Mtaani nakoishi wanahisi nauza dawa za kulevya kutokana na maisha nayoishi

Yofav

JF-Expert Member
Mar 12, 2021
3,940
6,835
Habarini Ndugu, Jamaa na Marafiki Mliopo JF

Bila kupotezea muda nataka kueleza kwanini nimeandika kichwa Cha habari chenye mshangao ndani yake.

Mimi Ni kijana mwenye umri wa miaka 21 sasa, Najishughulisha na biashara zangu za mapambo ya ndani. Biashara hii Nina uzoefu nayo kwa miaka minne sasa Nina Duka na pia nimeweka mtu wa kulisimamia na kutokana na technology kukua kwa Sasa nina nina uwezo wa kutafuta wateja mtandaoni na kuwapata hivyo imenirahisishia kiasi kwamba sasa ninajiamulia muda gani niende kazini na muda gani nisiende. Note:

Kukaa kwangu nyumbani hakunipunguzii chochote kwani dukani Kuna mtu wa kusimamia na pia niwapo nyumbani nakuwa busy kupost matangazo na kupromote ili kutengeneza wateja wengi zaidi hivyo unakuta jioni ndo hua naelekea dukani kufunga hesabu au nikitoka ujue Kuna mteja kahitaji mzigo na delivery service.

Hivyo unakuta ndo naenda dukani kuchukua mzigo na kumpelekea au kutuma Mkoani Kisha narudi zangu home kuchill. Na hivyo ndivyo ninavyoendesha maisha yangu.

Sasa kilichofanya niandike huu uzi ni kwamba kuna mtaa nimehamia sina muda mrefu sana (Nina miezi mi5) Sasa nadhani watu wa mtaani (majirani) hawajanielewa Lifestyle yangu.

Maana wanaona ninapoishi Pana hadhi kidogo then hawajui nafanya ishu gani then most of the time nakuwa home tu alafu maisha yangu yanaenda tu, Sikuwahi kujua kama kumbe kuna watu wananinasia muda tu.

Hadi jana kuna mtu kaja kimasihara tu kanikuta nje nafuafua tu tukasalimiana ndipo akaniuliza "Hiv bro we unafanya ishu gani?" nikamuelezea mwanzo mwisho akashangaa Sana ndipo akaniambia "Ujue mtaani habari zako Ni kwamba unauza madawa ndio maana maisha yako yanaenda"

Dah! nilishangaa sana ndipo nikasema nilete huu uzi kwenu.

Kumbe mtu unaweza ukawa busy na mambo yako kumbe watu wanakuchora tu.
 
Hisia za watu ni ktu cha kawaida Mimi niliitwa mpelelezi kutokana na tabia yangu ya kutokua muongeaji hivyo huwa nafika vijiweni alaf nakaa kimya kuskiliza stori bila kuchangia mada
Duh!
 
Back
Top Bottom