Mtaalamu wa uchumi (CCM) apigia chapuo sera ya CHADEMA ya serikali ndogo

Jatropha

JF-Expert Member
Apr 9, 2009
1,151
199
katika gazeti la guardian la leo tar 09 nov 2010 mtaalamu wa uchumi mmoja amepigia chapuo sera za chadema za kuwa na serikali ndogo na akatoa takwimu ya jinsi serikali ya jk ya muhula wa kwanza 2005-2010 ilivyokuwa na gharama kubwa za uendeshaji kiasi cha kuathiri utoaji wa huduma za jamii na maendeleo kwa ujumla.
 
mhh haya yatamwingia mkwere kweli? Ninapata wasiwasi na hii elimu yake ya uchumi,ndiyo maana mwandishi wa habari BMW mkapa was good kwenye uchumi kuliko hata msomi wa uchumi wetu!
 
tatizo ni kulipa fadhira, akiweka wizara chache ina maana kuna maswahiba zake alishawaahidi uongozi watakosa
 
Baada ya kutoka darasani, Kikwete hajawahi kupractice economics; alikuwa kamisaa wa jeshi na mpelelezi siku zote. Kwa hiyo anajua sana porojo na kufanya upelelezi namna ya kuwabana wapinzani wake.
 
Tatizo lina kuja maswahiba wake atawaweka wapi ?? kama akiweza kupunguza baraza la mawaziri tutegemee ufisadi mkubwa kuliko uliopita maana kuna mengi ya kulipwa kwa mafisadi ikiwemo kuwapa vyeo kama hilo halipo basi tenda zote zitatolewa kifisadi kufidia donations zao kwa jk.
 
hahahahaa! Home Economics;
Jamaa anasema, "this is the only way he can moderately meet his promises to wananchi"
 
Hlafu watu bado walikuwa wanamuamini muungwana na miahadi yake ya aliyokuwa anaitoa wakati wa kampeni!!!! Tuanze upya serious!
 
Ebwana iko safi jamani,huyo kada wa CCM nadhani alifuatilia sana kampeni za Dr Slaa. Maana aliyoandika humo ndio ulikuwa msistizo wa Dr Slaa.
 
Faili limegoma kufunguka..sijui ni kwanini?

Soma Guardian Ukurasa wa 11
moz-screenshot-2.jpg
moz-screenshot-3.jpg
 
Kwa kweli watanzania miaka hii mitano ijayo tutajuta kwanini tulimchagua jk coz mafuta yameanza kuadimika pia yamepanda bei mfuko wa bei umeanza kwa kasi zaidi nguvu zaidi na hari zaidi pia huduma muhimu kwa jamii zemeaza kuwa adimu,kwakweli sijui tutaenda wapi niliye mpa kura yangu kachakachuliwa,nadhani pale mungu alipo waambia wana waisraeli nimewawekea uzima na mauti chagueni uzima mkaishi au mauti mkaangamie ndo haya yanatokea tanzania leo watu wameukataa uzima wamechagua mauti wanasema baraba mwenye dhambi aachiliwe huru bali yesu asiye na kosa lolote asulubiwe na kuuawa watu wamemkataa slaa mkweli wamechagua jk muongo wamemkataa docta wa kweli wakamchagua kanali dokta wa mezani,madhara haya tunayoyaona sasa ni matokeo ya uchaguzi wetu mbaya uliopita waache watanzania wale fimbo ya mungu kwanza ndo miaka mitano ijayo wajue kuchagua chema na kukitema kibaya.hilo nalo neno sina maana hiyo!
 
Nimekuwa nikifuatilia kampeni za CHADEMA pamoja na mikutano yao ya hadhara, sijawahi kusikia mkakati wao kuhusu jinsi ya kukuza uchumi wa TZ, wimbo mkubwa wa CHADEMA ni ufisadi, sana sana namsikia mwenyekiti wao akiongelea siasa za majimbo. Kuna mfumuko mkubwa wa bei, sijawahi kumsikia katibu mkuu wa CHADEMA au hata mwenyekiti wakizungumzia ni jinsi gani wao wakiingia madarakani watakabili suala la mfumuko wa bei,kukuza kipato cha Mtanzania, ni jinsi gani watafanya hili taifa lijitegemee. Kuzuia UFISADI sio suluhisho pekee la uchumi wetu. Tunataka CHADEMA watuambie wataboreshaje maisha ya Mtanzania. Embu ona mtu kama Edwin Mtei ambaye ndie mlezi wa CHADEMA, kwanza huyu mzee anamiliki mashamba Meru wakati watanzania hawana mashamba, juzi juzi katoa maneno ambayo nisingetegemea mtu kama yeye kutamka, eti tume ya uchaguzi ina waislamu wengi kuliko wakristo.

Vijana wengi wa Tanzania wanamatarajio makubwa sana ambayo siyo realistic wanafikiri CHADEMA wataibadilisha hii, nawahakikishia hakuna mabadiliko yoyote yatakayoletwa na CHADEMA.
 
peleka magamba yako kule huna lolote you trying to cheat but you wil never succeced. Yaani unachekesha hujawai kusikia na huwezi kusikia maana uko aganst
 
Nadhani unafuatilia mambo nusu nusu. CHADEMA kupitia kwa mawaziri vivuli, walitoa 'alternative' budget kwa kila wizara. Na Zitto kama waziri kivuli wa fedha alieza vizuri nini kifanyike ili kuinua uchumi. Hivyo kwa kila wizara CHADEMA walitoa michango/maoni yao. All you have to do kama kweli una nia njema ya kujua sera na mikakati ya CHADEMA kuhusu uchumi etc ni kusoma (a) ilani yake ya 2010 na (b) kupata hansard.

Hata hivyo ni vema ukatambua relationship iliyopo kati ya UFISADI na Ukuaji wa uchumi. Ukishindwa kuelewa hili basi lazima utaona kuwa CHADEMA hawana sera!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom