Mzito Kabwela
JF-Expert Member
- Nov 28, 2009
- 18,857
- 7,615
Nimekuwa nikifuatilia kampeni za CHADEMA pamoja na mikutano yao ya hadhara, sijawahi kusikia mkakati wao kuhusu jinsi ya kukuza uchumi wa TZ, wimbo mkubwa wa CHADEMA ni ufisadi, sana sana namsikia mwenyekiti wao akiongelea siasa za majimbo. Kuna mfumuko mkubwa wa bei, sijawahi kumsikia katibu mkuu wa CHADEMA au hata mwenyekiti wakizungumzia ni jinsi gani wao wakiingia madarakani watakabili suala la mfumuko wa bei,kukuza kipato cha Mtanzania, ni jinsi gani watafanya hili taifa lijitegemee. Kuzuia UFISADI sio suluhisho pekee la uchumi wetu. Tunataka CHADEMA watuambie wataboreshaje maisha ya Mtanzania. Embu ona mtu kama Edwin Mtei ambaye ndie mlezi wa CHADEMA, kwanza huyu mzee anamiliki mashamba Meru wakati watanzania hawana mashamba, juzi juzi katoa maneno ambayo nisingetegemea mtu kama yeye kutamka, eti tume ya uchaguzi ina waislamu wengi kuliko wakristo.
Vijana wengi wa Tanzania wanamatarajio makubwa sana ambayo siyo realistic wanafikiri CHADEMA wataibadilisha hii, nawahakikishia hakuna mabadiliko yoyote yatakayoletwa na CHADEMA.