Mtaalamu wa mifugo (Dr. by Veterinarian): Karibuni kwa ushauri, tiba na dawa za mifugo tu

Jamani mbona kimekomaliwa kitu kidogo sana ikilinganishwa na thamani ya ushauri wa kitaalamu anaoutoa huyu ndugu yetu tena kwa bure kabisa? Wewe kama hufugi hata kuku jikate uende kwenye majukwaa ya udaku tuache na mtaalamu wetu aendelee kutusaidia. Mazuzu bado wengi sana TZ.
You must be one of them!!
 
Tumekuomba ondoka kwenye jukwaa letu maana huna mchango wowote constructive kwetu ni fujo tu, tuachie mtaalamu wetu tuendelee kupata faida na kukuza mitaji yetu.
Mkuu, fanya kumpuuza.

Unachotakiwa kufanya ni kwenda kwenye profile yake na kubonyeza kitufe cha IGNORE, hutoweza kuona upuuzi anaoandika.
 
Mkuu Os cordis,naomba kujua kama majan ya Lucerne yanafaa kutumika kama chakula cha nguruwe,na kama yanafaa yanamchango gan kwa fattening pigs?
Asante
Habari, kwa swali lako Majani ya Lucerne ndio hutumika kama moja wapo wa vichanganyo katika chakula cha nguruwe hasa kutengeneza chakula cha GROWERS na FINISHER.

Zifuatazo, ni sababu za kwanini lucerna hutumika kama moja wapo ya vichanganyo katika chakula cha Nguruwe.

(1) Majani hayo huwa na kiwango kikubwa cha protein ambacho ni kati ya 20-22% na katika chakula cha kukuzia nguruwe huitaji kiwango cha protein 18% na katika kumalizia au fattening huitaji kiwango cha protein 14%, kwa maana hivyo waweza ona ni kwa kiwango gani majani hayo yalivyo na umuhimu katika kujenga mwili wa nguruwe.

(2) Majani hayo yana kiwango kikubwa cha madini na vitamini na kama ikitokea yakavunywa mapema huwa na kiwango kizuri pia cha nishati na fibres. Ambazo ni muhimu sana katika ujenzi wa mwili wa nguruwe.

Zingatia; Kipimo cha lucerna katika mchanganyiko hutegemea na malighafi ulizonazo.
 
MSAADA
Habari wa ndugu naomba msaada nina ng'ombe wangu amezaa jana mwenyewe bila kusaidiwa kuvuta mtoto.
Leo nimerudi kazini nimemkuta amelala hawezi kuamka nimejaribu kila namna imeshindikana.

Naombeni msaada au hata ushauri.
 
MSAADA
Habari wa ndugu naomba msaada nina ng'ombe wangu amezaa jana mwenyewe bila kusaidiwa kuvuta mtoto.
Leo nimerudi kazini nimemkuta amelala hawezi kuamka nimejaribu kila namna imeshindikana.

Naombeni msaada au hata ushauri.
Unapatikana wapi? Shingo yake kaiweka vipi?
 
Habari Wakuu....
Nipo mbele yenu kujibu maswali yenu mbalimbali kuhusiana na tiba na ushauri wa magonjwa yanayosumbumbua mifugo yetu mbalimbali na hivyo kupelekea uzalishaji kupungua....

Na pia kwa wale wakazi wa Dar es salaam na viunga vyake wanaohitaji huduma za ki veterinarian natoa huduma za chanjo na kutibu kwa wanyama wote wa nyumbani kama vile ;
  • Pets (Dog and cat)
  • Cattle (Ng'ombe)
  • Shoats (Mbuzi na Kondoo)
  • Fresh water fish (samaki)
  • Poultry (Kuku)
  • Rabbit (Sungura)
Pia nafanya surgical operation kwa pets (mbwa na paka) kama vile castration and ovariohysterectomy (kufunga vizazi kwa madume na majike) and many other surgical operation kwa mifugo ya nyumbani tu.....

Updates.....

Vaccination schedules for Chicken......

