Mtaalamu wa Dawa na Tiba: Ninakaribisha maswali kuhusu Magonjwa, Tiba na Dawa

Habari wakuu,

Nakaribisha maswali yoyote kuhusu magonjwa, dawa, tiba na afya kwa ujumla. Kama una maswali kuhusu ugonjwa wowote, vipi kuishi na magonjwa, kufanya mabadiliko kwenye maisha baada yakupata ugonjwa, matibabu, matumizi ya dawa, matumizi ya dawa pamoja na dawa nyingine au athari zake.

Karibuni sana.

View attachment 361607

Kama umejibiwa maswali na mtu mwingine na haijakufaa ni kosa lako.
Mimi nitajibu maswali zote mwenyewe kama Daktari.









Doctor mimi Nina tatizo la Hepatitis B' je naweza kupata tiba kutoka kwako?
 
Vipi kwa tatizo la neurofibromitosis kuna dawa zinazowezaondoa uvimbe hasa uliomtokea mdogo wangu kuzunguka jicho na pua amefanyiwa operation 3 ila unarudi tu.
 
Habari za muda docta,kwa muda ss nimekuwa nikisumbuliwa na tatizo la kichefuchefu pale napotumia vitu vitengenezavyo na ngano kama maandazi,mikate,chapati n.k.nimeshamia dawa z minyoo mbqlimbali bila mafanikio.Je naweza kupata tiba maana nakosa amani kabisa na hli tatizo.
 
Habar zenu ndugu znguu,,mwezenu na Kama mwaka sas nasumbuliwa na tatizo la kuwaka Moto miguun na kushika ganzi pia(miguu yote miwil)...na sas imepelekea kukosa nguvu miguun hata nnavyo tembea huwaga napepesuka Kama vle nmelewa.......plz naomba ushauri ndugu znguu Ni ipi tiba au dawa ya kutumia ili npate kuponaaa
 
Naomba kujua side effects za dozi ya CEFTRIASONE INJECTION. Na jee hudumu kwa muda gani??.

Maana Toka nimalize hii dozi napata tabu Sana.
 
Maumivu ya koo, maumivu ya viungo, vitu kuchomachoma mwilini pia kuhisi miguu kuwaka Moto, maumivu hutokea Sana upande wa kushoto kwenye kiwiko, magoti, na kwenye mabega tumboni.

Ila kuwashwa hasa maeneo ya tumbo na mapajani... Hutokea wakati wa usiku
 
Dokta pole kwa majukumu. Naomba majibu ya;
1. Kupata kichefuchefu hasa nikila ndizi, chungwa, embe usiku. imepelekea kutokula matunda ama vyakula vya ndimu au vichachu usiku. Nini tatizo?
2. Mwanangu amefikisha miezi 5 na wiki 2, nimeanza kumpa serelac amepata kubabuka ngozi. Nikaacha kumpa. Nikaanza kumpa uji wa dona tu, ameanza kubabuka tena. Nini tatizo? maziwa ya mama ake ashibi sasa
 
Habar zenu ndugu znguu,,mwezenu na Kama mwaka sas nasumbuliwa na tatizo la kuwaka Moto miguun na kushika ganzi pia(miguu yote miwil)...na sas imepelekea kukosa nguvu miguun hata nnavyo tembea huwaga napepesuka Kama vle nmelewa.......plz naomba ushauri ndugu znguu Ni ipi tiba au dawa ya kutumia ili npate kuponaaa

Mkuu umecheki sukari ipo sawa??
 
Tatizo langu nikiendesha baiskeli au kukaa kwa muda mrefu kwenye gari, kiti etc tako moja/side moja inachoka nifanye nn ili tatizo liishe😐😐
 
Ninaomba unifahamishe chanzo na tiba ya tatizo hili...
Kupata baridi kali saana katika baadhi ya maeneo (baridi vamizi kama unamwagiwa maji gafla vile) kama mgongo, bega, mkono au mguu na wakati mwingine kifua, tumbo na mwisho mwili wote una pata baridi na hatimaye kutetemeka.
 
43 Reactions
Reply
Back
Top Bottom