Mtaani Serikali ya Rais Samia inapoteza uungwaji mkono kwa kasi ya kutisha

Tangu alipokiri kuwa hana uwezo wa kufanya hesabu kama alizokuwa anafanya magufuri nikajua moja kwa moja kwamba hatuna Rais
 
Boss, watu wa mtaani kwako ndio sisi tuko huku JF.

Mtaani hakuna Uhuru, watu wanayasema nyuma ya keyboard.

Enewei, leo nmeyagusa machungu ya Makato sikua mlalamikaji before ila kwa hili la kutuma hela shamba leo nimejua kwa nini Watanzania wengi wanalalamika.
Hicho ulichokijua leo, Mwigulu, Ndugai na hata SSH, hawawezi kukijua, hawatumi pesa kwa simu hao. Hii ndiyo tatizo la kuwa na wawakilishi (wabunge) wa chama pekee kinachounda serikali. Siku zote hoja zinazoletwa na serikali ZITAPITA tu bila hata msuguano wa mijadala. Tutulie dawa ituingie huenda akili zitazinduka.
 
Kwwli tukae kwa kutulia hadi zitukae kichwani
 
Hakuna mtu anamuunga mkono mama samia labda wachache mitandaoni ukianza na Mange na group take ile ya kuupiga mwingi
 
Ngoja Covid travel restriction iishe, nadhani hatakuwa anakaa ofisini. Air Bus 200-300 itakoma
 
Mtaa upi huo kamanda?acheni mama afanye kazi.Hadi sasa anaupiga mwingi,kazi iendelee!
Salamu zimfikie ndugu Samia
Huku mtaani ndugu rais kuna malalamiko, wananchi wanasema hawakusomi, hawakuelewi, na nitakueleza nilichosikia huku mtaani!

1. Suala la tozo za miamala
Wananchi wanakusikilizia tu waone utafanya nini, lakini wameanza kuona dalili za wewe kupiga konakona. Kuna kila dalili ya hasira ya wananchi kuwa kubwa zaidi maana wanaona unawafanya kama watoto wadogo wa kudanganyadanganya

2. Uonevu wa jeshi la polisi juu ya wapinzani
Ndugu rais, sasa badala ya kushawishi kwa hoja, serikali yako imegeuka ya mabavumabavu. Raia kwenye vijiwe vya kahawa, magazeti ya asubuhi wanashangazwa na miguvuguvu yote hii unayotumia, wanauliza unawapeleka wapi?, mbona kila siku polisi wanaokamatakamata wapinzani, wamefanya kosa gani?

3. Kwenye Chanjo watu wanakwenda na kauli ya Magufuli kuwa chanjo hazifai
Binafsi naamini umeleta chanjo kwa nia njema, umefuata ushauri wa kisayansi. Hata hivyo sayansi ni kitu kimoja na perception ya wananchi ni kitu kingine, wananchi mtaani wanaamini kuna hela ya mzungu mmechukua mnatafuta justification. Na hoja ambazo raia wanasema ni kuwa mbona wataalamu waliotwambia chanjo hazifai miezi michache iliyopita ndo haohao leo wanatwambia zinafaa, huko kufaa kumeanza lini. Watu wanaukubali msimamo wa hayati kwenye suala hili na wewe wanakuona kama mabeberu wamekuzidi nguvu

4. Influencers na kundi lililokuwa likikuunga mkono hapo awali linakukimbia kwa kasi
Wapo wale waliosimama kukutetea kwa hatua zako nzuri kabisa mwanzoni mwa utawala wako, watu kama akina Askofu Bagonza, watu wenye ushawishi mkubwa katika jamii. Leo hii wameanza kujidistance na wewe, wanasema mabaya unayoanza kuyatenda kwa kufanya utawala wa kimabavu kupitoa jeshi la polisi yanafuta mazuri uliyoyatenda kwenye siku zako za awali za utawala. Wakati kundi hili likikukimbia, lile kundi linalomkumbuka hayati bado halijakukubali sana, kwa hiyo usipokuwa makini unapoteza uungwaji mkono wa umma hivihivi, Labda uegemeze nguvu zako kwa vijana wa Simon Sirro, lakini hao ni wachache hawafiki hata 50000 nchi nzima, Sijui utawezaje.

