Mtaalamu wa mifugo (Dr. by Veterinarian): Karibuni kwa ushauri, tiba na dawa za mifugo tu

Mkuu pole sana kwa viranga wako kushambuliwa na ndui (chicken pox) kwa ushauri fanya yafuatayo
  • Kwanza hao viranga waliopatwa na ndui ni vyema ukawachukua na kuwatenga na viranga ambao hawajaonesha dalili yoyote ya ndui (hapa namaanisha uwahudumie peke yao)
  • Pili vyombo vyote vya chakula na maji unaweza kuvisafisha na bleach agent yoyote kama vile 10% ya sodium hydroxide or sodium hypochlorite kabla ya kuweka maji or chakula
  • Na mwisho kwa kuwa huu ungonjwa huenezwa na mbu ni vyema kama kuna madimbwi ya aina yoyote karibu na banda lako la kuku ni vyema ukayafukia ili kuepeka kuenea kwa ugonjwa huo katika kuku wako
Angalizo: usiwape kinga yoyote ya ndui kabla ya muda muafaka haujafika mkuu na imani nitakuwa nimekusaidia kwa namna moja ama ingine
Mimi vifaranga wangu wana umri wa mwezi mmoja na nusu, bado sijawapatia chanjo yoyote, je kuna tatizo nikianzia hapa kuwapatia mtiririko wa chanjo? Asante.
 
Mimi vifaranga wangu wana umri wa mwezi mmoja na nusu, bado sijawapatia chanjo yoyote, je kuna tatizo nikianzia hapa kuwapatia mtiririko wa chanjo? Asante.
Bila shaka watakuwa vifaranga wa kienyeji? Kama ndio wapatie katika umri huo hakuna tatizo lolote hapo.
 
Habari !

Ngombe wangu Wana tatizo . Kwanza walikua wanamimba wote wawili , then zlivofik miez minne - mitano zikatoka wote .

Baada ya hapo wamekua wakiingia joto lakin kila nkiwapandisha hawashiki mimba wote na ndama wao wameshakua wakubw wanakaribia mwaka, still ngombe bado wanakamuliw .

Tatzo langu ni kwanini hawashiki mimba wote kila wakipandwa . Nimewapandisha Kama Mara nne hivi .

Asanteni

nb: hao waliotoa mimba ndo hawashiki sahivi mwenzao mwingne yeye hakutoa mimba yake ni kubwa sahiv
Upo wapi?
 
Bila shaka watakuwa vifaranga wa kienyeji? Kama ndio wapatie katika umri huo hakuna tatizo lolote hapo.
NISAIDIE TAFADHALI. NGOMBE WANGU ANAKOHOA SASA NI KAMA MWEZI N ZAIDI , TATIZO NI NINI? Dawa za minyoo nimmpa, sindano za OTC 20 nimempa bado tu! Nisaidie nitumie dawa gani na ni ugonjwa gani
 
NISAIDIE TAFADHALI. NGOMBE WANGU ANAKOHOA SASA NI KAMA MWEZI N ZAIDI , TATIZO NI NINI? Dawa za minyoo nimmpa, sindano za OTC 20 nimempa bado tu! Nisaidie nitumie dawa gani na ni ugonjwa gani
Ukiacha dalili hiyo ya kukohoa kuna dalili nyingine ambayo ameionesha? Kuna dawa kiboko kwa ajili ya changamoto za kukohoa ila bei yake iko juu sana kampuni ya Zoetis kama utakuwa vizuri nikuunge na muuzaji moja kwa moja.

Na kuhusu bata wako mwezi mmoja bado wadogo sana labda kama utaweza kuwaandalia mazingira ya joto sehemu yao ya kupumzikia.
 
Asante Sana Dr. Ni Kama Bei gani kusudi ukiniunga naye niwe na hela tayari anitumie nimlipe maana ngombe wangu Ni wa muhimu kuliko hela.

Dr. Mbonà Bata wanalala peke Yao Wala mama Yao hawafuniki kwa mbawa?

Asante Sana kwa ushauri. Appreciated!
 
100mls inaenda zaidi ya 68,000 the best of the best from Zoetis
 
Ndigana ipi mkuu ?kuna ndigana baridi (anaplasmosis ),ndigana kali (ECF) Ndigana maji (heart water)
Ng'ombe wangu anatetemeka kama ambae pumzi inabana na tumbo lake na anahema sana, pia anatoa ute hasa nyakati za mchana...na manyoya yake yamesimama.
Nisaidie mtaalam itakuwa ni ugonjwa gani?

Sent from my SM-G532F using JamiiForums mobile app
 
Kiongozi umefunga Pm ninashida na wewe sana
Breed gani ya kuku wa mayai inafaa sehemu za baridi pia mayai yake yana ubora na makubwa,mfano kuna wauzaji kama interchik,silverland.....ambapo breed ni kama hyline,issa brown,bovan n.k..
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom