Mtaalamu Wa Mashine Na Zana Zote Za Kilimo(Eng.Chalangwa) Kwa Ushauri,Elimu Na Msaada Kuhusu Zana Na Mashine Za Kilimo.

Mar 7, 2018
15
9
Kwa wale wanaotafuta ushauri,Elimu Na Msaada Wa Jambo Lolote Kuhusiana Na Mashine na Zana Za Kilimo Kama vile Matrekta,Planters,Sprayers,Ridgers,Cultivators,Ploughs,Na Nyinginezo,Tuone Tutakusaidia Kwa gharama Nafuu kabisa.
Tunapatikana Muheza Tanga Ndani Ya Chuo cha kilimo MATI Mlingano.

Mawasiliano 0628938183,
0744142647
Email:levischalangwa01@gmail.com

Karibuni sana.
 
Hapana.Hatuuzi zana za kilimo ila tunatoa ushauri,na utaalamu wa matengenezo na marekebisho kwa wenye matatizo ya Mashine na zana za kilimo kwa ujumla.
Wasiliana na makampuni yanayojihusisha na uuzaji wa za za kilimo kama vile AgriCom,LonAgro N.k
 
Mkuu, Vp Diploma in General Agriculture.. Inapatikana hapo..?
Nahitaji nijiunge this year
 
Inatolewa hapa kwa mwaka mmoja ikiwa tu umesimama certificate of general Agriculture.
Ooh..!! Basi me nahitaji hyo maana Nina certificate, So nina Interest ya kusoma hicho chuo sasa..
Vipi kuhusu Maombi yakujiunga na chuo hapo ni wakati gani wanaanza..?
 
Ooh..!! Basi me nahitaji hyo maana Nina certificate, So nina Interest ya kusoma hicho chuo sasa..
Vipi kuhusu Maombi yakujiunga na chuo hapo ni wakati gani wanaanza..?
Maombi ya kujiunga na chuo hapa ni mpaka pale NACTE watakapofungua dirisha kwa vyuo vya elimu ya kati kuanza kupokea maombi ya udahili.Mara nyingi ni kuanzia may au june.Wakifungua tu NACTE dirisha,tuma maombi lazima utachaguliwa tu.Karibu sana MATI MLINGANO!
 
Tractor John Deer 4wd na Newholland 4wd ipi bora na inadumu?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwanza naomba niwaambie kwamba ubora wa tractor au mashine yoyote inayotumika shambani ama mahali popote hakutegemei tu ubora wa tractor au mashine husika pekee.
Bali unategemea vitu vifuatavyo:

1.Matumizi sahihi ya mashine au tractor sawa sawa na maelekezo ya watengenezaji husika.

2.Operator wako anazingatia safety and maintenence guidelines wakati ana operate tractor?

3.Unafuata zile daily and periodic maintenance tips?(service kwa wakati na kwa ubora)

Nikirudi specifically kwenye swali lako,Tractor Za John Deere 4WD Zina nguvu,imara na bora zaidi kuliko New Holland 4WD.

Lakini matatizo yanayozisumbua Tractor za John Deere mara nyingi ni Matatizo ya Engine,Leaks(kuvuja kwa oil hasa kwenye mfumo wa transmission na kuvuja kwa hewa )

Kwa New Holland baadhi zinakua na usumbufu katika uwakaji,transmission na misfiring (kuwaka nje ya mpangilio wake)

Aidha nilichokuwa hakina maana Tractor zote zipo hivyo lakini nimekuwa tu hayo ili ujue unapoinunua hakikisha imejaribu hiyo mifumo ili kuona ufanyaji wake wa kazi lakini baada ya kununua ni jukumu lako kuhakikisha unafuata ratiba ya service na maintenence kama mtengenezaji alivyoeleza kwenye kitabu cha matumizi.

Ahsante.
 
Maombi ya kujiunga na chuo hapa ni mpaka pale NACTE watakapofungua dirisha kwa vyuo vya elimu ya kati kuanza kupokea maombi ya udahili.Mara nyingi ni kuanzia may au june.Wakifungua tu NACTE dirisha,tuma maombi lazima utachaguliwa tu.Karibu sana MATI MLINGANO!
Thanks kiongozi..
Mungu akijaaliah.. Nitakuwepo maeneo hayo
 
Back
Top Bottom