Bavuvi
Member
- Mar 1, 2008
- 41
- 4
Ninapanga kuanzisha mradi wa mifugo (kuku wa kienyeji, mbuzi, nk.) kwenye shamba la ukubwa wa ekari 7 lililopo wilaya ya Bahi Dodoma. Natafuta mtaalamu mwenye uzoefu wa uchambuzi yakinifu wa mradi wa mifugo. Nahitaji mtaalamu anisaidie kufanya yafuatayo:
1. Kutembelea eneo na kukusanya taarifa, takwimu za haraka (rapid) na kufanya uchambuzi utakaosaidia upangaji biashara kwa kutumia ushahidi (Mshauri hatahitajika kuandaa mpango halisi wa biashara) --- siku 2
2. Kwa kuzingatia takwimu kwenye Na. 1 hapo juu, kushauri kuhusu kufaa kwa eneo husika kwa ufugaji wa kuku wa kienyeji, mbuzi, kondoo, ng'ombe, nk. kibiashara (angalau faida ya asilimia 20 ya mtaji uliowekezwa) --- siku 1
3. Kushauri kuhusu mpango wa matumizi bora ya ardhi, makadirio ya gharama za miundombinu na uendeshaji kwa kuzingatia matumizi ya malighafi zinazopatikani hapo kijijini, rasilimali watu na malighafi zinazohitajika kuendesha shamba kwa siku, wiki, mwezi, mwaka, nk. na matarajio ya uzalishaji (idadi ya mifugo inayokomaa kwa wiki, mwezi, mwaka, nk.) ---- siku 2
4. Kushauri kuhusu masoko
5. Jumla ya siku za utaalamu zinakadiriwa kuwa siku 5
6. Haihitajiki ripoti ndefu. Kurasa 10 zenye takwimu kujibu Na. 3 zinatosha kabisa.
7. Mwenye ujuzi, uzoefu na muda wa kuifanya hii kazi kuanzia mapema mwezi Juni 2020 anijibu tafadhali.
8. Sifa ya mwombaji: awe na elimu ya juu katika fani ya mifugo