Mtaji wa Tsh. Milioni 1 hadi 5: Naweza kufanya Biashara gani Tanzania?

Habari wapendwa katika bwana,

Mimi ni muajiriwa serikalini, nimeamua nichukue mkopo kutokana na ukweli kwamba serikali ya awamu ya tano si rafiki kwa watumishi wa umma, kufukuzwa kazi kuko nje nje tu kwa huu utawala uliopo,

Hivo nimeamua nichukue changu mapema hata kama ikiitokea bahati mbaya nikatimuliwa kazi niwe na pakuanzia.

Mtaji nilionao ni Milion 5, hoja inayonisumbua ni biashara gani ambayo nitaifanya angalau nipate faida ya laki 5 kwa mwezi. Ikumbukwe kuwa mkopo huu nimeuchukua bila kuwa na naandalizi ya aina yoyote, Bali ni hofu iliyonijaa dhidi ya utawala huu wa awamu ya tano kwa watumishi wa umma ambapo diwani, Mkuu wa wilaya nk. Wanayo mamlaka ya kukumwagisha unga bila hiyana.

Wataalamu naomba mnisaidie mawazo yenu ili nijikwamue kwa hiki kiasi nilicho nacho
sioni njia yako ya kusavaiv na huo mkopo rudisha tu pesa ya watu kabla ya haijakutokea puani.

sikukatishi tamaa nakuambia ukweli
 
Fungua duka la vyakula na vinywaji barid...ukipata frem nzur yenye eneo la wazi,,unaweka bia pia na nje unaweza kuweka chips na supu kongoro kwa ajili ya walevi wako


Inategemea na eneo ila hyo kitu inalipa sana
 
Siyo vizuri sana kukopa ukaanzisha biashara inapendeza sana ukope ukiwa tayari ushaanzisha busness ushajua changamoto zake ana wao angalia mazingira uliyonayo ujaribu yafatayo
1.kuuza nafaka
2.kutengeneza mkaa
3.fungua car wash
4.fungua mgahawa uza vyakula vikavu na sifa drinks mfano, chips, ndizi za kuchoma nk
5.fanya value addition kwenye vitu na uuze mfano maziwa(milkshake, yoghut)
Usiweke pesa yote mwanzoni kumbuka biashara ni usimamizi na bidii inahitajika sana, mwisho usisahau kumtanguliza bwana Yesu Kristo kwa kila jambo
 
Mkuu kwa awamu hii tena wew bado huna experience kabsa kwwmye biashara,hata ufanye biashara gan,tena mwanzo qa mwaka huu,yaan had uje ukae sawa mkuu hyo mil5 itakutokea puan,mim nna experienc kuubwa kwwnye biashara,..tuliza akil yako,hyo hela kuikopa bila kufanya upembuz yakinifu ulifanya makosa makubwa...we si unaona watu wanafunga frame sasa,si chakula si biashara gan,hali ni mbaya sana..mi nna biashara 3,nmefunga mbil mwez uliopita,imebak hii 1 nayo naipa muda tu...kua makin,stak kukukatisha tamaa ila biashara had uje kukaa sawa,sio kwa hela hyo ya mkopo mkuu,itakuumiza
 
Back
Top Bottom