Mtaalamu wa mifugo (Dr. by Veterinarian): Karibuni kwa ushauri, tiba na dawa za mifugo tu

asante sana. Looks this dawa is very expensive. How much does it cost in dar? Naweza kumchoma leo dose moja, then ingine nikatafuta ya bei nafuu Dar. I am in Tanga
300 x 5= 1500/120= 12.5 mls needed. Each meal is 2500 Tsh! .....12.5 x 2500= 31,250 Tsh. Vial nzima ya 50 mls is 75,000 Tsh
Sina uhakika sana wa bei maana dawa za mifugo awamu hii zimepanda sana, ila nahisi itakuwa kwenye 65,000 kwa chupa ya 50ml.

Pia inawezekana, ila kama inawezekana waweza mpa OTC 20% plus multivitamins hakikisha dawa ya OTC ni kutoka kampuni ya Norbook or Laprovet ndio effficacy inakuwa juu.
 
Unapatikana wapi mkuu? Huduma ipo hiyo tutafanye kubadilishana mawazo then tupange siku ya kuja kumfanyia Ovariohysterectomy (OH) paka wako.

Ahsante.
Najaribu kukuandikia kwenye private msg lakini system inagoma inataka niongeze (recipients 2). jaribu kuni- pm
Au nitumie namba/ email yako
 
Habari, kwa swali lako Majani ya Lucerne ndio hutumika kama moja wapo wa vichanganyo katika chakula cha nguruwe hasa kutengeneza chakula cha GROWERS na FINISHER.

Zifuatazo, ni sababu za kwanini lucerna hutumika kama moja wapo ya vichanganyo katika chakula cha Nguruwe.

(1) Majani hayo huwa na kiwango kikubwa cha protein ambacho ni kati ya 20-22% na katika chakula cha kukuzia nguruwe huitaji kiwango cha protein 18% na katika kumalizia au fattening huitaji kiwango cha protein 14%, kwa maana hivyo waweza ona ni kwa kiwango gani majani hayo yalivyo na umuhimu katika kujenga mwili wa nguruwe.

(2) Majani hayo yana kiwango kikubwa cha madini na vitamini na kama ikitokea yakavunywa mapema huwa na kiwango kizuri pia cha nishati na fibres. Ambazo ni muhimu sana katika ujenzi wa mwili wa nguruwe.

Zingatia; Kipimo cha lucerna katika mchanganyiko hutegemea na malighafi ulizonazo.
Mkuu naomba nisaidie ratio ya mchanganyiko wa lucerna katika chakula inakuwaje!,kama kuna formula nitashkuru kama utanisaidia,pia naulizia kama naweza kuchanganya lucerna na azolla kwa mara moja?
 
Sina uhakika sana wa bei maana dawa za mifugo awamu hii zimepanda sana, ila nahisi itakuwa kwenye 65,000 kwa chupa ya 50ml.

Pia inawezekana, ila kama inawezekana waweza mpa OTC 20% plus multivitamins hakikisha dawa ya OTC ni kutoka kampuni ya Norbook or Laprovet ndio effficacy inakuwa juu.
Hapa mkuu, ni kuhusu kuku wangu, kesho wananipiga wiki tatu so naweza wapatia Ile vitamins ulioniambia sio?
 
Naomba kuuliza kwamba kuku wakishatotoa unawanyan'ganya vofaranga so hivyo vifaranga unatumia joto gani kuvilea
Mkuu vifaranga unaweza kuvilea kwa kutumia;

1. Charcoal brooder ( vyungu maalamu vinavyotumia mkaa )
- Kwa kawaida vinaweza chungu kimoja kinaweza kulea vifaranga mia moja, faida yake unatumia rasimali mkaa ambao ni rahisi kupatikana.

- Hasara yake ni kuwa itakulazimu kila baada ya masaa 2-3 kwenda kuongeza mkaa na pia hakikisha madirisha yako huyafungi yote kuruhusu hewa safi kuingia ili kuondoa hewa chafu ya carbonmonoxide inayozalishwa na mikaa.

2. Infared light bulb (balbu maalumu za umeme)
- Hizi huwa zinakuja na rangi nyekundu na ni malaamu kwa ajili ya kulelea vifaranga, taa moja ina uwezo wa kulea vifaranga 200.

- Faida yake ni kwamba inatoa joto stahiki kwa vifaranga, na pia haizalishi hewa chafu kama mkaa kwa hiyo ukiwasha huna haja ya kuamka usiku kwenda kukagua vifaranga.

- Hasara yake ni kuwa inatumia umeme mwingi kiasi na bei yake ni 50000 kwa taa moja.

3. Gas brooder ( Bruda ya gesi )

- Hii ni maalamu kwa ajili ya kulea vifaranga kwa kutumia gesi hivyo ni ghali kiasi na bruda moja ina uwezo wa kulea vifaranga zaidi ya 1000 na pia ni nzuri una uhakika wa kuvuna vifaranga vyako vyote kwa sababu haitoa hewa chafu.

NB: Hapo sasa ni wewe kuangalia mfuko wako unasemaje mkuu.
 
Ahsante sana Dr na hii njia ya tatu amvayo ni gesi garama ipoje
Mkuu kwa gharama ya gesi bruda zinatofoutiana mara nyingi ya kawaida ni kuanzia milioni moja na kuendelea mara nyingi gesi bruda hutumiwa na wale wajasiliamali wakubwa au makampuni maana ni gharama kiasi mtungi wa gesi wa kilo 100 unaisha ndani ya siku 3 hadi 4 mkuu.

Kama wewe ni mzalishaji wa vifaranga wa kawaida chaguo sahihi kwako ni namba (1) na (2) ila infred light bulb ni nzuri sana mkuu.
 
Habari me no mgeni humu ila katika maisha yangu Nina ndoto ya kufuga kuku wa kienyeji pamoja na bata vp kuna hatua zozote nazopaswa kuzichukua ili kuepukana na changamoto mbalimbali
 
Habari Wakuu....
Nipo mbele yenu kujibu maswali yenu mbalimbali kuhusiana na tiba na ushauri wa magonjwa yanayosumbumbua mifugo yetu mbalimbali na hivyo
Habar mkuu,nauliza kuhusu uduvi unaopatka kwenye dagaa,je unaweza kufaa kama chakula Cha kuku na vifaranga? Maana Kuna baadhi ya watu wanadai husababisha magonjwa kwa kuu na hasa vifaranga nao huvimba kichwa na kufa,naomba ufafanuzi juu ya hili,na kama s kwel ni matumiz yap sahh ya uduvi hufaa kwa kulisha kuku
 
DR. ngombe wangu anaugua mastitis, nikamuita daktari, bila kuniambia akamchoma dexamethazone. sasa maziwa yote lita 10 a day yamekauka. Nifanyeje?

Kwa sasa namtibu na penstrep na intramammary. Nimemuita dakitari mwingine anampiga 40 mls , 20 each site. Is this proper?
tafadhali nisaidie.
 

Similar Discussions

36 Reactions
Reply
Back
Top Bottom