Ta’ha, aya-124).

Bila ya shaka hapana mtu aliye tayari kufufuliwa kipofu, kisha aingizwe motoni. Kwa hivyo hapana budi ila tuyapokee mawaidha ya Mola wetu.

Kwani umeambiwa kila mtu muislam??
 
Kisima
Asante sana kwa ushauri wako mkuu, kwa msimu huu nitaanza na nyanya, baada ya nyanya cabbage na mwez wa nne tikiti, pia nitaanza kupanda rasimi mwezi wa tisa katikati hadi wa kumi kwan kwa sasa naandaa shamba ili liwe tayari kupokea mazao(kusafisha na kulilainisha) na kuandaa samadi, naenda taratibu ili wafanya kazi wasione ninaharaka wakanibamiza, pia kwa kipindi hicho wengi watakua wameanza kilimo cha mazao ya msimu,
 
Last edited by a moderator:
Mkuu bab-D umakini kwenye Hali ya Hewa ya ukanda huo nao lazima uuzingatie sana sana! usianze kilimo kwenye kipindi cha changamoto na ukinzani mwingi kati ya hali ya hewa,soko na nguvu kazi.
Kwa nini nasema hivyo?
HALI YA HEWA
Ukianza project ya nyanya kipindi cha mvua nyingi,utakutana na vikwazo vingi sana. Kipindi hiki wadudu na ukungu hushamiri. Hivyo utatumia nguvu nyingi sana kuikabili hii changamoto hasa kwa nyanya. Nashauri bora upande HOHO.

SOKO
Kuna kipindi zao fulani huwa linafurika sokoni na kupelekea mpolomoko wa bei, ukikutana mkulima ambaye hajatumia nguvu nyingi kwenye gharama yeye yupo radhi auze hata plastic 1 ya nyanya kwa sh1000,lazima akuvuluge tu!
NGUVUKAZI
Mara nyingi sana kwenye msimu wa kilimo upatikanaji wa wasaidizi huwa ni tatizo kubwa sana. Make nao hujikuta wapo kwenye uzalishaji kwenye family zao. Inabidi uzidishe umakini kwenye kutarget kipindi gani huwa wapo loose.
Hakikisha unaingia nao mkataba. Chukua angalau wawili wenye uzoefu wa kazi. Ingia mkataba wa hadi mavuno. Mimi huwa tunaelewana sh200000-250000. Kawaida mkataba huanza baada ya kupanda zao.Utatoa advance baada ya kuona sustainance ya zao.

Nimeona nikazie hapo ili uangalie uwezekano wa either usipeedup project yako kujihami na hizo constraints tajwa hapo juu. Ukianza na ukinzani mwingi utateseka sana na kwanini ufail wakati kuna uwezekano wa kukwepa majanga? na why uanze na majanga?
Pambana mkuu na karibu sana kwenye kilimo!!
CC
Zanzibar Spices
 
Last edited by a moderator:
Mkuu bab-D umakini kwenye Hali ya Hewa ya ukanda huo nao lazima uuzingatie sana sana! usianze kilimo kwenye kipindi cha changamoto na ukinzani mwingi kati ya hali ya hewa,soko na nguvu kazi.
Kwa nini nasema hivyo?
HALI YA HEWA
Ukianza project ya nyanya kipindi cha mvua nyingi,utakutana na vikwazo vingi sana. Kipindi hiki wadudu na ukungu hushamiri. Hivyo utatumia nguvu nyingi sana kuikabili hii changamoto hasa kwa nyanya. Nashauri bora upande HOHO.

SOKO
Kuna kipindi zao fulani huwa linafurika sokoni na kupelekea mpolomoko wa bei, ukikutana mkulima ambaye hajatumia nguvu nyingi kwenye gharama yeye yupo radhi auze hata plastic 1 ya nyanya kwa sh1000,lazima akuvuluge tu!
NGUVUKAZI
Mara nyingi sana kwenye msimu wa kilimo upatikanaji wa wasaidizi huwa ni tatizo kubwa sana. Make nao hujikuta wapo kwenye uzalishaji kwenye family zao. Inabidi uzidishe umakini kwenye kutarget kipindi gani huwa wapo loose.
Hakikisha unaingia nao mkataba. Chukua angalau wawili wenye uzoefu wa kazi. Ingia mkataba wa hadi mavuno. Mimi huwa tunaelewana sh200000-250000. Kawaida mkataba huanza baada ya kupanda zao.Utatoa advance baada ya kuona sustainance ya zao.

