Biashara ya Duka la Jumla

marandu2010

JF-Expert Member
Aug 7, 2010
1,199
435
Habari zenu wakuu,

Hivi biashara ya duka la jumla la vitu mbalimbali inahitaji mtaji wa kiasi gani?

Na inawezekana kumweka mtu na akafanya biashara hii kwa uaminifu na wewe ukaendelea na mambo mengine??,,fikiria huyo mtu si mke wako.

Natanguliza shukurani zangu wakuu..

=====

Hiyo biashara inawezekana ila kabla hujaanza fanya Budget ya Kodi, vitu unavyotaka kuuza na bei zake utakazonunulia .

Vile vile tafuta kijana na weka control kwa kufanya stock taking kila wiki. Kwani tayari utakuwa umempa bei za kuuzia na una jua una stock ya kiasi gani jumla.

Kama kuna upungufu lazima utamuuliza.
 
Habari zenu wakuu:

Hivi biashara ya duka la jumla la vitu mbalimbali inahitaji mtaji wa kiasi gani??? Na inawezekana kumweka mtu na akafanya biashara hii kwa uaminifu na wewe ukaendelea na mambo mengine??,,fikiria huyo mtu si mke wako..

Natanguliza shukurani zangu wakuu.

Duh! swali gumu, unataka kuuza vitu gani? wapi?

Mtu mwaminifu ni ngumu kupata! lazima atapora, tatizo ni kwamba ataiba kiasi gani? Akichukua laki moja tu ujue ameondoka na faida ya siku mbili! teh teh. Niskutishe ndugu, fanya stadi ya soko, angalia mahitaji ya soko na wapi utanunua bidhaa kwa bei gani?
 
Hiyo biashara ina wezekana ila kabla hujaanza fanya Budget ya Kodi, vitu unavyotaka kuuza na bei zake
utakazo nunulia.

Vile vile tafuta kijana na weka control kwa kufanya stock taking kila wiki. Kwani tayari utakuwa umempa bei za kuuzia na una jua una stock ya kiasi gani jumla.

Kama kuna upungufu lazima utamuuliza.
 
Swali lako ni jumla sana.unataka kufanya biashara gani? Lakini biashara zote imara duniani zilianzia chini. Fanya reseach ya kutosha.Kuhusu kumwajili mtu mbali na wife,unaweza.Lakini hakikisha unaweka utaratibu unaoeleweka.

Hasa technolojia km stock database, order software, barcode system, scanning cash registers na Security cameras. Hivi vitakusaidia ku control stock kiurahisi. Pia ukisha jenga uaminifu na masupplier wako utakuwa una place orders online tu,jamaa haitaji kusafiri.

Hakikisha bidhaa zinakuwa na price stickers au weka electronic board price list display, hii itakusaidia kuongeza mauzo kwani itambana muuzaji, asiweze kuongeza bei ya vitu (commission) na kukimbiza wateja. Mwisho lazima uonyeshe tofauti ya ubora wa bidhaa zako na bei. Ila usi-commit murder kwa kutaka kum nyonya manager wako. Mpe mazingira mazuri yako with good pay.

Thank you.
 
Asante sana Tito kwa ushauri mzuri sana,,nitayafanyia kazi mawazo yako na bila shaka utakuwa miongoni mwa watu waliochangia mafanikio yangu ni biashara ya jumla ya vitu mbalimbali vidogovidogo. Once again, asante sana.
 
Ina ugumu wake, mosi risk yakuporwa mauzo, pili wizi wa wafanyakazi, tatu, lazima uwe karibu na benki ili usilale na mauzo. Ningeshauri umuajiri mtu wa karibu unaemuamini. close monitorring is also extremely important, lazima kufunga stock on daily basis. Good capital starting from 15m it can suffice at the biggining. let's talk I run similar business.
 
Asante sana Mwafrica kwa ushauri wako wenye tija, kwa kuwa wewe una fanya biashara hii tutawasiliana sana. Asante sana mkuu Africa. Tuko pamoja
 
Usije jaribu kumwajiri mtu wa karibu.Ajili mtu tofauti mwenye quality (creative na fast learner) ambaye uta mtreat professionally.
Mtu wa karibu utapoteza biashara na undugu.Cha muhimu ni pata reference ya huyo mtu.
 
Ina ugumu wake, mosi risk yakuporwa mauzo, pili wizi wa wafanyakazi, tatu, lazima uwe karibu na benki ili usilale na mauzo. Ningeshauri umuajiri mtu wa karibu unaemuamini. close monitorring is also extremely important, lazima kufunga stock on daily basis. Good capital starting from 15m it can suffice at the biggining. let's talk I run similar business.

Mkuu naweza pata contacts zako maana hii biashara imenijia akilini so I want to try it.
 
Habari zenu bhana, Naomba ushauri jamani, nina mtaji wa Sh. million 8, sasa nimepata idea ya kuanzisha duka la jumla, kwa wenye uzoefu na hii biashara naomba muongozo plzzzz. Sina hakika kama huu mtaji unatoshea. Natanguliza shukran zangu za dhati.
 
Nimejifunza mengi sana hapa. Natoa shukran kwa waliochangia kwan si tu wamemnufaisha muulizaji bali hata sie watazamaji.

Tuko pamoja
 
Kwa shilingi hizo unazozitaja hutaweza kuwa na duka la jumla la maana, sijui unapanga kufungulia wapi lakini kama unaweza kufungua duka la kuuza maji ya chupa na juice za Bakhresa itakuwa afadhali na polepole uongeze bidhaa .hata hivyo mtaji ni mdogo sana.
 
Nashukuru kwa ushauri wako, frame niliyopata rent ni elfu 90 per month tena unalipa kwa miezi sita sita hii ni separate na hyo 8m. Hiyo biashara ya juice ni kwa jumla? au rejareja? challenge ya market ipo vipi maana kama uwa naona magari ya bakhresa yana supply hadi kwenye maduka mitaani!
 
Kwa arusha hiyo ela yako ni kodi ya miezi 8 kwa frem ya duka ! Tafuta namna ingine tofauti na biashara ya jumla!

Mkuu me nipo Dar, na frame nimeshapata ni elfu 90 kwa mwezi tena mwenyew anapokea ya miezi sita sita hii ni mbali na hiyo 8m niliyo nayo ya mtaji.
 
Mkuu me nipo Dar, na frame nimeshapata ni elfu 90 kwa mwezi tena mwenyew anapokea ya miezi sita sita hii ni mbali na hiyo 8m niliyo nayo ya mtaji.

Vizuri sana ukiwa na uhakika kuwa na unacholipa! Kwa mfano arusha ukihitaji frem ya biashara huwezi na hutaweza kumwona mwenye pango kwani huwa kuna madalali tu! Na hata ukimwona huyo mwenye nyumba hawezi kupokea ela yako! Na hii imefanya maduka kupangishwa kwa bei ghali!
 
Back
Top Bottom