Mtaani kuna pesa nyingi sana inayotafuta wahitaji

Biashara ya kwenye makaratasi shida sana aise.

Ila Hongera kwa kupata milioni 1.8 kwa siku 20 tu.

Na imani utakata kiu ya Mh. Raisi naona ubilionea unakusogelea kwa kasi ya ajabu.
 
Sasa namuelewa sana JPM !

Jamani mtaani kuna pesa nyingi sana ambayo haina pa kwenda. Inatafuta mwenye uhitaji , ipo nyingi sana.

Ukiwa mbunifu (creative), mjanja na mhangaikaji hukosi pesa , tena nyingi tu. Ukiumiza kichwa ukachapa kazi (bila ubaguzi) unapata pesa tena kiulaini kabisa.

MAHINDI YA KUCHOMA

Hindi moja nimekuwa nikinunua kwa TZS 50 mpaka 100 shambani kulingana na wingi wake.

Nikishalifikisha mjini umbali wa 20 km nikalichoma , naliuza TZS 500 hadi 600.

Nikinunua mahindi 200 nitauza TZS 120, 000.

Matumizi:

Bei ya kununulia ni TZS 20,000 ; Usafiri 3,000 ; nauli yangu 3, 000 ; mkaa TZS 2,000. JUMLA YA MATUMIZI NI TZS 30,000 per day

Faida = 120,000 - 30,000 = 90,000 per day.


Kwa siku 20 = 1,800,000.


Endelea kudai kupandishwa madaraja na nyongeza ya mshahara mpaka Yesu arudi.
Muda wako wa kufanya hizo shughuli , umeuthaminisha!!!... huo mkaa utakuwa unauweka kichwani unachomea mahindi eti..??... Umeweka gharama za Ushindani/mshindani wako maana sio kila mara utauza hizvyo kutokana na ushindani?? vitu ni vingi aseee usirahisishe mpango biashara kama vile ni shughuli ya kwenda maliwato.
 
kuna muuza mahindi mmoja anachoma maeneo ya mbezi beach huko nilikaa nikapiga nae story mbili tatu kwa upande wake anasema inamlipa nikafikiria kweli lakini akawa ameniongezea maarifa.

tatizo ni watu tunawaza sana viwango vya elimu tulioipata na kazi tunayoenda kuzifanya au unazoambiwa kuzifanya
kwa uhalisia ukiwaaliza hata wananchi wa nchi zilizo endelea hasa wana vyuo wa nchi zinazoendelea mtu anasoma major yake ila hana hata mpango wa kufanya kitu anachokisomea ana enda kusimamia sehemu anayo ona kuja fursa
 
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom