Mtaalamu wa Dawa na Tiba: Ninakaribisha maswali kuhusu Magonjwa, Tiba na Dawa

Dokta naomba kujua Hilo, jamaa yangu amegundua mshipa wa demu wa kwenye uume wake kwa ndani kuna viuvimbe dizaini ya ulezi.
Atakuwa anaumwa ugonjwa? Madhara ya ugonjwa huu ni yapi na Tina yake ni ipi
 
Habari Doctor pole kwa majukumu ,mm hua napata maumivu chini ya mbavu kwa ndani kila napovuta pumzi kwa nguvu lkn baada ya mda hali hii inapotea ,naomba kujua izo ni dalili za ttzo lililopo kwenye mapafu ama ni kwenye figo.Ahsante
 
Mkuu umecheki sukari ipo sawa??
HABARI NZURI KWA WA WATANZANIA PAMOJA NA WAHANGA WA TATIZO LA MIGUU NA MIKONO KUWAKA MOTO

Kama ni muhanga nakushaur soma makala hii ili uweze kupata faida kubwa
JE, WAJUA CHANZO CHA MIGUU AU MIKONO KUWAKA MOTO, KUUMA, AU KUFAGANZI?

Katika mwili wa binadamu, kuna tatizo la kiafya ambalo huambatana na dalili za mtu kuhisi maumivu, kuhisi kuwaka moto na kufa ganzi kwa viungo vya pembezoni mwa mwili yaani miguu na mikono. Tatizo hili kitaalamu hujulikana kwa jina la Peripheral Neuropathy.

Mwili wa binadamu hutawaliwa na mifumo ya neva au kwa kitaalamu Nervous System, ambapo katika mifumo hii kuna mfumo mkuu, central nervous system (ubongo na uti wa mgongo) na pia kuna mfumo wa pembezoni ambao ni kazi za mwili mbali na ubongo na uti wa mgongo (peripheral nervous system), mfumo huu wa pembezoni hujumuisha kazi za misuli, mapigo ya moyo, mmeng’enyo wa chakula tumboni, uwezo wa kuhisi baridi au joto, kugusa vitu na kujua ukali wa ncha ya kitu na kadhalika.

Matatizo haya ya kiafya (miguu au mikono kuhisi ganzi, baridi au maumivu) husababishwa na kuumia au kudhoofika kwa neva za pembezoni mwa mwili (miguuni au mikononi) na hivyo kupotea kwa uwezo wa kufanya kazi wa neva katika sehemu husika, miguuni au mikononi.



Dalili zinazoambatana na ugonjwa huu ni hizi zifuatazo: Tu kuhisi ganzi
Maumivu au kuwaka moto maeneo ya miguuni au mikononi,
Kuhisi kama umevaa soksi au gloves wakati hujavaa,
Kuhisi kama kuna kitu cha ncha kali kinakuchoma miguuni au kwenye vidole,
Kushindwa kushika au kunyanyua kitu,
Kuchoka kwa misuli na kadhalika.

Miongoni mwa mambo ambayo hupelekea neva hizi za pembezoni kudhoofika na kushindwa kufanya kazi vizuri ni haya yafuatayo naomba uyafahamu:

Kupungua kwa virutubisho mwilini, katika hili tunamaanisha mwili kutokuwa na vitamini vya kutosha na hasa mkusanyiko wa vitamini B, (Vitamin B Complex).
Matumizi ya dawa, mtu kuwa katika matumizi ya baadhi ya dawa, mfano dawa za kutibu kifua kikuu au za kupambana na virusi vya ukimwi huweza kumsababishia mtumiaji matatizo ya neva.
Uzito mkubwa wa mwili: Hali hii hupelekea maumbile ya viungo vya mwili mfano umbile la uti wa mgongo lionekane tofauti na ilivyo kawaida, kubadilika huku husababisha baadhi ya neva katika uti wa mgongo zikandamizwe zaidi na misuli au uzito wa mwili na hivyo kusababisha neva hizo zishindwe kufanya kazi vizuri, matokeo yake ni wewe kuanza kuhisi maumivi au kufa ganzi kwa miguu.
Ugonjwa wa kisukari: Mtu mwenye tatizo la kisukari huwa hatarini zaidi kuugua au kupata matatizo ya neva, (diabetic polyneuropathy).
Shinikizo la damu: Mtu kuwa na shinikizo kubwa la damu (High blood pressure) pia ni kihatarishi kinachoweza kumfanya mtu apate ugonjwa huu wa neva.
Baadhi ya vitu hatarishi vinavyoweza kumfanya mtu apate matatizo haya, vinaweza kuepukika kwa mtu kuyabadili maisha yake mfano, kama ulikuwa hufanyi mazoezi ya mwili, basi ujitahidi kuupa mwili mazoezi ili kupunguza uzito wa mwili, kuepuka magonjwa ya kisukari na kuepuka kuwa na shinikizo kubwa la damu, kula chakula chenye virutubisho vya kutosha kama vile PHYTOGUARD, NEOTONIC, nk.

MATIBABU YA KITAALAM ZAIDI
Eternal international ndio suluhisho wasiliana nasi kwa simu 0653216061
 
Dawa ya maumivu makali ya kiuno nyuma ya mgongo. maeneo ya nyonga kwa mwanaume.. ni makali sana anapafa binamu yangu hadi kaambiwa astop sex kwa muda hadi? apone je atapona lini kwani mke, wake ana muhitaji.. nisaidie please jamani binamu yangu anateseka sana kwa maumivu hayo ...

Jaman mwenye maelezo kuhusu hayo maumivu mwenyew naona kuna maumivu yameanza,nin dawa yake na nin kinasababbisha.
 
Jaman mwenye maelezo kuhusu hayo maumivu mwenyew naona kuna maumivu yameanza,nin dawa yake na nin kinasababbisha.
The best thing to do anywe quality amount of water that's it coz hata meds anapatiwa ziko zikifnya kazi ya kustimulate ADH ili apate kutake in a lot of water daily.
It's Dr.D
Nasumbuliwa na kidneystones imeshanisumbua muno. Nisaidie
Shkamoo doctor. Ninaishi na asthma tangu kuzaliwa huwa natumia triam injection nakaa miezi nane bill kuugua lakini nableed Sana mwezi was Kwanza baada ya kutumia Hadi siku 16 nifanyeje. Bill kuichoma swez kuishi pia alienianzishia tiba alinipa madawa mengi mno hivyo vidonge hunikataa milele
IMG_20190928_151504.jpeg
 
Naomba kuuliza, tatizo la visigino kuuma linasababishwa na nini? Na tiba yake ni ipi?!
 
Dokta pua yngu ya upande wa kushoto kama vile imeziba na jicho la upande wa kushoto linauma kwa ndani, mwaka 2011 nilifanyiwa upasuaji wa mtoto wa jicho, then kifua kizito hadi mapegani, mgongoni, shingoni pia sometimes napatwa na vichomi kifuani sijui shida nini? Nimezunguka Hospital wee yapata miaka 7 sasa nimepigwa x-ray, ultrasound , echocardiogram, hapo kwenye X-ray kuna kipindi ikaonesha nina moyo mkubwa lkn baadae nilivyopimwa na kipimo cha echo ikaonekana niko fresh lkn nikaandikiwa dawa propranolol, asp cardiovascular, capriprol lkn sijaona nafuu naomba msaada
 
samahani doctor kuna hali inanitokea mara kwa mara,sasa ni kama mara 3 hivi ila sielewi ni nini?,kuna wakati nilikuwa natoka kulala nikaenda nnje kukojoa,lakini baada ya kukojoa najisikia kizunguzungu,wakati mwingine naweza kuzimia dakika chache na kuzinduka,nimeenda pima pressure iko normal,je hii hali husababishwa na nini,na nawezaje epukana nayo???,naomben msaada ndugu zangu.
 
Habari wakuu,

Nakaribisha maswali yoyote kuhusu magonjwa, dawa, tiba na afya kwa ujumla. Kama una maswali kuhusu ugonjwa wowote, vipi kuishi na magonjwa, kufanya mabadiliko kwenye maisha baada yakupata ugonjwa, matibabu, matumizi ya dawa, matumizi ya dawa pamoja na dawa nyingine au athari zake.

Karibuni sana.

View attachment 361607

Kama umejibiwa maswali na mtu mwingine na haijakufaa ni kosa lako.
Mimi nitajibu maswali zote mwenyewe kama Daktari.








Habari doctor,
Mimi ni ni muathirika wa masikio yaan hayasikii vizuri. Na nina experience vitu vifuatavyo!
a)Yana unguruma kwa ndani.
b)Mtu akiongea namsikia ila sijui n nn anamaanisha
c)Mtu akiwa mbali simsikii kabosa.
d)Hayaumi wala kutoa usaha.

Mwanzo nilitumiaga hizi ear drop za kunyunyizia sikion hazikufanya kazi. Badae nikaenda kupima na kupewa dawa zinaitwa neuroloton nilitumia miezi mitatu ila nazo hazija fanya kazi.

Nimesikia altenative way n kufanyiwa cochlear implant.

Rai yangu kwako ni je kuna dawa zaid ya hiyo ? na je kufanyiwa cochlear implantvina cost sh ngap?
 
NINA TATIZO LA VIDONDA VYA ULIMI ,HUNIJA MARA KWA MARA.
KAMA NIKIPATA NAFUU MWEZI MMOJA AU MIWILI ,TENA VINAREJEA.
VINASABABISHWA NANINI?
NA NINI TIBA YAKE?
 
43 Reactions
Reply
Back
Top Bottom