Mtaani kwetu na vituko vya paka mweusi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mtaani kwetu na vituko vya paka mweusi

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by NasDaz, Oct 4, 2010.

 1. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #1
  Oct 4, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280

  Wahenga wa Kizungu wana msemo wao; eti " A blck cat may be a bad luck ONLY if you are mouse!" Chambilecho waungwana, kama wewe si panya, ya nini kumwogopa paka mweusi?!

  Nataka kuzungumzia kauli ya Msemaji wa JWTZ, Bwana Abdulrahman Nyimbo! Kauli ya Bwana Shimbo inanikumbusha vituko vya mtaani kwetu. Sisi tuishio ushenzini, yaani uswahilini ++ hatukosi kushuhudia vituko kila uchao! Siku moja tukiwa kijiweni, jirani na hapo kulikuwa na akina dada wanne waliokuwa wakisukana nje ya dirisha la nyumba moja! Wakati wakiendelea kusukana; mara alipita dada mmoja jirani kabisa na akina dada waliokuwa wakisukana! Alipowapita tu; mara akina dada waliokuwa wakisukana waliangua kicheko cha kipashikuna au kishambenga ukipenda! " haloo! Haloo! Utamaliza wanaume wa mtaa mzima sasa!" Dada mpita njia hakujali wala kushituka! Huyooo, akaendelea na hamsini zake!Akapita dada mwingine; akina dada wasuka nywele nao wakaendeleza mchezo wao-vicheko vya kipashikuna! Huyu nae, hakujali, hakugeuka wala kushituka! Nae, kama ilivyokuwa yule wa kwanza akaendelea na hamsini zake!

  Dakika chache baadae, akapita dada mwingine! Kama ilivyokuwa awali, akina dada wasukana nywele nao wakaangua tena kile kicheko chao cha kishambenga! Mungu wangu! Dada huyu wa sasa akaja juu, kheri ya moto wa kifuu! Dada wa watu akafura kwa hasira na kisirani, mithili ya faru majeruhi! Akatokwa na povu mdomoni mithili ya ng'ombe dume lililokumbwa na ugonjwa wa sotoka(rindapest)! Ndani ya sekunde chache, akaporomosha mvua ya matusi ya nguoni iliyomfanya kila aliyekuwa pale kijiweni atafute kwa kuficha sura yake! Nilitamani ningekuwa kobe, ili nizame ndani ya gamba langu; lakini haikuwezekana! Akina dada wasukana nywele nao wakabaki kimyaa; macho yamewatoka mithili ya mjusi aliyebanwa na mlango!

  Kuja kutanabahi, ukweli ukadhihiri! Kumbe akina dada wasukana nywele wala hawakuwa wakimcheka yule dada mpita njia! Walikuwa wakimchamba dada jirani yao aliyekuwa akiishi kwenye nyumba ile ile ambayo wao walikuwa nje wakisukana nywele! Inasemekana dada jirani yao alikuwa na tabia ya kutembea(kujivinjari) na waume na ma-boyfriend wa majirani zake!

  A black cat may be a bad luck only if you are a mouse!


  Kwa muda sasa, CCM wamekuwa wakiwatisha wananchi kwamba endapo wapinzani wataingia madarakani basi vita itazuka nchini! Ninavyofahamu mimi; anayeanzisha vita ni yule aliyeshindwa kwenye uchaguzi na sio yule aliyeshinda uchaguzi! Ya nini aanzishe vita wakati ameshinda?! Hivyo basi, endapo upinzani ukishinda uchaguzi basi vita itazuka nchini; basi ni dhahiri kwamba watakaoanzisha vita hiyo ni CCM kwavile wameshindwa uchaguzi na wao hawapo tayari kushindwa! Sasa inakuwaje Dr. Slaa aje juu kutokana na kauli ya Meja Abdulrahman Shimbo?! Bwana Shimbo hakutaja jina la chama chochote kwamba wanaelekea kutokubali matokeo ya uchaguzi! Hata hivyo, CHADEMA wakaja juu kufuatia kauli ya Bwana Shimbo!!

  Am afraid kwamba, a black cat may be a bad luck only if you are mouse!!! Busara zenu zimeenda wapi? Nilitarajia kwamba, endapo busara ingetumika, basi Dr. Slaa angejibu hivi "Tumefurahishwa sana na kauli ya majeshi yetu ya ulinzi na usalama kupitia kwa Bwana Shimbo! Kwa muda mrefu sasa, CCM wamekuwa wakiwatisha wananchi kwamba endapo CHADEMA itaingia madarakani, basi vita itazuka nchini! Ninavyofahamu mimi, na hivyo ndivyo inavyokuwa; mtu aliyeshinda uchaguzi hawezi kuanzisha vita bali yule aliyeshindwa kwavile hakubali kushindwa! Hivyo basi, CCM kuwatisha wananchi kwamba CHADEMA ikiingia madarakani vita vitazuka nchini; hiyo inadhihirisha wazi kwamba CCM hawatakubali matokeo ya wao kushindwa kwavile wakishindwa tu, wataingia msituni na kuleta vita nchini!"

  Hata kama JWTZ kupitia Bwana Shimbo walikuwa wanawalenga CHADEMA basi jibu hilo hapo juu lingewaacha shushu! Lingewaacha shushu kwavile badala ya kupata negative reaction kama walivyotarajia (kama ambavyo Dr. alivyowajibu) wangejikuta wamepewa positive reaction! Ni kama mtu anayekupiga masinge kichwani huku akitarajia utakasirika ili mzichape, badala yake anakuta ndo kwanza unacheka! Meja Shimbo na wenzake ni watu makini hivyo jibu hilo lingekuwa ni bakora zaidi kwao kwavile wangejuwa kwamba si jibu la moyoni bali ni bezo!

  Wakati mimi nataraji Dr. angetumia udaktari wake na kujibu kwa busara, Dr. Slaa na wenzake wakaja juu dhidi ya kauli ya Bwana Shimbo mithili ya yule dada mpita njia wa tatu! A black cat may be a bad luck only if you are mouse! Otherwise, wala sioni sababau ya kwanini Dr. Slaa aje juu dhidi ya kauli ya Bwana Shimbo kwa madai kwamba kauli hiyo ina lengo la kuibeba CCM na kuwatisha wananchi! Binafsi, naona kauli hiyo sio vitisho bali ni tahadhali! Madai kwamba JWTZ wanajiingiza kwenye kazi ya jeshi la polisi nayo hayana mashiko kwavile moto ukilipuka watakaokuwa na wajibu wa kuuzima ni JWTZ na wala sio polisi! Madai kwamba kazi ya JWTZ ni kulinda mipaka ya nchi nayo hayana msingi wowote!

  A black cat may be a bad luck only if you are a mosue!
   
 2. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #2
  Oct 7, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  mkuu, dr slaa sio mtu wa kuchaguliwa cha kuongea labda kama umetumiwa
   
 3. N

  NasDaz JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2010
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 11,308
  Likes Received: 1,651
  Trophy Points: 280
  Napata taabu sana ninapokutana na jibu lililojaa busara lakini sipati shida hata chembe ninapokutana na jibu la aina yako! hapo hapo nafahamu jibu hilo limetoka kwa m2 wa aina gani!
   
Loading...