Mtaji wa CCM

Inkoskaz

JF-Expert Member
Nov 6, 2010
6,372
2,374
Naliona hili CCM wamelifanya mtaji:-

Uteuzi wa mgombea uraisi kwa tiketi ya CDM imekuwa ni ajenda kubwa kwa ccm na pia wameweza hata kuipenyeza kwa wanaCDM na kuwatumia bila wao kujijua lengo likiwa ni kuleta mfarakano na mgawanyiko ili chama kikose dira na mwelekeo na hivyo kupunguza uelemeo wanaoupata sasa kumjua au kumtambulisha candidate kwa sasa kuna athari na faida zake kama hizi:

Faida
Kutamjenga na kumuandaa kifikra na pia changamoto atakazozipata zitamfanya ajue wapi ana mapungufu ya kuyarekebisha kabla

Athari
Inaweza ikawa ndio kifo chake cha kisiasa ama cha umauti kwani atasakamwa na kuibuliwa kashfa kedekede na hata kuwindwa adhurike, mitego mbalimbali pia itawekwa katika njia yake ili akiteleza ipatikane sababu

Kwa kulijua hilo nadhani CDM wangeliweka hili ndani yamakabrasha hadi muda muafaka ukifika na pia kuwepo azimio la kuzuia wanachama wao kuzungumzia NIA nje ya vikao vya chama

Ni ushauri tu....
 
Ukifuatilia hoja nyingi za akina Nape na thread za Le Mutuz utagundua kusudio lao
 
Zitto alishalitolea ufafanuzi hili kwenye ile exclusive interview kati yake na maswali ya members wa JF wakiwakilishwa na AshaDii. Hili suala kwa sasa ni liability sio asset tena!
 
Umeongea vema! Hata Mimi naliona hilo! Ndio maana CCM wanaanza kupachika wazo la ZK ili kupima upepo! Ni vema CDM ikakaa kimya kwa sasa!
 
Back
Top Bottom