Mtaalam wa Kijeshi: Harmonize ametuaibisha Makomandoo kwani alitua Kishamba na Kizembe kama gunia la viazi mbatata

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,544
108,872
"Nilikuwa naliangalia lile tukio zima ila nilipoona tu ghafla Msanii Harmonize anapita juu kwa ile Kamba kama Mtu wa Medani nilichukizwa mno kwani hakuonyesha hata tu 5% ya kwamba Yeye ni Mjeshi na alikosea mambo mengi ya Kimsingi sana huku ile tua yake kama Gunia la Viazi Mbatata limerushwa kutoka katika Lori, kutupa Bendera huku akihema hadi kupatwa na Kizunguzungu liliharibu kila Kitu. Rai yangu tu kwa hawa Wasanii waache Kujiita Majina ambayo hayaendani nao Kiuhalisia na bora ya hata huyu sijui Diamond anavyojiita Simba kwani ni kweli kabisa ukimuangalia mambo mengi ni makubwa na ya Kujiamini kama alivyo Simba halisi"

Haya mnaopingana na huyu Mtaalam wa Kijeshi jitokezeni mtoe Hoja zenu za Maana na wale mnaomuunga mkono karibuni katika Kumpongeza tu.
 
Uanajeshi n ukakamavu,ushawah ona wanashuka na #parachute# skydivers wanashukaje? Sio kila kitu ujikute unachambua kana kwamba unajua. Haaaah kwa tuliopitia mafunzo twajua jamaaa kajitahd na kwa MTU wa kawaida hawezi Fanya .

Alichofanya #HARMONIZE# JESHI# KONDEBOY# kilitakiwa kifanywe na MAKOMANDOOO MBELE YA MH: RAISI KUADHIMISHA MIAKA 59 YA UHURU MWAKA HUU...

#Risk aliyoichukua ndio iliwaogopesha watu,na ndio kilichothibtsha kuwa usaniii ni zaid ya make- up na #ON STAGE BLAAHBLAAH
 
Kuna siku mtu atafia kwa mkapa sababu ya kufurahisha umati, he took that risk just to please " Wananchi"

Inahitaji mazoezi maalumu ya kimedani hasa uvukaji vikwazo kwa kutumia kamba na nyenzo nyinginezo, bahati yake hiyo na ingependeza Kama polisi wangeonya juu ya hizi risk stunts zisizo na ufahamu wa kina.

Siyo Jambo la kupongezana Hilo, it's too risky!
 
SIBANDUKI HAPA MPAKA SARA ALETE MREJESHO IKIWA JOGOO LINAPANDA MTUNGI MAANA NAHISI PINGILI ZA SPINAL CODE ZIMECHEZA SEMA ANAJIKAZA

Mkuu jana 'nilicheka' sana tu hasa pale alipokuwa kila 'akitambaa' angani na ile Kamba halafu akiangalia chini ni mbali huku kila mara akionyesha kabisa 'Ishara' za kwamba anaomba 'Majamaa' wamshushe kwani alikuwa 'ameshachoka' ila 'Majamaa' nao wakaamua 'Kumkazia' vile vile na taratibu nikaanza kuona 'Machozi' yanamtoka na ghafla baadae nikaona 'Kadondosha' Bendera na kuna wakati tuliokuwa tukimtizama katika Runinga ( Television ) ya Azam tulianza kusikia 'Milio' fulani hivi ya 'Ngurumo' tukajua ya kwamba ama alikuwa 'anajamba' kwa 'Kitete' chake au pengine hata 'Chembe Chembe' za 'Haja Kubwa' zilikuwa zinaanza Kubisha Hodi 'Makalioni' mwake. Ile 'tua' yake tu kama Gunia la Viazi Mbatata huku akisimama kwa dakika kama Tatu hivi akiwa na 'Kizunguzungu' tukajua kuwa tayari alishayaharibu 'Mazingira' yake ya 'Unyabeni' na ndiyo maana alipomaliza tu Kuimba pale 'alichomoka' mbio mno kuwahi zake Maliwatoni ( Chooni ) pale Taifa VIP Wing.

Watu wanajifunza mambo hayo ndani ya Miezi na hata Mwaka ili 'Kuyaweza' hasa 'Kimedani' halafu linatokea 'Pimbi' moja linataka Kuiga. Mtakufa!
 
Itoshe tu kusema Simba imekua ni Benchmark kwenye soka la Tanzania.

Baada ya Simba day kuanzishwa sasa kuna siku ya mwananchi pia kuna ile ya Azam.

Baada ya Simba kumleta msanii adimu Afrika Mashariki na kati kupiga show kwenye Simba day...Azam wakakimbilia kwa Ally Kiba huku Yanga wakielekea kwa Konde boy mjeshi.

Baada ya Simba kumleta uwanjani msanii nguli Diamond Plutnumz Chibu Dangote aka Simba kwa kutumia Helicopter....Ndiyo sasa tukaona vituko vya Konde boy kujipa zoezi guuumu...ilimradi kujifananisha na bosi wake huyo wa zamani...ambaye pia ni mentor wake anayemuiga mpaka sauti..kama ilivyo kwa timu iliyompa tender ya kutumbuiza Siku hiyo inavyowaiga wababe wa Afrika Mashariki na kati Simba Sports kwa kila kitu...anyways siyo mbaya ni wivu wa maendeleo.

Itoshe tu kusema Simba Baba Lao..Pia hongera timu ya Simba kwa kuchukua Ngao Ya Hisani Kwa Mara ya nne mfululizo...Wabheja Sana
 
"Nilikuwa naliangalia lile tukio zima ila nilipoona tu ghafla Msanii Harmonize anapita juu kwa ile Kamba kama Mtu wa Medani nilichukizwa mno kwani hakuonyesha hata tu 5% ya kwamba Yeye ni Mjeshi na alikosea mambo mengi ya Kimsingi sana huku ile tua yake kama Gunia la Viazi Mbatata limerushwa kutoka katika Lori, kutupa Bendera huku akihema hadi kupatwa na Kizunguzungu liliharibu kila Kitu. Rai yangu tu kwa hawa Wasanii waache Kujiita Majina ambayo hayaendani nao Kiuhalisia na bora ya hata huyu sijui Diamond anavyojiita Simba kwani ni kweli kabisa ukimuangalia mambo mengi ni makubwa na ya Kujiamini kama alivyo Simba halisi"

Haya mnaopingana na huyu Mtaalam wa Kijeshi jitokezeni mtoe Hoja zenu za Maana na wale mnaomuunga mkono karibuni katika Kumpongeza tu.

Yaani huyu atafia mbele za watu na sifa za kijinga, na Utopolo hawatalipa hata sent tano kama fidia. Mishahara tu kitendawili plus jezi zimekwama hapo nani liu... ashauriwe kiki nyingine zitamzimisha moja kwa moja.

Walioona lile tukio watakubaliana na ukweli kwamba ule mgongo ulipigizwa km mara tatu hivi na tulimuona msanii huyo akitoa macho kama kapoteza network uwanja ulikuwa kimya dakika kadhaa ukiomba Mungu awaepushie UTOPOLO AIBU ile.

Wakulaumiwa ni uongozi wa huyo dogo walikosa idea? Hata reheasal hawakufanya?
Hivi walimuona Mjeshi gani anashuka kwa kupiga matako yake chini? Si atakufa vitani?

Naungana na wewe.... labda mjeshi mavi
 
Ndo maana wasanii makini hufanya maandalizi "rehearsal" kabla ya siku ya tukio na ikifika hiyo siku hufanya kazi yao kwa ufanisi wa hali ya juu.

Akumbushwe msemo usemao, "Usiige ...ya kwa Tembo, utapasuka msamba".

Na huyo alieruhusu hicho kitendo kuwekwa kwenye ratiba anastahiki semina elekezi.

Huyu msanii hana sifa za kufanya kitendo hicho.
 
Back
Top Bottom