Mtaalam: Watanzania mnadanganywa Stiglers Gorge haiwezekani kwani Kina cha Maji Mto Rufiji kinapungua mno

unaongelea River Rejuvenation ww unaejiita mtaalam,mbona hiyo ni constant sana duniani kote,kubadilika kwa kina cha maji ya mto husababishwa na sababu nyingi,pia kubadilika huku kinaweza kukawa kwa msimu,mwaka,au hata miaka kadhaa,pia kubadilika huku sio lazma iwe kupungua tu kwa kina cha maji,kina kinaweza kikaongezeka pia,sasa kwann hujawaza kuhusu sababu zilizopelekea kupungua zikibadilika na kuwa sabab zitakazoongeza kina cha maji ktk bonde la mto Ruaha????toa sababu nene ww mtaalam,kama haya ni mawazo ya kitaalam bas kupitia ww jamii tuamini kuwa tuna wataalam wa hovyo sana
Mnapowekwa kwenye mgao kisa Mtera maji yana kina kidogo, au kuna tope huwa mnaelewa nini?...... Msishambulie tu kwa kudhani mpo sahihi.....
Wengi mmewashambulia sana lakini mwishooooniii mkaja kuamini walichokuwa wanakisema.......
 
Ni kizungumkuti watu wachajipigia mahera wamesepa kama lowasa sasa wamekuja na mradi mwingine ili waendelee kutengeneza njia ya kupiga hera za wachovu
Huu mradi ametolea ushauri kama mtaalamu sawa, atwambie umeme wa gas alishaulije kipindi kile unashupaliwa na sospeter mhongo kuwa ni mwarobaini wa umeme nchini mpaka Leo haieleweki
 
Asante Mtaalamu kwa Ushauri,sasa bwana mtaalamu kwanini ushauri huu haukuutoa mapema wakati project tu imeanzishwa?,why now?
kwa sasa tunaomba uwaachie wataalam wenzio waendelee na kazi kwani tulipofika ni pazuri ngoja wamalize halafu tutaruhusu maoni baadae😁
Nani wa kumpelekea anayeshaurika? Wa chini yake wote wakipelekea kilicho tofauti na atakacho MKUU, wanawatimua waletaji kabla hajijafika juu....
 
Hakuna kitu kinachohuzunisha katika nchi yetu kama ukuaji mbaya wa siasa hasa katika eneo la uadilifu na uwajibikaji .

Siasa za kanyaboya ndio zinaonekana siasa safi na hii ni tatizo la afrika nzima si vyama tawala tu bali hata vyama pinzani kumekuwa na mambo ya kufunikiana mapungufu na kuingilia utaalamu kwa mfumo kama wa “BOGUS PIPELINE APPROACH “

Matokeo yake wasomi (wanataaluma) huwekwa nyuma na kila jambo kufanywa kimazoea angalia kwenye kodi,vikokotozi vya wastaafu,ongezeko la mshahara,makato ya PAYE nakadhalika.

Hili swala la Stiglers Si jambo baya na kiukweli kabisa ni mapinduzi yenye nia madhubuti na ya dhati kutatua kero na uhaba wa nishati katika nchi yetu lakini ningependa kutahadharisha juu ya ushirikishwaji wa wataalamu ili mradi huu uwe na tija kwa taifa letu.

Kuna siku nilipita pale viwanja vya kijitonyama maarufu kwa jina la SAYANSI nikaangalia zile ofisi za tume yetu picha ikanijia ya vijana waliosoma sayansi za IT wanavyolalamika swala la ukosefu wa ajira na changamoto zake nikajiuliza tume hii inadeni kubwa kwa wanasayansi wa TANZANIA inadeni kubwa kwa watanzania haijafanya sehemu yake.

Miradi hii ya maendeleo isiposhirikisha wataalamu wazawa wenye uzalendo tutarudi kulekule kwa DART na mafuriko ya jangwani
 
Kwenye wengi pia kuna mengi. Kuwalazimisha wote waone kitu kimoja sawasawa na anachokiona yule, ni ndoto.
Watu zaidi ya m50 wafikiri na wakubali mawazo ya mtu mmoja tu, ni ndoto pia. Ndo maana wanatumia nguvu kubwa sana kujaribu kila mmoja wetu aamini kwamba hii ni 6 wakati upande wapili wao wanaona 9.

Kosa kubwa sana la kikatiba mumrundikia madaraka mengi hivyo na kinga yote hiyo mtu mmoja tu kati ya zaidi ya watu m5 na Nchi kwa ujumla.
Huu mradi ulibuniwa kabla ya Magufuli
 
Mwambie huyo mtaalam ampelekee taarifa kamanda msaliti ili akatushitaki ubeberuni apate pesa ya kujikimu. Tumechoshwa na ubabaishaji wenu na porojo za kila siku.
 
Hapana, hatuachi kufanya vitu kwa kusikiliza, acha tufanye hivyo hivyo, tukiharibu au kupoteza pesa tutakuja na uongo wa kujisafisha, tutatumbua tumbua ki uongo na kweli yatapita kama yanavyopita mengine...



Cc: mahondaw
 
An Eagle,
Huyu mtaalamu ndiyo mzalendo wa kweli maana ametoa angalizo ambalo walio karibu na wenye mamlaka ya maamuzi hawawezi kusema kweli daima.
 
" Nasikitika sana Mamlaka husika za Tanzania kwa kuendelea Kung'ang'ania huu Ujenzi wa Mradi wa Stiglers Gorge wakati Sisi Wataalam tumeshatolea Ufafanuzi wa Kutosha kuwa kwa sasa hili jambo linaweza lisiwezekane kwakuwa Maji ya Mto Rufiji hadi vyanzo vyake kila Siku yanapungua Kina chake. Watu wa Mazingira na wale Wasaidizi wa Rais kwanini hawamuambii huu ukweli ili kufanyike utaratibu mwingine na badala yake wanamdanganya tu na kumpa Moyo wakati hali si shwari? " amesema Mtaalam.

Tujadili.
Hata kina cha bahari pia kinapungua,ziwa victoria linapungua
Tutajenga tu hata maji yakiisha yote,tutafanya kutuo cha utalii
Pinga pinga mnahaha sana
 
Mnachosahau waandikaji kama nyie ni kuwa Viongozi hawahavgaikiii umeme kwa ajili yao wenyewe. Sina la ziada mana
" Nasikitika sana Mamlaka husika za Tanzania kwa kuendelea Kung'ang'ania huu Ujenzi wa Mradi wa Stiglers Gorge wakati Sisi Wataalam tumeshatolea Ufafanuzi wa Kutosha kuwa kwa sasa hili jambo linaweza lisiwezekane kwakuwa Maji ya Mto Rufiji hadi vyanzo vyake kila Siku yanapungua Kina chake. Watu wa Mazingira na wale Wasaidizi wa Rais kwanini hawamuambii huu ukweli ili kufanyike utaratibu mwingine na badala yake wanamdanganya tu na kumpa Moyo wakati hali si shwari? " amesema Mtaalam.

Tujadili.
 
Back
Top Bottom