5. Miradi ya Hayati hata uisimamie na kuifanikisha vipi, wananchi wanampa credit hayati.
Japo hii binafsi naona wananchi hawana hoja kwa sababu serikali ni taasisi endelevu lakini ukweli ni kuwa huku mtaani bado hawajakuidentify na kitu chako binafsi
Mwanzo raia walisema labda wewe utakuwa mwanademokrasia, mtenda haki lakini mtu wa maendeleo, leo hiyo credit wamekuondolea kwa sababu ya ukandamizaji na uonevu serikai yako inayoufanya kwa wapinzani, lakini wakati huohuo hata miradi unayoebdelea kuifanya (Kitu ambacho ni kizuri) raia wanakuona unakamilisha kazi ya Magufuli. Ukipokea ndege, wanasema ni Magufuli huyo, Raia hawajakuelewa wewe ni Magufuli asiye Magufuli, Au ni Muungwana asiye Muungwana?

Mwisho:
Ndugu rais watanzania ni wapole sana lakini wakikuchukia watakuchukia kwelikweli. TENDA HAKI NA EPUKA UONEVU ili ukistaafu wakukumbuke kwa wema la sivyo watakunyanyapaa sana, Haya madaraka huwa yanaisha na yanapita usijisahau sana!
 
Huyu mama hakua tayari kushika nafasi hiyo nyeti. Mambo ya mipasho kwenye maisha ya watu ni sumu.

Amini nakuambia hakuna hata mmoja anayemuunga mkono. Sio ccm wenzake sio sisi tusio na chama sio kwa wapinzani.

Amegusa pabaya sana tena wakati mbaya ambao watu wanahangaika wapate japo mlo mmoja
Umetumia tafiti gani? Sample yako ya uliowahoji na maeneo yapi?

Ni rahisi wewe kusema haungwi mkono kwa kuandika mawazo yako tu!! Ziko taasisis kama REDET, TWAWEZA na Research International ndizo naweza kuziamini
 
Endelea kuziamini hizo wakati unajua fika maisha halisi yapo huku chini.

Mimi naishi na watu na siishi tu, bali tunajadiliana na kuzungumzia hali halisi za maisha.
Amini nakuambia, mama hana mvuto tena. Yaani amewaacha watu midomo wazi
 
4. Influencers na kundi lililokuwa likikuunga mkono hapo awali linakukimbia kwa kasi
Wapo wale waliosimama kukutetea kwa hatua zako nzuri kabisa mwanzoni mwa utawala wako, watu kama akina Askofu Bagonza, watu wenye ushawishi mkubwa katika jamii. Leo hii wameanza kujidistance na wewe, wanasema mabaya unayoanza kuyatenda kwa kufanya utawala wa kimabavu kupitoa jeshi la polisi yanafuta mazuri uliyoyatenda kwenye siku zako za awali za utawala. Wakati kundi hili likikukimbia, lile kundi linalomkumbuka hayati bado halijakukubali sana, kwa hiyo usipokuwa makini unapoteza uungwaji mkono wa umma hivihivi, Labda uegemeze nguvu zako kwa vijana wa Simon Sirro, lakini hao ni wachache hawafiki hata 50000 nchi nzima, Sijui utawezaje.
Kundi la wanawake ambalo ni kubwa na lenyewe limeanza kupoteza imani na Rais ambaye na yeye ni mwanamke.
 
Kwa jinsi Magufuli alivyotukanwa humu mimi binafsi naona haya yanayoendelea ni sawa tu. Watanzania maneno mengi na hatuna jema
Tozo za simu,
Kupanda maradufu Kwa mbolea na gesi,
Vifaa vya ujenzi vinazidi kupaa,
Mafuta yakupikia hayashikiki. petrol bei juu!.
Sintofahamu kuhusu chanjo ya corona.
Ndio Kwanza asubuhi tutarajie mengi ya ajabu zaidi.
Hata hivyo sisi sio wanyonge tutalipa tu hamna tabu. Wasiotaka wahame nchi!
Lala salama Magufuli
 
Binafsi hata ukifuatilia michango yangu huku utaona nguvu niliyotumia kupambana na MATAGA waliokuwa wanampinga mama. Ila sina hata hamu nae tena.
 
Umejaribu kuongea nao? Au ulitaka kila ukipita uwe unasikia habari za tozo....tozo....tozo...

Ukitaka kujua watu wanatembea nayo, jaribu hata kumuongelesha yeyote kuhusu mtazamo wake juu ya hizi tozo mpya za uzalendo.

Alafu uje uniambie ni wangapi wanasema imekaa vizuri na inatekelezeka.

Pia huenda unajitenda na watu ndio maana huwezi kusikia
dini mkuu imewa-blind, watu wanamtetea kwa sababu ni dini yetu na sio vinginevyo!

huyu jamaa uliyem-quote sijaona popote akimkosoa huyu mama, yeye ni sawa kila kitu!
 
33 Reactions
Reply
Back
Top Bottom