Kwanza TV
Member
- May 2, 2017
- 33
- 69
Mtaalam wa picha za ndege (Aviation Photographer) anayetumia jina la Woody Aeroimages ameithibitishia Kwanza TV kuwa ndege iliyoagizwa na Tanzania ni LN19 ambayo ni mmoja ya "Terrible Teens" kama ilivyoelezwa na mbunge Zitto Kabwe bungeni wiki iliyopita.
Kupitia mtandao wa Twitter, akaunti ya Woody Aeroimages imeweka picha ya ndege hiyo ikiwa nyeupe bila nembo na pia bila injini kuonekana.
Kufuatia swali la kuhakikisha kuwa picha hiyo ni ya ndege yenyewe iliyowekewa oda na Tanzania, Woody Aeroimages imethibitisha kuwa ni picha halisi.
Kwanza TV inaendelea kufuatilia suala hili ndani na nje ya nchi.
UPDATE: Woody Aeroimages amesisitiza kuwa kitaaluma yeye ni mpiga picha mtaalam wa ndege. Tumefanya marekebisho hayo ili kuweka habari iliyo na uhakika zaidi.
Woody Aeroimages pia ameeleza kuwa kutokana na kazi yake ana vyanzo vingi ambavyo anafanya navyo kazi kwa karibu katika makampuni ya ndege ikiwemo Boeing. Ametuhakikishia kama taarifa alizopewa na vyanzo vyake vya kuaminika zikithibitika siyo za kweli basi ataiweka wazi.
Update 2:
Woody Aeroimages amerudi na jibu muda si mrefu na kusema anarekebisha taarifa yake pamoja na kuwa awali alithibitisha kuwa Tanzania ilipata LN19. Sasa amesema amethibitisha hivi punde kutoka vyanzo vyake Boeing kuwa ni LN719
Kama tulivyowaahidi tunaendelea kuwaletea habari mpya kadri tunavyovipokea.