Mtaala Mpya wa Elimu Kenya, Competency Based Carriculum (CBC). Sisi bado tuko busy na kukaririsha watoto

BLACK MOVEMENT

JF-Expert Member
Mar 11, 2020
2,704
6,499
Kenya wameisha anza mfumo wao mpya wa elimu wa CBC yaani Competency Based Curriculum, huu mfumo unachukua nafasi ya mfumo ulio kuwepo ambao ni sawa tu na wetu kwa sasa, mfumo wa Mwalimu kuingia na chaki na kuanza kuandika na watoto kuandika au kukariri.

Huu mfumo wao mpya unafuta pia mitihani ya Taifa, hivyo kwa walio anza na huu mfumo hawatakuwa na kitu kinaitwa mitihani ya Taifa bali watapimwa mashuleni mwao.

Huu mfumo pamoja na kwamba ni ghari sana lakini ni mfumo mzuri kabisa wa wakati huu, huu mfumo watoto wana fanya Practical zaidi, group work na Group Discusion kuliko kaukaririshwa vitu na Kwa wale wenye watoto wanao soma zile shule za mbele za International School, wanatumia sana huu mifumo pia.

Tanzania bado tunawakaririsha wanafunzi, kuna she moja nilishangaa kukuta Wanafunzi wa Darasa la saba tangu janauary hadi wanahitimu walikuwa wana solve tu past paper, yaank ni mwendo wa past paper mwanzo mwisho, tujiulize mwanafunzi anapata nini kwenye hizo past paper zaidi ya kukariri?

Pia hii mifumo ya mitihani ya Taifa isha pitwa na wakati, na hii ndo inafanya shule zijikite kukaririsha watoto past paper, watoto wanafundishwa kujibu paper na sio kuelewa mambo.

Tuna lag behind.
 
Yes Jamaa wamefuta na waliopo wana maliziai malizia, sio Kenya tu nchi nyingi zisha achana na hii mambo ya mitihani ya Taifa ya kushindanisha mashule, ni Mfumo wa elimu wa zamani sana sema kwetu ni fasion sana
 
Huu mfumo nashangaa watu kuushangilia, hii ya kushindanisha mashule ni academic suicide, Shule hujikita kuandaa watoto kujibu mitihani ikiwemo kusolve past paper mwaka mzima. Watoto nje ya Mitihani hakuna wanacho toka nacho shuleni, na triend huenda Secondary hadi Chuo, angalia watoto wa Secondary hakuna wanacho toka nacho pale na now day hata vyuoni
 
Kenya wameisha anza mfumo wao mpya wa elimu wa CBC yaani Competency Based Curriculum, huu mfumo unachukua nafasi ya mfumo ulio kuwepo ambao ni sawa tu na wetu kwa sasa, mfumo wa Mwalimu kuingia na chaki na kuanza kuandika na watoto kuandika au kukariri.
Wanatumia lugha ya kiEngereza bado.. au Kiswahili?
 
Safi Sana. Elimu yetu ni Ile alioicha mkoloni hadi sasa ndo hiyo hiyo. Kipindi kile ilikuwa kuwaanda watu kwa ajili ya kufanya kazi maofsini lakini siku hizi maisha yamebadilika,lakini elimu ni Ile ile.
Wabadilishe mfumo mzima wa elimu
 
Uzuri wa Kenya kuna mambo wakianza kuyakadili huwa wanaacha siasa...

Hapa lazima tuwaulize kwanza ndugu zetu UVCCM na kaka zao pale viunga vya UDOM wanasemake mjengoni aka chama cha wakulima na wafanyakazi..hahahaha
 
Na wanaenda kuondoa class 7 & 8
Basi wanangu wanapenda kutembea sijui ndo study tour yaani kuna muda naona uzungu utakuja uwapoteze wanangu na wanankera sana hasa kunikosoa na 7 langu

Mbona hakuna cha ajabu hapo,hizo study tour zipo siku zote tena mashule kibao tu hapa hapa Bongo, au unadhani hiyo mitaala kwa hapa Bongo hakuna? Sema hivi,uwezo wa ku afford School fees kwa shule za hiyo mitaala ndiyo mtihani lakini Shule zipo tena nyingi tu,wewe tu na Wallet yako,ukitaka hata wawe wanaongea ile English kama ya kwa Malikia zipo pia,nenda pale Braeburn,HOPAC,ISM,IST na nyingine nyingi tu zipo hapa hapa Bongo.
 
Hio mitala ipo shule zipi? Landa unazungumzia Internatioanal School ambazo hazifuato mitala ya Bongo. Ila unataka kusema hizi hizi shule za kawaida kuna zenye mitaala yao? Hahaa na paper je?
 
Mbona hakuna cha ajabu hapo,hizo study tour zipo siku zote tena mashule kibao tu hapa hapa Bongo, au unadhani hiyo mitaala kwa hapa Bongo hakuna? Sema hivi,uwezo wa ku afford School fees kwa shule za hiyo mitaala ndiyo mtihani lakini Shule zipo tena nyingi tu,wewe tu na Wallet yako,ukitaka hata wawe wanaongea ile English kama ya kwa Malikia zipo pia,nenda pale Braeburn,HOPAC,ISM,IST na nyingine nyingi tu zipo hapa hapa Bongo.
International school hawafuati mitala ya Tanzania, Kenya wamebadili mitaala yao kwa nchi nzima, hivi wewe ni asilimia ngapi ya Watanzania wanasoma hizo International school unazo sema? Nazani hata asilimia 1 haifiki
 
Back
Top Bottom