Mtaalamu wa mifugo (Dr. by Veterinarian): Karibuni kwa ushauri, tiba na dawa za mifugo tu

Du pole ningepata huu uz mapema. Wake doxcol kwa doz ya kijiko cha chakula kwa maji Lita 10. Pamoja na multivitamin kama farmvita. Yalikua mafua makali eidha yaliambatana na Kuku kuvimba macho, kukoroma n.k ko ilibid ubadili dawa.
Hiyo ya macho kuvimba mara nyingi huwa ni infectious coryza na mara nyingi dawa ya enrofloxacin huwa inatoa matokeo mazuri zaidi...

Na kabla ya yote hakikisha unawasafisha macho vizuri kwa kutumia kitambaa safi ukiwa umeweka providone iodine kisha baada ya hapo weka otc wound powder katika macho then malizia na enrofloxacin katika maji...

Ila kwa yote zingatia usafi kuku wengi wanaopata mafua tatizo ni wewe mfugaji kuwa mchafu hasa maeneo ya ndani ya banda...

Kila la kheri i
 
NAFUGA PAKA JIKE ILA NATAKA ASIZAE JE NI FANYAJE?
Hapo dawa ni kumtoa kizazi kwa kumfanyia operation maalumu aina ya Ovariohysterectomy....

Ila pia unaweza mchoma baadhi ya hormone kila baada ya miezi 6 pia hawezi pata mimba...

Ila njia ya sindano ni ghali zaidi ukilinganisha na operation ya kutoa kizazi...

Karibu...
 
kuku wangu wamezidiwa na mafua na kikohozi mpaka imepelekea kifo cha kuku wanne aina ya saso mpaka sasa,niliwapatia tylodox nkiwa na mix na eggbooster ila sikufanikiwa kutibu chochote zaidi ya tatizo kuzidi,na saivi nimeshauriwa kuwapa otc 50%,cjui itanifaa kwa wale mlio wataalam naombeni msaada wenu please kuku wangi wana miezi 6 saivi,wananitian stress kwa kweli
Nishalijibu hapo kwa chini...

Njia mbadala wa mafua sugu ni kuanza kuwachanja kuku wako dhidi ya infectious bronchitis chanjo hii huja pamoja na kideri na gharama yake ni 15000 tu...
 
Habari, naomba kwa wazoefu ni ukubwa kiasi gani kitahitajika kwa ujenzi wa banda la kuku wa mayai wa kisasa 500, pia ningependa kujua vitu muhimu vya kuzingatia wakati wa ujenzi wa banda hilo na mwisho aina nzuri ya kuku wa mayai!

Sent using Jamii Forums mobile app
Nenda na hii hesabu kwa kawaida kuku 7 wanatosha vilivyo katika mita moja za mraba je kuku miatamo watahitaji ukubwa wa banda kiasi gani...

Weka urefu 15 na upana 5 kuku mia tano watatoshelezea vizuri pia lina uwezo wa kubeba hadi kuku 800...

Karibu kwa msaada zaidi
 
Dr vipi kati ya hawa wanaojulikana kwa jina la kuku wa Malawi (australorp) na kuroiler ni wapi wenye kutaga zaidi mayai? Na pia hao australorp nitawapataje nikiwa Dar?
Kuku wa malawi sijabahatika kuwajua vizuri kuroiler pia wako vizuri tatizo linakuja kwa hao kuku chotara watu wanajizalishia wenyewe majumbani kwao kwa hiyo unaweza kuta unauziwa kuku wa kizazi cha 3 au 4 ambapo performance ya kuku husika iko chini sana...

Ila ukienda kiwandani wanapozalishwa utawapata wenyewe "1st generation na watakupa good performance ....

Karibu kwa msaada zaidi
 
Naomba ushauri wako mkuu mm mwezi huu was January 2019 nataka kuanza kufuga ngombe madume ntaanza na ndama wadogo wa 2 npo mkoa wa Kilimanjaro huku naomba unisaidie kiutaalamu nifanyeje fanyeje ili waweze kuwa na afya na baada ya miaka 2 niwauze angalau nipate Vicent kidogo vya kusogeza siku
 
Kuku wa malawi sijabahatika kuwajua vizuri kuroiler pia wako vizuri tatizo linakuja kwa hao kuku chotara watu wanajizalishia wenyewe majumbani kwao kwa hiyo unaweza kuta unauziwa kuku wa kizazi cha 3 au 4 ambapo performance ya kuku husika ila ukienda kwa kiwandani wanapozalishwa utawapata wenyewe 1st generation na watakupa good performance ....

Karibu kwa msaada zaidi
Ahsante sana Dr. Vipi group lako la whatsapp bado lipo ili nijiunge? Kama lipo naomba link.
 
Mafua sugu yaweza kuwa ni infectious bronchitis ni ugonjwa wa virusi ambao kuku wakiupata wanakuwa na mafua ya muda mrefu bila kupona...

Matumizi ya antibiotic si mazuri maana utaingia gharama kubwa ya kuwatibia kuku wako na tatizo likabakia palepale...

Ni vyema sasa nyie wakulima mkaanza kuwachanja kuku wenu dhidi ya infectious bronchitis na mara nyingi chanjo hii inachanjwa sawa na kideri na bei yake ni 15,000 ukinunua hicho kichupa cha chanjo ndani yake utakuta chanjo ya kideri na infectious bronchitis.

Mkuu umeongea vizuri sana. Ubarikiwe.
 
Kuku wa malawi sijabahatika kuwajua vizuri kuroiler pia wako vizuri tatizo linakuja kwa hao kuku chotara watu wanajizalishia wenyewe majumbani kwao kwa hiyo unaweza kuta unauziwa kuku wa kizazi cha 3 au 4 ambapo performance ya kuku husika iko chini sana...

Ila ukienda kiwandani wanapozalishwa utawapata wenyewe "1st generation na watakupa good performance ....

Karibu kwa msaada zaidi
Mkuu samahani....mbuzi wangu wanasumbuliwa na minyoo..dawa ni ip mkuu..na nn kifanyike kudhibiti tatizo
 
NAOMBA UNISAIDIE HILI. Nilinunua Mayai ya koroila na kuyaweka kwenye kitotoleo. Ilipofika siku ya siku 7, niliyapima ili kujua kama yatatoa Vifaranga sikuona kitu,hali hii mpaka siku ya 25 hali haikubadirika.

Nilipouliza kwa walioniuzia wakanijibu kuwa, miezi ya Jan,Feb na march majogoo huwa hawawezi kurutubisha Mayai. Hii ni kweli?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
NAOMBA UNISAIDIE HILI. Nilinunua Mayai ya koroila na kuyaweka kwenye kitotoleo. Ilipofika siku ya siku 7, niliyapima ili kujua kama yatatoa Vifaranga sikuona kitu,hali hii mpaka siku ya 25 hali haikubadirika. Nilipouliza kwa walioniuzia wakanijibu kuwa, miezi ya Jan,Feb na march majogoo huwa hawawezi kurutubisha Mayai. Hii ni kweli?

Sent using Jamii Forums mobile app

Uwongo.
 
Dar unapatikana maeneo gani. Waweza ni PM kwa msaada zaidi
Mkuu habari.

Nafuga ngurue, nilipandisha majike 6 kwa wakati mmoja, huu mwenzi ilibidi wazae.
Lakini mda wakuzaa ulivyokaribia hali ikabadilika hawataki kula wanalala tu hawanyanyuki baada ya hapo wanakufa.
Nimekwisha wazika ngurue wa 3. Mpaka mda huu.

Nifanyeje!?
 
Mkuu habari.

Nafuga ngurue, nilipandisha majike 6 kwa wakati mmoja, huu mwenzi ilibidi wazae.
Lakini mda wakuzaa ulivyokaribia hali ikabadilika hawataki kula wanalala tu hawanyanyuki baada ya hapo wanakufa.
Nimekwisha wazika ngurue wa 3. Mpaka mda huu.

Nifanyeje!?

Pole sana kwa kupoteza nguruwe wako mkuu.

Ningependa kujua kama ni uzao wao wa kwanza.
 
Hapo shida huwa ni maungo ya uzazi kuwa madogo. Unaweza niambia upo na breed gani? Na unapatikana wapi
 

Similar Discussions

36 Reactions
Reply
Back
Top Bottom