Mtaalamu wa mifugo (Dr. by Veterinarian): Karibuni kwa ushauri, tiba na dawa za mifugo tu

Dr kwema vp nawezaje kupata mbegu ya mbuzi wale wanaozaa mapacha na je inawezekana nikawapandikiza mbuz hawa wa kawaida wakazaa mapacha?
 
Dr kwema vp nawezaje kupata mbegu ya mbuzi wale wanaozaa mapacha na je inawezekana nikawapandikiza mbuz hawa wa kawaida wakazaa mapacha?
Ulzia kuna mbuz wanaitwa buha hio breed inapatikan sana maeneo ya kigoma wanauwezo wa kuzaa mpk mapacha watatu wanaweza kukusaidia kweny biashara yako
 
Habari mkuu, mbwa wangu kapoteza sauti, tatizo ni nini mkuu. Yani akibweka sauti inakuwa kama mtu mweny kikohoz vile
 
Dr.kwema...samahani naomba unisaidie nna kuku wa kienyeji nawafuga nusu huria wamevamiwa na ugonjwa wa ndui na nna vifaranga havijafikisha mwezi...unanishauri nini cha kufanya?
 
Mkuu vifaranga unaweza kuvilea kwa kutumia;

1. Charcoal brooder ( vyungu maalamu vinavyotumia mkaa )
- Kwa kawaida vinaweza chungu kimoja kinaweza kulea vifaranga mia moja, faida yake unatumia rasimali mkaa ambao ni rahisi kupatikana.

- Hasara yake ni kuwa itakulazimu kila baada ya masaa 2-3 kwenda kuongeza mkaa na pia hakikisha madirisha yako huyafungi yote kuruhusu hewa safi kuingia ili kuondoa hewa chafu ya carbonmonoxide inayozalishwa na mikaa.

2. Infared light bulb (balbu maalumu za umeme)
- Hizi huwa zinakuja na rangi nyekundu na ni malaamu kwa ajili ya kulelea vifaranga, taa moja ina uwezo wa kulea vifaranga 200.

- Faida yake ni kwamba inatoa joto stahiki kwa vifaranga, na pia haizalishi hewa chafu kama mkaa kwa hiyo ukiwasha huna haja ya kuamka usiku kwenda kukagua vifaranga.

- Hasara yake ni kuwa inatumia umeme mwingi kiasi na bei yake ni 50000 kwa taa moja.

3. Gas brooder ( Bruda ya gesi )

- Hii ni maalamu kwa ajili ya kulea vifaranga kwa kutumia gesi hivyo ni ghali kiasi na bruda moja ina uwezo wa kulea vifaranga zaidi ya 1000 na pia ni nzuri una uhakika wa kuvuna vifaranga vyako vyote kwa sababu haitoa hewa chafu.

NB: Hapo sasa ni wewe kuangalia mfuko wako unasemaje mkuu.
Shukrani Dr. Kwa maelekezo mazuri sana. Hizi Infra red light bulbs naweza pata kwenye Agrovet stores, ama ni kwenye maduka ya vifaa vya umeme?
 
Habari Mkuu, pole kwa kuuguliwa na mfugo wako ningependa kujua ulitumia njia gani kupima na kujua huyo ng'ombe yuko na Anaplasmosis ( Ndigana baridi) na Ulihakikisha vipi kuwa ng'ombe wako alipona ECF ( ndigana kali) na pia inaweza kuwa babesios.

Najua watu wengi huwa wanachanganya hayo magonjwa wakati wa kufanya diagnosis unaweza kuta unatibu anaplasmosis kumbe mfugo wako ana ECF..

Ndio maana dalili ni muhimu sana wakati wa kufanya diagnosis na dalili ukiwa expect mzuri unaweza kuwa correct kwa 60 % ila vipimo vya maabara ni 100%

Hivyo basi kama uko na uhakika ni anaplsmosis kweli jaribu kubadili dawa na tumia dawa hizo hapo chini;

View attachment 1105279


Me naomba nisaidie hiyo pdf mkuu ninauhitaji nao mkubwa, au nielekeze naipataje.

Natanguliza shukran,.
 
Ni sahihi mkuu unaweza kumkamua ila pia sidhani kama achelewa inawezekana anapata silent heat we unashindwa kuona kawaida wastani wa kupata joto kwa ng'ombe ni siku 21 (18-24) .
 
Habari !

Ngombe wangu Wana tatizo . Kwanza walikua wanamimba wote wawili , then zlivofik miez minne - mitano zikatoka wote .

Baada ya hapo wamekua wakiingia joto lakin kila nkiwapandisha hawashiki mimba wote na ndama wao wameshakua wakubw wanakaribia mwaka, still ngombe bado wanakamuliw .

Tatzo langu ni kwanini hawashiki mimba wote kila wakipandwa . Nimewapandisha Kama Mara nne hivi .

Asanteni

nb: hao waliotoa mimba ndo hawashiki sahivi mwenzao mwingne yeye hakutoa mimba yake ni kubwa sahiv
 
Anaejua kifaa kinaitwa PIG SNARE kinauzaa bei gani na naweza kukipata wapi msaada please
Hiki kifaa unaweza kukipata kwenye duka la kuuzia dawa na bidhaa nyingine za mifugo. Bei yake ni kati ya Tsh 50,000 hadi 80,000 kutegemeana na mahali ulipo. Mwaka juzi nilinunua kifaa hiki farmbase kwa Tsh 50000 tu. Karibu mkuu.
 
Habari
Nina ng'ombe anajisaidia kinyesi chepesi muda sasa nawenzake kinyesi chao kizuri kiko kawaida.pia macho yake anayatoa sana mpaka yanaonekana makubwa kuliko kawaida.pia anakohoa kohoa.naomba msaada juu ya hili suala
 
Anakohoa na kutoa aina ya hicho kinyesi kwa mda gan?
Habari
Nina ng'ombe anajisaidia kinyesi chepesi muda sasa nawenzake kinyesi chao kizuri kiko kawaida.pia macho yake anayatoa sana mpaka yanaonekana makubwa kuliko kawaida.pia anakohoa kohoa.naomba msaada juu ya hili suala
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom