Mtaala Mpya wa Elimu uko tayari, utafikishwa kwa Wadau wa Elimu kwa mapitio

Kubadili mtaala wa elimu sio kazi ndogo maana ni kubadili mfumo mzima wa Elimu kwa wananfunzi ikiwemo walimu, zana za kujifunzia na kufundishia pamoja na wadau wote wa elimu nchini, nasubiri kuisikia gharama yake kubwa itakapofikia kwenye kuutekeleza

Tujipongeze kwa uthubutu
 
Waziri ni mwakilishi wa rais kisera na kisiasa kwenye wizara, ila kwenye wizara kuna wataalamu wa kiufundi kwenye hio wizara, changamoto inakuja pale waziri anapoingia maswala ya kitaamu na kiufundi kwenye hio wizara .

Wizara ya elimu ni wizara athirika na sera na mambo ya kisiasa dhidi ya utaalamu..
 
Nasubiria huo mtaala kwa hamu kubwa maana huu uliopo umepitwa na wakati mpaka basi.

Elimu ya Tehama, Ufundi stadi, biashara, michezo, ujasiriamali na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali; vioewe kipaumbeke kwenye huo Mtaala mpya.
 
Kubadili mtaala wa elimu sio kazi ndogo maana ni kubadili mfumo mzima wa Elimu kwa wananfunzi ikiwemo walimu, zana za kujifunzia na kufundishia pamoja na wadau wote wa elimu nchini, nasubiri kuisikia gharama yake kubwa itakapofikia kwenye kuutekeleza

Tujipongeze kwa uthubutu
Kiswahili kutakua lugha ya kufundishia!?
 
Nasubiria huo mtaala kwa hamu kubwa maana huu uliopo umepitwa na wakati mpaka basi.

Elimu ya Tehama, Ufundi stadi, biashara, michezo, ujasiriamali na uzalishaji wa bidhaa mbalimbali; vioewe kipaumbeke kwenye huo Mtaala mpya.
Jaji mkuu alisema miaka michache ijayo Elimu yetu inaexpire
 
Kuna ujinga unaenezwa hapa nchini kuwa eti mitaala yetu ni mibovu hivyo inafanya wasomi wetu wawe watu wa kukariri tu na kupelekea wasiweze kujiajiri.

Hivi wale wasomi wa SUA, wamekariri? Hawajawahi kujifunza kwa vitendo jinsi ng'ombe, mbuzi na wanyama wengine wanavyozalishwa na kulishwa?

Hawa wasomi wa SUA hawajawahi kuona mimea insvyotunzwa na kuzalishwa?

Bila shaka majibu ni kwamba wamefundishwa kwa vitendo namna ya kuzalisha, kulea na kukuza mifugo na mimea. Sasa kwann hatuoni hawa wasomi wa kilimo wakijiajiri kwenye kilimo?

Hapa nchini kuna kundi kubwa la vijana na wasomi wamejiajiri kwenye bodaboda, mama ntilie na umachinga. Nani aliwapa elimu hii? Chuo kipi hapa nchini kinatoa elimu ya bodaboda, umachinga na mama ntilie?

Kitendo cha wizara ya elimu kujaribu kubadili mitaala ni sawa na kutupa jiwe gizani. Ni mradi wa wakubwa wa wizarani kutaka kupiga hela za semina na uandaaji na mafunzo ya mitaala mpya utakaopatikana.

Ujinga mwingine unapigiwa chapuo.
Halafu watanzania wapo kimyaaa. Wapo bize kumuongelea "Mtu Kazi", Simba na Yanga.
 
Back
Top Bottom