Mtafiti Mwandamizi Dkt. Stella Nyanzi atimuliwa Chuo Kikuu Makerere

Influenza

JF-Expert Member
Jul 1, 2018
1,445
3,403
Mtafiti mwandamizi mwenye utata katika Taasisi ya Utafiti wa Jamii ya Chuo Kikuu cha Makerere nchini Uganda, Dk Stella Nyanzi ametimuliwa chuoni hapo kufuatia mabadiliko yaliyowasomba pia wanataaluma wengine 45 katika taasisi hiyo.

Dk Nyanzi aliwekwa rumande katika gereza la Luzira akikabiliwa na mashitaka ya unyanyasaji kwenye mitandao na kumkosesha amani Rais wa Uganda, Yoweri Museveni.

Aliendelea kuwekwa rumande katika gereza hilo Desemba 19, 2018 na ilikuwa aile Krismasi gerezani baada ya kuyakana mashitaka ya makosa ya mitandao akisema hayana msingi.

Kwa mujibu wa Makamu mkuu wa chuo kikuu cha Makerere, Profesa Barnabas Nawangwe amesema idadi kubwa ya wana taaluma hao walioondolewa ni wale waliokuwa watoro kazini kwa zaidi ya miaka mitano huku wengine wakihusishwa na kesi za unyanyasaji wa kijinsia.

Dk Swizen Kyomuhendo ambaye ni mhadhiri wa Shule ya Sayansi ya Jamii naye ameondolewa kutokana na hasara iliyopatikana kwa utendaji uliokiletea sifa mbaya chuo hicho.

Dk Kyomuhendo aliingia matatani baada ya televisheni ya NBS kumhusisha na tukio la kulala na mwanafunzi wake kwa ahadi ya kumpa maksi Februari 26, 2018. Hata hivyo mahakama haikumkuta na hatia kwa makosa hayo.
 
Sema wanasiasa wajanja sana. Inasemekana wabunge na mawaziri ndo wanaongoza kusex na wanafunzi wa universities huko uganda
 
Huyo mama ni tishio kwa serikali ya museveni. Ni mkosoaji sana Wa museveni na serikali yake na anaushawishi mkubwa kwa watu huko Uganda. Ndio maana wamamuweka gerezani. Hata kumtimua kazini yawezekana kumechangiwa pia na msimamo Yake katika utetezi wa haki za RAIA.
 
hivi nyie kama muko na mufanyakazi na akaacha kuja kwa kazi zaidi ya miezi sita bila sababu na wewe kwa uvumilivu wako ukaendelea kumlipa mshahara kila mwezi unaweza vumilia hadi lini???? pili stela nyanzi ni mtu wa kawaida tu hana uwezo wowote wakuofanya serikali itishike
so wote mkae mkao wa kula na muache chuo na serikali vifanye kazi zake
 
Back
Top Bottom