Siku ya kwanza : Chanjo dhidi ya Marek's na chanjo hii huchanjwa nyuma ya shingo chini ya ngozi but mara nyingi chanjo hii huchanjwa kiwandani (Hatchery)

Siku ya Kumi: Chanjo dhidi ya Gumboro (1st dose) hii huchanganywa na maji

Siku ya kumi na nane: Chanjo dhidi ya Gumboro (2nd dose) hii huchanganywa na maji

Wiki ya tatu: Chanjo dhidi ya Newcastle (1st dose) Hii huchanganywa kwenye maji au huwekwa kwa tone kwenye jicho

Wiki ya sita: Chanjo dhidi ya Ndui Hii huchanjwa kwenye bawa (Inahitaji mtaalamu)

Wiki ya nane: Chanjo dhidi ya Newcastle (2nd dose) Hii huchanganywa kwenye maji au huwekwa kwa tone kwenye jicho

Wiki ya kumi na nane: Chanjo dhidi ya Newcastle (3rd dose) Hii huchanganywa kwenye maji au huwekwa kwa tone kwenye jicho (Baada ya Hii chanjo ya tatu unashauriwa kuchanja kuku wako kila baada ya miezi 3)

Wiki ya kumi na tisa: Wape kuku wako dawa ya Minyoo, Mara nyingi hupewa kwenye maji (Baada ya Hii chanjo ya tatu unashauriwa kuchanja kuku wako kila baada ya miezi 3)

------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

MAELEZO MUHIMU KUHUSIANA NA LISHE KWA MBWA NA NAMNA YA KUANDAA CHAKULA CHA MBWA

★ Utangulizi

Lishe/chakula/mlo kamili kwa mbwa ni muhimu sana kwani humpa mbwa afya nzuri na pia huwakinga mbwa na mashambulizi mbalimbali ya magonjwa na hivyo kuwafanya wavutie muda wote

Kwa sasa vyakula vingi vya mbwa hupatikana madukani kutoka viwandani maana vimefanyiwa utafiti na kuzingatia afya ya mlaji ambaye ni mbwa na wanasayansi wameenda mbali zaidi wameweza kutengeneza chakula kutegemea aina ya breed ya mbwa

Lakini hayo yote hayakuzuii wewe mmliki wa mbwa kujitengenezea chakula mwenyewe ambacho kitakuwa kimekidhi vigezo vyote vinavyohitajika kwa mbwa ili kuepuka gharama ya chakula kwa namna moja ama nyingine kama nitakavyoelezea hapa chini

★ Umuhimu wa maji kwa mbwa

✓ Vyakula vyote hata vile ambavyo hukaushwa na hewa maalamu kiwandani huwa na kiwango kidogo cha maji, ingawa mbwa anaweza jipatia maji kwa njia ya kunywa lakni kiwango kingine cha maji kinatokana na chakula

✓ Mbwa anaweza kukaa muda mwingi bila kula chakula ( Hunger tolerance) lakni hawezi kukaa muda mrefu bila kunywa maji kwa maana hiyo mbwa asipokula chakula hutumia mafuta na baadhi ya nyama za mwili kama mbadala wa kupata nishati ya nguvu lakni akipoteza moja ya kumi ya maji yake mwilini mbwa hupoteza maisha

✓ Bila maji ya kutosha mbwa hatoweza kumeng'enya chakula chake na hata kama akifanikiwa kwa hilo chakula hakitoweza kunyonywa vizuri katika mfumo wa chakula hivyo anahitaji maji muda wote na unywaji wa maji hutegemea na mazingira na wingi wa chakula

★ Sifa za mlo kamili wa mbwa

✓ Chakula cha mbwa kinatakiwa kuwa na ladha na harufu ya kuvutia

✓ Chakula kikidhi kiwango cha nguvu (wanga) kinachohitajiwa na mbwa

✓ Chakula kiwe na kiwango cha protini cha kutosha kuwezesha ukuaji wa mbwa na kumkinga na magonjwa

✓ Chakula kiwe na kiwango cha madini na vitamini cha kutosha

Zingatia: Mbwa ni jamii ya wanyama wanaokula nyama (carnivores) lakni tukija katika suala la mchanganyo wa chakula ulio kamili ni lazma uwe na protini, wanga, vitamini na madini na hata mbwa mwitu wanapowinda mbugani mara nyingi wanawinda jamii ya wanyama wanaokula majani na wakifajikisha kumuua hula kitu ukijumuisha matumbo ambayo huwa na majani yaliyomeng'enywa na mifupa yote hivyo kuwawezesha kupata madini na vitamini kwa njia hiyo hivyo basi kwa mbwa wanaofungiwa ndani ni lazma wapate mlo kamili kama nitakavyoelezea hapa chini

★ Vyakula vinavyotakiwa na mbwa na jinsi ya kuandaa vyakula hivyo

a) Nyama

Nyama ndio chanzo kikubwa cha protini kwa mbwa na katika mchanganyo inatakiwa kuwa zaidi ya 50%. Nyama hii yafaa ichemshwe kwanza ingawa mbwa wanapendelea nyama mbichi lakni kwa hili lazma ichemshwe na baada ya hapo ndio inatakiwa kuchanganywa na vyakula vingine

Kama nyama ina mifupa ni vyema mifupa ikaondolewa hasahasa kama nyama ni ya mbuzi/kondoo au kuku maana mifupa yao huwa ni midogo na hivyo inaweza kuleta shida katika mfumo wa chakula wa mbwa baada ya kuondolewa mifupa inatakiwa kuchemshwa pekee hadi pale itakapotoa supu ambayo itatumiwa kuchanganywa na vyakula vingine

b) Maziwa na Mayai

Maziwa na mayai hutumiwa kama mbadala wa nyama pale nyama inapokosekana hapa unatakiwa kuchukua maziwa kiasi cha lita 1.8 yachemshe yaache yapoe kisha changaya na mayai mawili yaliochemshwa vizuri then malizia kwa kuchanganya na vyakula vingine

c) Wali

Wali hutumika kama chanzo cha wanga na mchele unaotakiwa hapa ni ule unpolished (mchele mchafu) maana huwa na virutubisho vingi zaidi tofouti na ule Polished (mchele safi) na unaadaliwa kwa kuchemsha na maji kutengeneza bokoboko ambalo huchanganywa na vyakula vingine

d) Unga wa ngano

Unga wa ngano hutumika kama mbadala wa mchele endapo utakosekana hapa unatakiwa kuuchanganya kutengeneza uji mzito ambao utatumiwa kuukaanga kutengeneza chapati au pancakes ambazo utazikatakata na kuchanganya na vyakula vingine

e) Uji

Uji pia hutumika kama mbadala wa mchele na uji unatakiwa hapa ni ule ambao umetengenezwa na unga wa mahindi ambao haujakobolewa unauacha upoe kisha changanya na vyakula vingine. Mbwa wanaupenda sana uji huu.

f) Mbogamboga

Ingawa mbwa hawapendi mbogamboga lakni ni muhimu kuwemo kwenye mchanganyo maana ndio chanzo cha vitamini na madini mbalimbali mboga kama sukumawiki, chinese ni nzuri lakni ukikosa hizo unaweza chemsha carrot au beetroots na ukachanganya kwenye vyakula vingine na ikumbukwe kuwa kiwango cha mboga kitengeneze 1% ya mchanganyo wote

★ Vitu vya kuzingatia katika ulishaji wa mbwa

✓ Kwa kawaida tumbo la mbwa ni kubwa kulinganisha na viungo vingine vya mfumo wa chakula hivyo anatakiwa kula ambacho kitaweza kukaa mwilini kwa muda mrefu na kwa kawaida mbwa anayakiwa kula mara moja kwa siku ingawa watu wengine huwalisha mara mbili ambapo hutenga chakula kama chakula cha kawaida (light diet) au chakula cha kutosha (heavy diet)

✓ wali kidogo na mbogamboga huandaliwa kivyake baada ya hapo huchanganywa na supu na nyama kidogo na hii tunaita light diet na chakula kamili huwa na nyama,mbogamboga,wali au chapatti na vyote hivi huchanganywa na supu ya mifupa

✓ Na mbwa aina ya chakula kutegemea na majukumu yake yako muda gani ' Kama mbwa analinda usiku basi asubuhi anatakiwa kula heavy diet na jioni masaa machache kabla ya kuingia lindoni anatakiwa kula light diet na kama mbwa anaingia lindoni mchana basi jioni anatakiwa kula heavy diet na asubuhi kabla ya kuingia lindoni ale light diet

✓ Chakula cha mbwa kinatakiwa kuandaliwa muda kidogo kabla ya mbwa kula na kama chakula kikibakizwa na mbwa hatakiwi kulazimishwa kula na chakula hicho kiondolewe ndani ya dakika 10-15

✓ Vyombo vya chakula na maji vinatakiwa kuwa safi na salama muda wote na hakikisha maji hayaishi ndani ya chombo cha maji na kinatakiwa kuwa karibu na bakuli la chakula muda wote

✓ Mbwa wasipewe vyakula vya sukari au chumvi maana vyakula hivyo huwapunguzia umri wa kuishi na pia huwasababishia magonjwa mbalimbali ya ngozi

✓ Muda na mahali pa kulia chakula uwe/pawe sehemu moja hakuna haja ya kubadili ratiba ya chakula kama ni asubuhi ya saa 11 na jioni ya saa2 iwe hivyo muda wote hakuna haja ya kubadili ratiba ya chakula

✓ Kwa siku mbwa anatakiwa kuwa gm 350 za chakula na mara moja unaruhusiwa kumpa mbwa maji yaliyochanganywa na glucose na iwe kila siku

------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

MAELEZO KUHUSU UGONJWA WA (PARVOVIRUS INFECTION) KWA MBWA

★ Utangulizi

Ugonjwa huu huenezwa na virusi wanaoitwa parvovirus aina ya 2b, na ni miongoni magonjwa hatari sana kwa mbwa maana huambukiwa kutoka kwa mbwa mmoja kwenda mwingine na uligunduliwa miaka ya 1970's...

Ugonjwa huu huwa na tabia ya kushambulia seli maalamu ambazo hupatikana katika mfumo wa chakula hivyo (GIT) na hivyo kumsababisha mbwa kuonesha dalili kama vile kuharisha au kutapika. Na kupitia kuharisha virusi hawa hutolewa kwa wingi mno kwa wiki kadhaa baada ya mnyama kuugua na hivyo kuongeza uwezekano wa mbwa mwingine kuugua ugonjwa huo.....

Ugonjwa huu hushambulia mbwa wa umri wowote lakni kwa asilimia kubwa mbwa ambao wako katika hatari ya kupata ugonjwa huu ni wale wadogo wenye umri kati ya wiki 6-20 na jamii ya mbwa ambao hushambuliwa sana na ugonjwa huu ni Doberman pinscher na Rottweiler na hadi sasa haijajulikana kwanini kinga yao haiwasaidii sana wanapo shambuliwa na ugonjwa huu ( sio hao tu jamii nyingine pia hushambuliwa na ugonjwa huu mfano German shepherds, pit bull na Labrador retriever).....

★ Njia za uenezaji wa ugonjwa huu

Ugonjwa huu huenezwa kwa njia kuu mbili nazo nitaziweka katika makundi mawili njia ya moja kwa moja (directly) na njia isiyo ya moja kwa moja (indirectly)

a) Njia ya moja kwa moja (directly)

Ugonjwa huu huenezwa moja kwa moja iwapo mbwa asiye mgonjwa atagusana (manyoya au miguu wakati wa kucheza) na mbwa ambaye ni mgonjwa na hivyo kupelekea yeye kuwa na ugonjwa huo

b) Njia isiyo ya moja kwa moja (indirectly)

✓ Kama nilivyoelezea hapo mwanzo virusi hawa hutolewa kwa wingi kupitia kuharisha hivyo mbwa anaweza kupata ugonjwa huu baada ya kunusa au kula/kunywa chakula/maji ambayo yamechangamana na kinyesi hicho

