Mtaji wa Tsh. Milioni 1 hadi 5: Naweza kufanya Biashara gani Tanzania?

Mdogo wangu kwanza nikupe hongera kwa kuwa na akili ya kazi. Kuona kwamba expenses sio sawa na asset.

Pili nikwambie kwamba usiwasikilize wanaokupa adisi za kwenda kuspend 60% ya capital yako kwenye expense moja katika business operational yako.

Ushauri wangu sababu bado upo shule, zunguka kwenye mabank mbali mbali angalia interest rate kwenye fixed deposit accounts. Kisha tulushie hizo rate hapa nitakuchambulia wapi ni bora.

Weka hiyo pesa kwenye fixed deposit kwa muda wote ambao upo shule, maliza shule hiyo fedha itakuwa imepata atleast 15% return. Then baada ya hapo twende kazi unaweza kuangalia wapi uwekeze.

Mwisho kumbuka unaweza 100% debt (sababu ni mkopo) na debt to equity ratio ni kwamba kwenye kila shilingi unayotaka kuwekeza umekopa shillingi nzima...
Hongera mkuu umenirudisha Shule IFM
 
Ni ngumu kumanage biashara na masomo kwa wakati mmoja.

Biashara nayo inahitaji uangalizi wa makini.

Mimi niliwahi kuwa na duka la nguo nikamwachia ndugu yangu ambaye nilimuamini.

Sasahivi imebaki historia. Nakushauri uende maeneo ya chanika au kibamba ndani ndani ukanunue ardhi.

Hadi ukija kumaliza chuo hata ukitaka kuiuza utaiuza kwa faida maana ardhi value yake inapanda kila siku.

Au unaweza ukanunua printer na computer ukawa unatype kazi za watu hapo chuo.
Kama ulishauriwa hivi mwaka 2011 kuhusu ardhi, HONGERA Mkuu.... HONGERA SANA... Ardhi ndio kila kitu... Huyu alokushauri hivi MWAMBIE SHIKAMOO....

Sent from my TECNO F2 using JamiiForums mobile app
 
Biashara inaanza na wewe mwenyewe, hilo wazo unaloulizua jf huwezi toboa maana ukikutana na changamoto kubwa utakimbia kwa kasi ya 5g.

So kwa kifupi wazo imara la biashara linatoka katika akili yako mwenyewe maana wazo lenyewe linakua chachu ya kukufanya upambane hata wakati wa changamoto.
 
Ivi mtu akiwa na milioni zake tatu
Ana weza akawekeza kwenye Biashara gani na akapata faida nzuri apa Dar es salam
Fungua duka la nafaka, uwe unuza unga aina zote,mchele bei tofauti, maharage, njegere na mafuta.....
 
Nenda kariakoo ukatandaze nguo/sandals chini hukosi pesa pale ili mradi tu ujue kuchagua bidhaa quality na bei iwe rafiki. Hiyo pesa yako usijiloge ukafanya biashara inayohusu kukodisha frem 1.2M ni hela ndogo sana kwa biashara inayohusu frem.

Pia ni hela nyingi snaa ukiamua kufanya umachinga smart, utapiga hela mtaji utaongezeka na utapata idea nyingine kubwa ukiwa humo. Cheers.
Hivi ukitandaza nguo chini unamlipa nani
 
Niaje wanajamvini?

Nina mtaji wa mil.2 ninahitaji wazo la biashara itakayoingiza atleast 20 kwa siku.

Yeyote mwenye uzoefu na makadirio ya mtaji, shughuli husika na faida yake anijuze


Ukifikiria vipodozi na urembo njoo nikuuzie vitu vya ukweli napatikana Arusha
 
Back
Top Bottom