Kaaya10
Member
- Dec 11, 2017
- 37
- 50
Makala ya tatu
Namna ya kupata mtaji wa kuanzisha biashara ndogo au kuongezea palipopelea.
Mtaji na pesa ya kuendeshea biashara yako ni kama damu na oksjeni kwenye mwili wako.
Kuna namna mbalimbali za kupata mtaji zikiwepo;-
• Akiba
• Mtaji kutoka kwa marafiki na wazazi
• Mikopo kutoka taasisi za wakopeshaji
• Wawekezaji wa aina zote
• Misaada kutoka serikalini na mashirika binafsi
Hizi ni baadhi ya njia ambazo zimezoeleka kama vyanzo vya mitaji na zingine nyingi ambavyo unazijua.
Kuna chanzo kingine ambacho nataka kukushauri ukiangalie kwa JICHO LA TATU uone kama pia kinaweza kukusaidia nacho ni MALI AMBAZO HAZIZALISHI zinaitwa DEAD ASSET kwa Kimeru.
Mali ambazo hazizalishi ni mali ambazo unamiliki na manufaa yake kwa sasa ni madogo ukilinganisha na riba zinazoelekezwa na serikali.
Riba elekezi za serikali unaweza kusema ni riba ambazo serikali inatoa kwenye hati fungini zake yaani Treasury Bills and Bonds kwa kimeru. Kwa mnada wa serikali wa 05/05/2021 waliuza hati fungani ya miaka saba kwa riba ya 10.08%, tunawe kutumia hii kama riba ya serikali kwa pesa utakayowekeza kwake ambayo serikali lazima italipa.
Hivyo, kama MALI faida yake ni chini ya 10% ni mali isiyozalisha au imekufa. Unaendaje kukopa mkopo wenye riba ya 30% kwa mwaka wakati unamali unawekuuza ikakusaidia na haizalishi kwa sasa?
Sasa nikuoneshe baadhi ya mali ambazo unazo ukilinganisha na mtaji unaotafuta na hujapata.
• Una viwanja kila kona ya mji na unahangaika kutafuta mtaji wa 10M, hutaki kuuza kwa sababu unaamini kuna siku patakua pa thamani uuze au ujenge, ni sawa lakini je huo mtaji unaotafuta huna Imani kua unaweza ukauzalisha kipindi hicho kikifika ukanunua tena? Kuna miji mipya inafunguka kila siku sio lazima huo mmoja tu.
• Una Tv ya inchi 42 ya tzs 3M na unahitaji mtaji wa 1m, kwanini usiuze hiyo tv 2.5M ukanunua ile ya 700k na ukapata mtaji?
• Umepewa nyuma 3 za urithi zote hazizalishi maana umeshindwa kuziboresha kwanini usiuze moja ukakarabati hizo zingine zikafanya biashara umeacha popo wanaishi huko na wewe unalia huna mtaji?
• Una gari na halizalishi chochote….
• Simu ya 500K una unataka kuanzisha biashara ya matunda ya 300k…. unataka mpaka uwe na friji ya 1M ili uweke maji katoni mbili na matunda ya 20K
• Una vitu vingapi ambavyo kiukweli ukiangalia uzalishaji wake na uwezo wako wa kuifanya hiyo pesa izae Zaidi na baadae ukakinunua tena hicho kitu.
Nimekutajia tu baadhi ya vitu ambavyo unaweza kufanya ukapata mtaji unaohitaji kwa kuanzishia biashara yako. Unaogopa biashara itakufa na kitapotea lakini unataka pesa ya bank au ya mtu mwingine ili biashara ikifa wewe usipoteze, hii ni ishara kua bado hauiamini ndoto yako au hiyo biashara yako kua itafanikiwa, usisumbue kusema huna mtaji, sema hii biashara bado siiamini
Mwanzo 26:18 BHND
Isaka akavichimbua visima vilivyokuwa vimechimbwa wakati Abrahamu baba yake alipokuwa hai, visima ambavyo Wafilisti walikuwa wamevifukia baada ya kifo cha Abrahamu. Akavipa majina yaleyale aliyovipa baba yake.
Kuna fursa imefukiwa, ichimbue. Usikope kwa kufuata Mkumbo, njaa ilipokua kali hata Isaka alitaka kukimbilia Misri kufuata Mkumbo akakatazwa na Roho wa BWANA. Mwanzo 26.
Tafuta Vyombo vilivyowazi (Fursa) ili uvijaze. (Soma Habari yule mjane Mke Wa nabii katika 2wafalme).
Angalia ni kipaji gani ulichonacho na hukitumii vema kwa sasa Anza kukitumia ili uongeze kipato.
Tafakari, jadili.
Nakutakia mafanikio Mema.