✓ Pia mbwa anaweza kupata ugonjwa huu kupitia viatu, mara nyingi katika matembezi ya kawaida mmliki anaweza kukanyaga kinyesi cha mbwa mgonjwa na hivyo kubeba virusi hao nyumbani ambapo katika kuingia ndani ya banda anaweza sababisha mbwa kupata ugonjwa huu

★ Dalili za ugonjwa huu

Baada ya mbwa kuambukizwa ugonjwa huu itamchukua siku kati ya 4-5 kuonesha dalili za ugonjwa huo nazo ni kama ifuatavyo;

✓ Siku za mwanzo mbwa atakuwa mnyonge na atapoteza hamu ya kula

✓ Mbwa atatapika na kuharisha ( mara nyingi maharisho haya huwa na mchanganyiko wa damu/kamasi au vyote kwa pamoja)

✓ Baadhi ya mbwa huwa na joto kali linalofika 41.1 °C na wengine huwa na joto la kawaida

✓ Wakati wa uchunguzi wa mnyama katika maeneo ya tumbo huonesha dalili za maumivu na mara nyingi hupindisha mgongo na kuwa kama upinde hii ni dalili ya kwamba anasikia maumivu maeneo ya tumbo

✓ Mbwa huishiwa maji na hivyo kufanya ngozi kuvutika kirahisi na mwisho wa siku mbwa hupoteza uzito maana huwa hawezi kula tena

Kwa hapo mashambulizi ya moyo yalikuwa mengi kwa mbwa wagonjwa lakini kwa sasa njia hiyo ya mashambulizi kwa moyo imezuiwa na kufanikiwa baada ya chanjo zinazotolewa kwa mbwa jike mwenye mimba kati ya wiki 2-4 kabla ya kuzaa, Chanjo hii huongeza antibodies kwa mama ambazo mwisho wa siku hutumika kumlinda mtoto pindi anapozaliwa hivyo kuondoa mashambulizi ya virusi hawa kwa moyo wa mbwa wadogo (puppies)

★ Njia za kugundua ugonjwa huu

Zifuatazo ni njia zinazokuwezesha mmliki wa mbwa kujua mbwa wako kapata shambulizi la parvovirus;

✓ Dalili ya kutapika na kuharisha kinyesi kilichochangamana na damu au kamasi au vyote kwa pamoja

✓ Njia mbalimbali za maabara kama vile ELISA na IFAT hii ni baada ya kuchukua damu ya mgonjwa kwa uchunguzi zaidi ingawa matokeo yanaweza kuwa negative/postive

★ HITIMISHO

✓ Kama mjuavyo magonjwa mengi yanayosababishwa na virusi hayana tiba na ikumbukwe ugonjwa huu ni hatari sana hivyo ikitokea mbwa wako kaugua ni vyema kumjulisha Veterinarian kwa msaada na mbwa wako anaweza kurudi katika hali yake ya kawaida kwa zaidi ya 80%

✓ Kumbuka kuwachanja mbwa wako kwa wakati kuepuka kumpoteza mbwa wako ingali bado unampenda (Siku zote chanjo ni bora zaidi kuliko tiba)

✓ Usiruhusu kuwachanganya mbwa wako wadogo na mbwa wakubwa hadi
watakapo maliza ratiba za chanjo na inatakiwa wakae wiki mbili mbali na wakubwavbaada ya chanjo ya mwisho....

✓ Ratiba ya chanjo ni kama ifuatavyo wiki 6,9 na wiki 12 (Na kwanini kuanza na wiki sita hii ni kwa sababu wiki 2-4 za mwanzo mbwa huwa yuko chini ya ulinzi wa antibodies za mama hivyo ukiwachanja kwa wiki hizo za mwanzo ile chanjo itahisiwa kama shambulizi kwenye mwili wa mbwa mdogo hivyo kuliwa na hivyo inashauriwa kuanzia wiki ya 6 maana baada ya wiki 4 antibodies za mama huwa zinaanza kupungua kwenye mwili wa mbwa mdogo.

------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------

Utahitaji vifuatavyo ili kuwa na duka la mifugo

Site
Mtaji

VYETI VIFUATAVYO

Daktari aliyesajiliwa cheti
Chet cha msaidizi enroled or enlisted
TIN
TRA LESENI
TFDA
TPRA
FIRE
VCT for veterinary facility
BRELA

Kwa mahitaji ya cheti cha daktari aliesajiliwa tunaweza wasiliana.....

Karibuni sana....
Dr ngombe wangu amezaa sasa miezi mitatu. Alipatwa na ECF nikamtibu akapona. Lkn anakonda kila siku. Nikampima wakasema ana anaplasmosis. Nikampiga OTC 30%, akapata nafuu. Baadaye akaanza kudhoofu. Nikapima wakasema bado anaplasmosis. Nikampiga hi tech akapata nafuu. Jana nampima wanasem bado ana anaplasmosis. Nifanyeje?.

Nyongeza: Kuna Dr alisema labda kala nylon, nikampa epsom salt .. magnisium sulphate??? akaharisha, wakasema salt inasaga nylon into pieces, then anainya. Mwingine aksema immunity imeshuka na hivyo anaplasmosis ina surface.... na ni ngumu kutibu. which is which?
 
Dr ngombe wangu amezaa sasa miezi mitatu. Alipatwa na ECF nikamtibu akapona. Lkn anakonda kila siku. Nikampima wakasema ana anaplasmosis. Nikampiga OTC 30%, akapata nafuu. Baadaye akaanza kudhoofu. Nikapima wakasema bado anaplasmosis. Nikampiga hi tech akapata nafuu. Jana nampima wanasem bado ana anaplasmosis. Nifanyeje?.
Habari Mkuu, pole kwa kuuguliwa na mfugo wako ningependa kujua ulitumia njia gani kupima na kujua huyo ng'ombe yuko na Anaplasmosis ( Ndigana baridi) na Ulihakikisha vipi kuwa ng'ombe wako alipona ECF ( ndigana kali) na pia inaweza kuwa babesios.

Najua watu wengi huwa wanachanganya hayo magonjwa wakati wa kufanya diagnosis unaweza kuta unatibu anaplasmosis kumbe mfugo wako ana ECF..

Ndio maana dalili ni muhimu sana wakati wa kufanya diagnosis na dalili ukiwa expect mzuri unaweza kuwa correct kwa 60 % ila vipimo vya maabara ni 100%

Hivyo basi kama uko na uhakika ni anaplsmosis kweli jaribu kubadili dawa na tumia dawa hizo hapo chini;

Screenshot_20190523-074635_1.jpeg
 
ngependa kujua ulitumia njia gani kupima na kujua huyo ng'ombe yuko na Anaplasmosis ( Ndigana baridi) na Ulihakikisha vipi kuwa ng'ombe wako alipona ECF ( ndigana kali) na pia inaweza kuwa babesios.
Kuna mtaalamu wa maabara ndiye alitibu. Huyu baba ni mtaalamu alikuwa nafanya kazi ya utafiti kwenye maabara kuu ya Mko ilipokuwa inakuwa funded na Germany/ Uholanzi. Anaaminiwa sana katika microscopy.

Ng'ombe anakula, anacheua vizuri maziwa yamedrop kidogo toka lita 6 mpaka 4/4.5 kitu kama hicho.
 
Kuna mtaalamu wa maabara ndiye alitibu. Huyu baba ni mtaalamu alikuwa nafanya kazi ya utafiti kwenye maabara kuu ya Mko ilipokuwa inakuwa funded na Germany/ Uholanzi. Anaaminiwa sana katika microscopy.
ngombe anakula, anacheua vizuri maziwa yamedrop kidogo toka lita 6 mpaka 4/4.5 kitu kama hicho.
Fanya kumpa hiyo choice ya 3 katika hiyo picha niliokupa hapo juu..

Na imani ata recover vizuri..
 
Nahitaji huduma ya ku- spay paka wangu. alikuwa mmoja mara kakaja kengine kutoka porini nikashindwa kukatupa. nitapataje hiyo huduma
 
Nahitaji huduma ya ku- spay paka wangu. alikuwa mmoja mara kakaja kengine kutoka porini nikashindwa kukatupa. nitapataje hiyo huduma
Unapatikana wapi mkuu? Huduma ipo hiyo tutafanye kubadilishana mawazo then tupange siku ya kuja kumfanyia Ovariohysterectomy (OH) paka wako.

Ahsante.
 
as
Habari Mkuu, pole kwa kuuguliwa na mfugo wako ningependa kujua ulitumia njia gani kupima na kujua huyo ng'ombe yuko na Anaplasmosis ( Ndigana baridi) na Ulihakikisha vipi kuwa ng'ombe wako alipona ECF ( ndigana kali) na pia inaweza kuwa babesios.

Najua watu wengi huwa wanachanganya hayo magonjwa wakati wa kufanya diagnosis unaweza kuta unatibu anaplasmosis kumbe mfugo wako ana ECF..

Ndio maana dalili ni muhimu sana wakati wa kufanya diagnosis na dalili ukiwa expect mzuri unaweza kuwa correct kwa 60 % ila vipimo vya maabara ni 100%

Hivyo basi kama uko na uhakika ni anaplsmosis kweli jaribu kubadili dawa na tumia dawa hizo hapo chini;

View attachment 1105279
asante Dr. sasa nitumie dawa gani kati ya hizo for better results?
 
asante sana, ubarikiwe. Dosage tafadhali nisaidie
Dosage kuna hizo mbili hapo 3mg/kg kama lowest dose na 5mg/kg kama highest dosage...

So, nakushauri nenda kwa highest dose kupata volume for injection chukua uzito wa ng'ombe husika in (kg) zidisha na dosage ambayo ni 5mg/kg then gawanya na concentration ambayo ni 120mg/ml kupata injection volume mkuu...

Hope umenielewa hapo maana una akili kubwa mpe sindano ya kwanza leo then sindano ya pili irudiwe baada ya wiki mbili kumbuka kuchoma kwenye nyama ya shingo au kwenye rump area juu karibu na eneo la mkia kule utaingia mtandaoni kuona site hiyo mkuu..

Goodluck
 
Dosage kuna hizo mbili hapo 3mg/kg kama lowest dose na 5mg/kg kama highest dosage...

So, nakushauri nenda kwa highest dose kupata volume for injection chukua uzito wa ng'ombe husika in (kg) zidisha na dosage ambayo ni 5mg/kg then gawanya na concentration ambayo ni 120mg/ml kupata injection volume mkuu...

Hope umenielewa hapo maana una akili kubwa mpe sindano ya kwanza leo then sindano ya pili irudiwe baada ya wiki mbili kumbuka kuchoma kwenye nyama ya shingo au kwenye rump area juu karibu na eneo la mkia kule utaingia mtandaoni kuona site hiyo mkuu..

Goodluck
asante sana tena. Nashukuru sana tena.
Hapana sina akili kubwa, ila I can precisely follow instructions as given. nimefanya kazi for 30 yrs as a research scientist with speciality in Immunology//microbiology in one of our research Institutions.
Ubarikiwe tena.
 
asante sana tena. Nashukuru sana tena.
Hapana sina akili kubwa, ila I can precisely follow instructions as given. nimefanya kazi for 30 yrs as a research scientist with speciality in Immunology//microbiology in one of our research Institutions.
Ubarikiwe tena.
Tupo pamoja mkuu pale utakapoona kuna shida mahali, na unahitaji msaada zaidi kuwa huru kuuliza.

Nitakupa all necessary information required as per asked.
 
Tupo pamoja mkuu pale utakapoona kuna shida mahali, na unahitaji msaada zaidi kuwa huru kuuliza.

Nitakupa all necessary information required as per asked.
asante sana. Looks this dawa is very expensive. How much does it cost in dar? Naweza kumchoma leo dose moja, then ingine nikatafuta ya bei nafuu Dar. I am in Tanga
300 x 5= 1500/120= 12.5 mls needed. Each meal is 2500 Tsh! .....12.5 x 2500= 31,250 Tsh. Vial nzima ya 50 mls is 75,000 Tsh
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom