matunduizi
JF-Expert Member
- Aug 20, 2018
- 6,276
- 14,511
lita 1000 ya maji ya Chumvi tulikuwa tunanunua Tsh 15000.
Tuliletewa na Gari na lenyewe hadi uwe unachukua kuanzia lita 3000.
Hadi unaondoka tunaipata mubashara kwa tap Lita 1000 T-sh Kama 1500. Punguzo la asilimia
Hatukuwahi kufikiri iko siku Muujiza utatokea maji yatiririke bafuni. Nilisimama kidete kubishana nap kada babu was CCM Kuwa rais katupiga fix tu ili apate kura Anachosema hakitekelezeki.
Nilikuwa nambishia kwa fact maana nilikuwepo awamu iliyopita tulipoona mbwembwe za wachina wenye kaundasuti za kungfuu wakisimamia kwa makeke yote mradi wa Maji ambao haukuwahi kutoa maji zaidi Yale mabomba yaligeuka chakula ya mchwa.
Nilistaajabu nilipopita serikali ya mitaa kukagua maendeleo ya mtaa wangu nilipokuta shehena ya mabomba ya blue Ya Maji (nchi 6+).
Sijakaa sawa baada ya kusafiri nakuta mbele ya maskani yangu yanazikwa mabomba na mtaro umechimbwa kitambo.
Nikamfata kada Mzee wangu nikamuuliza, "nini hiki?" mzee ananiambia "Dogo usiishi kwa mazoea hiki ni chuma, kikisema jambo lazima kitokee".
Leo mtaa mzima shida sio maji shida ni ujinga mkubwa wa kataasisi kalikopewa kutusambazia maji. Wanazidiwa ari na sisi wananchi.
Nakushukuru Mama nanii ulipoamaua Kwenda kuwatolea uvivu Ofisini ukijua hawawezi kuleta nyodo maana chuma kimeshika usukani. Fasta siku hiyohiyo wakaachilia maji hadi leo. Sina hakika kama wangekuwa na wepesi huo in absence ya chuma, Mwamba, hapa kazi tu.
Mwezi ujao nitakuja Chato hapo nione ulipolazwa maana jana nilipania nikuone lakini Wapo waliopania zaidi yangu hadi wakajikuta wanaunga mkono juhudi.
Ni hayo tu...