SoC02 Mtaala Wa Elimu; Nini tuboreshe kwenda sambamba na madadiliko ya Dunia

Stories of Change - 2022 Competition

prototypeman

JF-Expert Member
Apr 4, 2014
288
108
Habari wakurungwa wa Jamii Formu.

Nakumbuka nilipokuwa mdogo yapata kama mtoto wa darasa la tatu hivi, siku moja nilikuwa na mzee wangu akaniambia jitahidi sana kusoma kwani elimu yako ndio ufunguo wa maisha yako.

Kwa kweli sipingani na ushauri wa mzee maana miaka ile ya 2000 mwanzoni mwanzoni kauli hii ilikuwa hai na sio mimi niliyetamkiwa hii kauli natumaini watu wengi tuu humu tushakutana nayo kutoka kwa watu wetu wa karibu.

Elimu ni swala muhimu sana kwa ustawi wa jamii na maendeleo ya Taifa, lakini ifike wakati tukubali kuwa ile kauli ya elimu ni ufunguo wa maisha kwa sasa inatunyoosha maana kufuli limebadilishwa na funguo tunayotumia ishapitwa na wakati na haina uwezo wa kufungua kufuli kwa haraka, kwa maana hiyo ni lazima tubadili funguo ili kauli hii isionekane miyeyusha kwa vijana wengi wa kitanzania, nauhakika huwa mnasikiaga minong'ono huko mitaani " Jamaa ana degree ila tupo nae mtaani tuu hana mbele wala nyuma" Lakini miaka ile ya 2000 kushuka chini kijana wa form 6 tuu anapata heshima zote za mtaa.

Kuna changamoto nyingi sana katika mfumo wa elimu wa sasa, ikiwemo wahitimu kukosa maarifa ya msingi unakuta kijana aliemaliza form 6 hata kutumia microsoft word kuandika barua kwa mchumba hawezi, mtoto aliemaliza darasa la saba hawezi kusoma wala kujibu table ya 9 kwa ufasaha( 9×1,9×2.....) na vijana wengi waliamaliza chuo hawana umahiri na walichosomea.

Juzi juzi hapa nilisikia Wizara Ya Elimu ipo mbioni kubadili mtaala wa elimu. Nikajiuliza huu mtaala watakao ubadili utaendena na ulimwengu wa sasa unaohitaji watu wenye uwezo mkubwa katika nyanja ya Sayansi,Teknolojia na Sanaa? Au tutapunguza topic za mambo ya kds na kks na stori ya kina Mkwawa? Hapa bado sijui wacha tuendelee kugonga mtori labda nyama zipo chini.

Tufanye haya kuunda Elimu bora na yenye tija katika Taifa letu

Awali nilitangulia kusema funguo tulioaminisha na wazazi/walezi inafungua kufuli lilifunga maisha ni miyeyusho kwa nyakati hii.

Nasema hivyo kwa sababu kuna lundo la vijana mtaani wana elimu nzuri lakini bado maisha yanawapiga vitasa vya Mandogo na mateke ya punda. Hapo hapo unaweza kuta kijana hajui cha lufanya na mtaji anao( inastajabisha sana) ila sio kosa letu vijana bali ni mfumo mbovu wa elimu yetu.

Baada ya kusema hayo machache naomba nielezee jinsi gani tunaweza kuboresha elimu yetu ikawa bora zaidi.

Mosi, Tuboreshe maslai ya wafundishaji.
Tunaweza fanya yote kama tulivyoona awamu ya 5 na 6 inavyofanya kama kujenga madarasa, maabara kwa shule za sekondari, kuondoa ada nk ila bila kuboreshe maslai mazuri kwa mwalimu tusitarajie kuwa na wahitumu mahiri
wengi kutoka shule za serikali.

Pili, Tuondoe masomo yasiokuwa na maana katika mtaala, napendekeza shule za msingi kuanzia darasa la kwanza hadi la nne kuwe na masomo manne tuu yaani,
1. Hesabu 2. Kiswwhili( kuandika na kusoma) 3. Sayansi na 4. Sanaa

Darasa la 5 hadi 7 kuwe na masomo 5 tuu,
1. Hesabu
2. English( kuonge na kuandika)
3. Sayansi
4. Uraia
5 Tehama ya Habari( ICT)

Secondari kidato cha kwanza hadi cha nne kuwe na masomo matano tuu hapa mtoto achague anapendelea mchepuo gani kama ni sanaa, biashra au sayansi ndio ataanza nao kuanzia form one.

Mfano
1. Physics, chemistry, Math ICT plus Englishi(Speaking and writing)
2. Book-keeping, commerce, Math, ICT and English( S&w)
3.HGK, ICT plus English, HGL plus ICT etc
Kwa ujumla English na ICT ni masomo ya lazima isipokuwa wanaosoma HKL na HGL watakuwa na ICT kama compulsary.

Katika mtaala topic zichanganywe zile za Olevel na Alevel kulingana na uhitaji na umuhimu watoto wasome miaka mnne Then waende Chuoni moja kwa moja wakitimiza sifa zitakazowekwa na TCU.

Haya ndio mawazo yangu, unaweza kujiuliza kwa nini nimeweka ICT na English kuwa compusaly kwa nini isiwe Ujariamali.

Ni hivi ICT na English ni masomo muhimu sana kwa utandawazi wa sasa vijana wakiwa vizuri kwenye haya masomo mawili ni rahisi sana kuchangamana na watu wa mataifa mengine kama USA na Nigeria, kuna fursa nyingi sana za kazi huko mitandaoni mfano mzuri ni Upwork, Freelancer dot com, Fiver, Amazon nk bila kuwa na ujuzi wa ICT na kutumia English vzr ni vigumu kushiriki fursa za mitandaoni.

Pia nchi nyingi kama Canada,USA kuna kazi huko za kutosha ila ukiangalia idadi ya watanzania ni wachache sana kuliko ya wakenya na wanaija pamoja na wasouth Africa tena wengi wanaochangamkia fursa huko unakutana ni vijana wa form 4 leavers, lakini ukija hapa bongo form 4 leaver hata kutumia adobe photoshop hawezi, maana yake tunatengeneza Taifa la vijana wenye kutegemea ajira rasmi tuu na ni mbaya sana kwa ustawi wa Taifa.

Nakaribisha maoni na pale niliposea nipe tayari kurekebishwa.
 
Naomb kabla sijauliza naomb nipewe fact ili jarida lako lime base katika control based and competence based?
 
Then apo naomb unitajie nchi zinazoendelea tano zinazotumia huu mfumo ?
Sijashauri tuangalie nchi nyingine yaani tu copy mfumo wa nchi nyingine bali lengo ni kuwa na mfumo wetu utaomfunya muhitimu kuwa competent na kuendena na dunia ya sasa, katika huo mfumo kidogo nimegusia nchi ya Kenya na Nigeria hada katika somo la ICT kupewa kipaumbele Msingi na Sekondari, Kenya kwa sasa shule ya msingi wanasoma coding tunaweza kuona kama ni jambo la ajabu ila kulingana na dunia inapoelekea matunda yake yataonekana baadae.
 
Sijashauri tuangalie nchi nyingine yaani tu copy mfumo wa nchi nyingine bali lengo ni kuwa na mfumo wetu utaomfunya muhitimu kuwa competent na kuendena na dunia ya sasa, katika huo mfumo kidogo nimegusia nchi ya Kenya na Nigeria hada katika somo la ICT kupewa kipaumbele Msingi na Sekondari, Kenya kwa sasa shule ya msingi wanasoma coding tunaweza kuona kama ni jambo la ajabu ila kulingana na dunia inapoelekea matunda yake yataonekana baadae.
Ujaelewa swal ivi nchi zinaendelea zinatumia mfumo gan wa elimu
 
Ujaelewa swal ivi nchi zinaendelea zinatumia mfumo gan wa elimu
Kuna kitu kimoja ambacho nadhani kila mtu atakubali. Mfumo wetu wa elimu siyo mzuri na hauendani na mazingira na wakati. Kama ni hivyo, suala liwe ni kuchangia kwa kuboresha au kufuta kabisa alichoandika na kuandika kipya kama hatukubalini naye. prototypeman kwangu mimi nadhani kitu ambacho tungezingatia kama nchi kingetutoa kwenye umaskini bila kuhitaji wawekezaji wengi na mitaji mikubwa ni kilimo. Nchi yetu ina ardhi na hali ya hewa nzuri sana hivyo tungewekeza kwenye kilimo na kulifanya somo la kilimo liwe la lazima kwa kila shule, huku tukiwa na mashamba ya kufanyia practicles kwa university level tungeweza kupiga hatua haraka.
 
Kuna kitu kimoja ambacho nadhani kila mtu atakubali. Mfumo wetu wa elimu siyo mzuri na hauendani na mazingira na wakati. Kama ni hivyo, suala liwe ni kuchangia kwa kuboresha au kufuta kabisa alichoandika na kuandika kipya kama hatukubalini naye. prototypeman kwangu mimi nadhani kitu ambacho tungezingatia kama nchi kingetutoa kwenye umaskini bila kuhitaji wawekezaji wengi na mitaji mikubwa ni kilimo. Nchi yetu ina ardhi na hali ya hewa nzuri sana hivyo tungewekeza kwenye kilimo na kulifanya somo la kilimo liwe la lazima kwa kila shule, huku tukiwa na mashamba ya kufanyia practicles kwa university level tungeweza kupiga Mawazo na

Kuna kitu kimoja ambacho nadhani kila mtu atakubali. Mfumo wetu wa elimu siyo mzuri na hauendani na mazingira na wakati. Kama ni hivyo, suala liwe ni kuchangia kwa kuboresha au kufuta kabisa alichoandika na kuandika kipya kama hatukubalini naye. prototypeman kwangu mimi nadhani kitu ambacho tungezingatia kama nchi kingetutoa kwenye umaskini bila kuhitaji wawekezaji wengi na mitaji mikubwa ni kilimo. Nchi yetu ina ardhi na hali ya hewa nzuri sana hivyo tungewekeza kwenye kilimo na kulifanya somo la kilimo liwe la lazima kwa kila shule, huku tukiwa na mashamba ya kufanyia practicles kwa university level tungeweza kupiga hatua haraka.
Wazo ni zuri kaka
 
Back
Top Bottom