Nimeona nikazie hapo ili uangalie uwezekano wa either usipeedup project yako kujihami na hizo constraints tajwa hapo juu. Ukianza na ukinzani mwingi utateseka sana na kwanini ufail wakati kuna uwezekano wa kukwepa majanga? na why uanze na majanga?
Pambana mkuu na karibu sana kwenye kilimo!!
CC
Zanzibar Spices

Asante saana kamanda
Huu umempa ushauri mzuri saaana.

Kwa mkulima anaeanza lazima hizi tahadhari asichukue mapema.Lakini angekuwa mzoefu wa muda mrefu basi angejua kwamba namna ya kupambana na hizi changamoto na angeweza kulima muda wowote.

Ila mwanzo lazima uchukue tahadhari sana ili usije kuchukia Kilimo kwa kukosea Target katika muda wake na masoko pia

Suala la wafanyakazi pia naungana na wewe mkuu,wapo ambao kama hawana mkataba wanaweza kukupoteza wakati mazao yanapoelekea kuzuri,maana siku hizi kilimo kimeingiliwa na wafitinishaji.
Anaweza mtu kuona mazao yamestawi basi akaja kumshawishi mfanyakazi wako aache kazi aende kwake kwa dau kubwa.Ila kama kuna mkataba basia takuwa anaogopa,maana anajua ukimnasa basi kote atakosa
 
Kwa planner mim kwanza naselect idea ya kujenga choo, nipate super profit niitumie kuinvest kwingne. Gud idea for short term project/business
 
Nashukuru iposiku lengo litatimia la kulima na kumwagilia kwa drip irrigation kwani wasambazaji wameanza kupunguza bei
za drip lines, kwa sasa wengi wanauza
tsh 600/mita. wakati walikua wanauza
tsh950/mita nazani nanenane zitashuka
zaidi ngoja tusubiri.kwa sababu kwa nyanya eka moja itahitaji kama mita 5000 sawa na 5000*600= tsh3 000 000/=ambapo bado ni gharama kubwa sana
 
Nashukuru sana Kisima kwa ushauri wako, pia kuonyesha kunijali na kunisindikiza kuelekea mafanikio,Bado naliludia kulima ili lilainike zaidi il wiki ijayo nianze kufanya hallowing na kupiga matuta kama ikiwezekana, kwani miche bado sana
 
Last edited by a moderator:
Kopa pikpik za miguu mi3 (piagio) mbili kwa milion tatu kila moja yan jumla yake milion 6 then zilipie na BIMA kubwa! tafuta madereva ingia nao mkataba ambao huwa ni miez 18 baada ya hyo miez chombo knakua cha dereva

Kila siku elfu 40 kwa zote mbili ambazo watakua wanakuletea kwa wik laki 2 na elfu 80 kupata kwa mwez utazdsha hapo mara 4

Then uingie mkataba na hao wahind kila mwez uwe unapeleka milion yan lak 5 kila piagio..then ndan ya miez sita znakua za kwako
 
Mkuu Limited Edition kwa sasa tayari nishaanza kilimo siwezi badili kwa sasa, sema niweke wazo jingine kwa mradi mwingine na kwa mpango mwingine, pia kwa wazo lako sawa, ila mi naona labda tax, ukipata kwa 4M na ukawa unaletewa kiwango cha 20 000/siku sio mbaya kwan huwa hazifanyi kaz sana kijiweni.
 
Last edited by a moderator:
Swala siyo ukubwa wa mtaji ila kwanza jua unataka kufanya biashara gani kwani biashara nyingi zinaweza kuanza hata na milioni 1 sema aina ya biashara ushauri upo tele
 
wajameni eeh, nimebahatika "kupata" mahala ka-Mtaji. Ni kiasi cha shs. milioni kumi tu, (10,000,000/=) za Kitanzania.

Nipeni mapendekezo nizi invest wapi, kivipi na matarajio ya faida.
(i.e biashara gani inalipa (plus location), kwa muda gani, na SWOT analysis zake)


-----------------


Hapa atahitajika kununua eneo pia?akinunua hela hiy haitatosha nazan
 
Back
Top Bottom