Mtaani wanauliza, kwanini wanaoachiwa ni matajiri wenye kesi za ufisadi?

Serikali ya kulinda vibosire sasa iko madarakani; serikali ya kula na kuwahadaa wananchi sasa iko madarakani; serikali ya maneno mengi na vitendo kiduchu sasa iko madarakani. Serikali ya kutetea ufisadi, rushwa, uhujumu-uchumi, uzembe, upigaji-dili, na ubadhirifu sasa iko madarakani. Uzalendo sasa ni suala la historia. Utetezi wa wanyonge ni historia.

Anyways, tuchape kazi tu kwa bidii maana yajayo yanafurahisha. Kama Mzee Ruksa, Mzee wa Masasi na yule wa Msoga awamu zao zilipita, basi na huyu naye ni suala la muda tu.
Acha ujuha
 
Tutegemee Home Shopping Centre kurudi ulingoni!! Zama hizo zinaelekea kurudi!! Tutegemee Riz 1 kurudia enzi zake!! Zama hizo inaelekea kurudi!! Ila cha kufurahisha ni kwamba Mungu wetu ataipigania nchi yetu!! Wenye tamaa za kuifisadi watakumbana na mkono wa Mungu, ni suala la muda tu!! Mungu amlinde rais wetu na amtie nguvu dhidi ya mafisadi!!
 
Wanafunguliwa ili waje waongeze ajira mtaani.tulifungwa hata waajiri binafsi waliacha kuajiri.tukawa kote kote hatupati.ajira serikalini na private sector pia.

Sent from my Infinix X690 using JamiiForums mobile app
 
Baada ya mfululizo wa kuachiwa huru kwa watu mbalimbali maarufu haswa wafanyabiashara wakubwa.

Mitaani yameibuka maswali mbona maskini walio jela hawaachiwi?

Mbona watoto wa wanyonge wanaendelea kuozea jela!

Mjumbe hauwawi nimeona niwapenyezee namna mitaa unavyochukulia hizi ishu.
Ni kwa sababu CCM ni Chama Cha Mafisadi
 
Baada ya mfululizo wa kuachiwa huru kwa watu mbalimbali maarufu haswa wafanyabiashara wakubwa.

Mitaani yameibuka maswali mbona maskini walio jela hawaachiwi?

Mbona watoto wa wanyonge wanaendelea kuozea jela!

Mjumbe hauwawi nimeona niwapenyezee namna mitaa unavyochukulia hizi ishu.
Braza, tunatawala kutokea Msoga na hii ndio Sera yetu.
 
Vibaraza vya kahawa ndio tunabadilishana mawazo tunaoishi mjini. Na ndio kwenye sauti ya kweli ya watanzania.
Kama hawakutangazwa wakati wana kamatwa unafikiri watatangazwa wakati wanaachiwa. Wapo wengi tu wameachiwa
 
Lakini JPM amejua kunyoosha watu jamani?!

Eti wengine walikuwa akikuta kiwanja popote akakipenda anamrubuni mlinzi anampa hela anamtimua anacolude na maafisa ardhi wanabadilisha hati milki halafu anasema tutakutana mahakamani au baraza la ardhi kwakuwa anahela akifika anahonga anashinda!

Dhuluma kubwa sana.

Mnyonge asinyongwe bali apewe haki yake JPM ameonesha uthubutu wa kunyoosha watu.

Nasema hivi hata sasa watu wakirudia tena kufanya dhuluma,

Atakuja Rais mwingine mwenye kariba ya JPM ataagiza kurudi Miaka ya nyuma makaburi kufukuliwa jamani itakuwa patashika?!

Asomaye na afahamu.
 
Kama kuna waloonewa kuwekwa mahabusu au jera lakini kuna wengine walistahili hizo adhabu.

Machozi ya watu walodhulumiwa mali na haki zao Mungu huwa anajibu kwa wakati
 
Baada ya mfululizo wa kuachiwa huru kwa watu mbalimbali maarufu haswa wafanyabiashara wakubwa.

Mitaani yameibuka maswali mbona maskini walio jela hawaachiwi?

Mbona watoto wa wanyonge wanaendelea kuozea jela!

Mjumbe hauwawi nimeona niwapenyezee namna mitaa unavyochukulia hizi ishu.
Wewe ulieandika uzi huu pamoja na hao watu wako,wote hamsomi magazeti wala kufuatilia vyombo vingine vya habari,kuna sikukuu moja ya kitaifa juzijuzi hapa wametolewa
Wishful thinking.
Rais Mama Samia aliamuru kesi 147 za kubambikwa na TAKUKURU zifutwe.
Akafyeka kichwa cha Mkuu wa TAKUKURU Gen Mbung'o.
Na akaiambia polisi wafanye hivyo.
Huyu Mbung'o ndiye yule mdudu arukaye anayenyonya damu za wanyama pori kule mbuga za Katavi au ni tofauti?.
 
Baada ya mfululizo wa kuachiwa huru kwa watu mbalimbali maarufu haswa wafanyabiashara wakubwa.

Mitaani yameibuka maswali mbona maskini walio jela hawaachiwi?

Mbona watoto wa wanyonge wanaendelea kuozea jela!

Mjumbe hauwawi nimeona niwapenyezee namna mitaa unavyochukulia hizi ishu.
Tafuta pesa sheikh,pesa ndio kila kitu
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom