Mtaalamu: Mafuriko yanayotokea Tanzania ni neema na fursa kubwa kiuchumi

Hivi punde

JF-Expert Member
Apr 1, 2017
2,554
8,581
Wakuu. Mm ni mtaalam wa maswala ya maji na umwagiliaji. Mtaalam wa kusanifu, kusimamia na kuendeleza miundombinu ya maji na umwagiliaji.

Kuna kitu kinaitwa "Spate Irrigation or Flood Irrigation". Hapa unaweza kulima kwa kutegemea tu maji ya mafuriko yaliyotapakaa maeneo yanayofaaa kwa kilimo. Kwa lugha nyingine ni kilimo kwa kutokana na uvunaji wa maji ya mvua. Maji yanaelekeza sehemu salama yanaenda kutulia huko, yakipungua kidogo, wakulima wanapanda mazao ya mbogamboga na mahindi. Haya huchukua muda mfupi kukomaa (miez 3 mpaka 5).

Maji ya mafuriko yanatakiwa yaelekezwe kwenye mkusanyiko kama mabwawa, madimbwi ambayo yatahifadhi maji kwa muda mrefu. Baadae watu watayatumia kunyweshea mifugo na kumwagilia mbogamboga.

Ugabda wanatumia sana hii aina ya kilimo na wanakuwa na chakula cha kutosha sana. Penye maji kuna mali, maji ni fursa, maji ni uhai.

Tuwekeze kwenye miundombinu na njia salama kwa ajili ya kuelekeza maji ya mafuriko kwenda sehemu sahihi kwa ajili ya matumizi yetu wenyewe. Maana maeneo mengi ambayo yanakumwa na mafuriko, ni ya ukame na wananchi wamekuwa wakilalamika swala la njaa.

"Miundo mbinu, miundombinu jamani". kilimo kinatoa sana. Hakina direct taxes za kumuathiri mkulima, agricultural inputs nyingi ziko VAT exempted.

Wasalaam.
 
Unaweza kusaidia nika level shamba langu la mpunga la acre 100? Niambie tafadhali tuwasiliane
 
MKUU UMEONGEA POINT SANA, NILIKUWA NAWAZA JE TANZANIA INAWEZA KUVUMBUA TEKNOLOJIA YA KUVUNA MAJI YA MVUA YAWE NEEMA NA SIO MAAFA
 
Back
Top Bottom