Mtaji wa milioni 1-5: Naweza kufanya Biashara gani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtaji wa milioni 1-5: Naweza kufanya Biashara gani?

Discussion in 'Biashara, Uchumi na Ujasiriamali' started by maguu, Aug 12, 2011.

 1. m

  maguu Member

  #1
  Aug 12, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wakubwa nina mtaji wa shilingi milioni mbili na nataka nifanye biashara.

  Je, biashara gani ninaweza kufanya kulingana na pesa hiyo?

  Nimetafakari sana ila nakosa kujua kwa usahihi biashara gani inanifaa.

  ===========
  SIMILAR CASES:
  ===========

  May 18, 2012:
  May 10, 2014:
  May 16, 2014:
  Oktoba 09, 2014:
  Oktoba 22, 2014:
  Novemba 10, 2014:
  Feb 18, 2015:
  Aprili 13, 2015:
  -----------

  12 Aprili 2016

   
 2. Son of Africa

  Son of Africa JF-Expert Member

  #2
  Aug 12, 2011
  Joined: Jan 16, 2011
  Messages: 233
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Nipe cv yako nikushauri ipasavyo. Mimi ni mtaalamu aliyebobea biashara na uchumi
   
 3. m

  maguu Member

  #3
  Aug 12, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Wakubwa nina mtaji wa shilingi milioni mbili na nataka nifanye biashara.

  Je, biashara gani ninaweza kufanya kulingana na pesa hiyo?

  Nimetafakari sana ila nakosa kujua kwa usahihi biashara gani inanifaa. Hiyo pesa nimekopa bank.
   
 4. m

  maguu Member

  #4
  Aug 12, 2011
  Joined: Aug 12, 2011
  Messages: 12
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Mimi ni mfanyakazi wa Serikali nipo Mbeya, nina elimu ya degree ya sheria, ila ninafanya kazi tofauti na sheria, hivyo kutokana na ugumu wa maisha nimeona bora nikope bank ili niweze kuanzisha biashara kwa ajili ya kuongeza kipato.
   
 5. m

  mihiwe Member

  #5
  Aug 12, 2011
  Joined: May 28, 2011
  Messages: 23
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sina uhakika ila ukiomba mkopo si unapeleka mchanganuo kwanza na wakiridhika ndio unapewa hela, sasa kama ni hivyo ni bora ufuate huo mchanganuo vinginevyo,tunasubiri majibu baada ya sikukuu.
   
 6. pomo

  pomo JF-Expert Member

  #6
  Aug 12, 2011
  Joined: Jun 26, 2011
  Messages: 265
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  soma thread ya jamaa mmoja yeye alikuwa na 3m huenda michanganuo ilio tolewa itakufaa
   
 7. d

  damashizo Member

  #7
  Aug 12, 2011
  Joined: Jan 20, 2011
  Messages: 61
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 13
  kuomba ushauri wa biashara ni muhimu lakini nafikiri watu waliojirani na eneo lako au wanaokuzunguka watatoa ushauri mzuri kwani wanajua biashara gani hapo ukifanya kutokana na mazingira hayo italipa zaidi, siwezi sema uazishe duka au stationary wakati kwenu maduka ni mengi sana kiasi kwamba kuna uwezekano wa kukosa mteja kwa siku. TRY TO EXPLORE OPPOTUNITIES SO PRESENT IN YOUR LOCAL AREA AND CONSULT BUSINESS ADVICES TO YOUR LOCAL AREA. TNKS
   
 8. Mshiiri

  Mshiiri JF-Expert Member

  #8
  Aug 12, 2011
  Joined: Jun 16, 2008
  Messages: 1,894
  Likes Received: 73
  Trophy Points: 145
  Katika entrepreneurial skills unatakiwa kuwa na business plan kwanza, then plan itagharimu kiasi fulani. Hivyo capital ni swala linalojileta lenyewe. Usipofuata principle hii hutafanikiwa kama mjasiria mali.

  Naomba kuwakilisha
   
 9. Nkandi

  Nkandi Member

  #9
  Aug 15, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 83
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 15
  Kwanza yabidi ufahamu what is your interest in Business!where are you located and who are your predicted customers!ukishajua hayoutafanya uamuzi
   
 10. Pascal Mayalla

  Pascal Mayalla JF-Expert Member

  #10
  Aug 15, 2011
  Joined: Sep 22, 2008
  Messages: 25,622
  Likes Received: 23,762
  Trophy Points: 280
  1. Sifurahishwi na Mwanasheria kukopa benki milioni 2 kama mtaji wa kuanzisha biashara wakati wanasheria straight toka vyuoni ndio wanalipwa ujira huo wakiwa Legal Officer tuu kwenya law firms!.

  2. Kama ni mhitimu wa zamani kabla ya sheria ya law school, nakushauri fanya petition, usajiliwe kama wakili ndipo ufanya biashara ya maana zaidi kwa mtaji huo, fungua legal firm yako hapo Mbeya and you'll make it!.

  3. Kama umeshakata shauri biashara ya sheria wewe hapana, then jifanyie utafiti wewe mwenyewe, jee ni biashara gani ina fall kwenye line yako and you are capable to do it within your limited resources?.

  4. Zingatia sana bussiness line yako kwa kufanya kile unaweza. Nakushauri usiige biashara kwa kutazama kwa vile yule ameweza na wewe ni lazima utaweza.

  5. Ukijiona huna bussiness ideas, then just search around common bussiness katika eneo lako ni biashara gani, fanya little research kama inalipa and what it takes, then tia mguu japo mwanzo mgumu.

  6. Kwa haraka haraka 2.M unaweza kuanzisha biashara ya boda boda utainvest 1.8 na kuvuna 20,000 per day baada ya miezi 4, 2.M yako inarudi. Miezi 8 inayofuatia unatengebeza faida ya 4M. unaweza kuamua kuongeza boda boda nyingine 2 hivyo faida ita double na ku triple.
   
 11. Chiwa

  Chiwa JF-Expert Member

  #11
  Aug 15, 2011
  Joined: Apr 17, 2008
  Messages: 1,871
  Likes Received: 1,225
  Trophy Points: 280
  tehee......... tehee......... sipitendi kuwakera watu lakini kwa mazingira niliyopo ningenunua nguruwe mia kwa 20,000 and make money kwa mwezi sita
   
 12. t

  tinya Member

  #12
  Aug 15, 2011
  Joined: Jan 4, 2010
  Messages: 77
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 15
  Ndugu huwa tuna plan ka biashara ka ya kukopa sasa. Kama umekopa kwenye mabenki kama CRDB, NMB maranyingi mazingira ya ulipaji huwa ni mazuri kidogo ukilinganisha na sehemu nyingine.

  Narudia kama umekopa huko, Fuga kuku wa kinyeji, watakulipa sana, ila baada ya miezi sita kama ukiamua kuuza mayai au nyama au vifaranga, kuna aina ya kuku wanatoka huko ni weusi kwa huku tunawaita kuku wa malawi, wanataga mayai 30 kwa raundi moja, ukiwapata hao ni wazuri unaweza kufika nao mbali. Sina uhakika kama wanalalia ila watu ukiwa unauza mayai kwa waanguaji utapata faida nzuri kwa ushauri zaidi tafuta vitabu vya ufugaji.

  Hilo ni wazo langu tu.
   
 13. N

  Nyuki baby Member

  #13
  May 18, 2012
  Joined: Feb 24, 2012
  Messages: 85
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Msaada jamani nataka kufanya biashara nina 1m. Sijui nifanye biashara gani?

   
 14. m

  mbezinho New Member

  #14
  May 18, 2012
  Joined: May 9, 2012
  Messages: 2
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  na mimi nataka kujoin humo kwny business mnasemaje.....sereously
   
 15. OGOPASANA

  OGOPASANA JF-Expert Member

  #15
  May 19, 2012
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 35
  kaka Michael, una ujuzi gani? una elimu gani? unaishi wapi? unapendelea nini? unaishi na watu wangapi? una vyanzo gani vya mapato? una ndoto gani? una udhaifu gani? una uwezo gani? una uelewa gani wa biashara? ulishawahi kufanya biashara yoyote kabla?... Biashara si tu kuwa na mtaji...ujuzi (knowledge) na uzoefu (experience) ni muhimu sana, na wazo la biashara (aina ya biashara unayotaka au unayoweza kufanya) inategemea na unachoweza na unachokipenda. Milioni moja ni mtaji mzuri sana kwa kuanzia biashara ndogo.
   
 16. OGOPASANA

  OGOPASANA JF-Expert Member

  #16
  May 19, 2012
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 30
  Trophy Points: 35
  unaweza kufanya yafuatayo:
  1 - kufanya biashara ya kusambaza bidhaa ndogo ndogo za vyakula ama vinywaji kama vile ubuyu wa zanzibar, crips za viazi na mihogo, mchele, unga, wine, spirits, perfumes nk katika supermarkets, mini supermakerts na maduka makubwa.

  2 - ukapanga eneo na kuweka kibanda kisha ukauza vocha kwa jumla hasa kwenye maeneo yaliyo changamka na yenye wahitaji wengi. Na unaweza kuajiri mtu kama una shughuli zako nyingine.

  3 - nunua mitumba mizuri na ya ukweli ya suruali na mashati ya kiume hasa wa maofisini kisha zisambaze na kuziuza kwa kuzitembeza katika maofisi na maeneo yenye vijana wengi wanaofanya kazi katika maofisi, vituoni nk.

  4 - anza biashara ya kukopesha fedha kwa riba nafuu na marejesho ya muda mfupi (mfano kwa siku, kwa wiki au kwa mwezi)kama LOAN SHARK katika maeneo unayoishi kwa kuwakopesha watu waaminifu na wenye uhitaji kwa makubaliano rasmi ya kisheria (mfano kuandikishiana kwa mjumbe, mwenyekiti wa serikali za mitaa, afisa mtendaji wa kata, mwanasheria, au wakili) bila kusahau wadhamini.

  5 - tafuta mtu muaminifu aliyeko mwanza au ukerewe au unaweza kwenda mwenyewe kuchukuwa aina mbalimbali za samaki wanaopataikana huko kwa bei nzuri na kuja kuuza huko unakoishi. Unaweza kununua bidhaa kama nguo, viatu na urembo katika miji mikubwa kama Dar na kuuza huko (mwanza na ukerewe) wakati unaenda kununua samaki (hivyo utakuwa unaua ndege wawili kwa jiwe moja).
   
 17. P

  Prime Dynamics JF-Expert Member

  #17
  May 19, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 525
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Mkuu kwanza unatakiwa kuwa na idea yako ya biashara. Mimi nadhani kama unataka kusaidiwa, nivizuri kutaja biashara ambayo ungeipenda kuifanya, hapo utasaidiwa mawazo mazuri.
   
 18. REX

  REX JF-Expert Member

  #18
  May 19, 2012
  Joined: Mar 24, 2012
  Messages: 329
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  jaman mi nina wazo la biashara ya mtandao,ni biashara kubwa yenye hadhi ya kimataifa na mtaji wake mdogo hata 1m haifiki.binafsi naifanya na nimeona faida zake.kwa vijana wenye ndoto za mafanikio na wapo tayari kufanya kaz tutafutane.0715720276
   
 19. P

  Prime Dynamics JF-Expert Member

  #19
  May 19, 2012
  Joined: Dec 30, 2010
  Messages: 525
  Likes Received: 22
  Trophy Points: 35
  Je muhusika ataipenda? Na akiipenda anatambuaje risks zake? Na akisha zitambua risks zake atadevelop vipi plan? Mkuu generally ningumu sana to impose your idea to another person. Ni vyema kwanza muhusika ajitokeze na wazo lake la kibiashara.
   
 20. wiseboy

  wiseboy JF-Expert Member

  #20
  May 19, 2012
  Joined: Mar 22, 2011
  Messages: 2,849
  Likes Received: 2,138
  Trophy Points: 280
  mkuu chukua nguo za mitumba grade A Kwa lobota mfano vitop, magauni, mashati ya kiume....then tegeshea wakati wa boom vyuoni mfano SUA, SAUT, MZUMBE, tembeza mzigo chumba hadi chumba...inalipa mbaya...nguo unainunua buku 3 kule unaiuza hd 15
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...