Mswahili ni nani? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mswahili ni nani?

Discussion in 'Jukwaa la Lugha' started by bbtwins, Sep 1, 2010.

 1. b

  bbtwins New Member

  #1
  Sep 1, 2010
  Joined: Sep 1, 2010
  Messages: 3
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Nilipata kumsikia mtu akisema hangependa aitwe "mswahili". Nikapatwa na maswali mengi kichwani kwani mtu huyu alikua mzawa, mweusi na anaishi DSM.

  Kabla sijamtaka undani kwa kauli yake hii, nilidhani uswahili ni title ya mtu mwenye ngozi nyeusi na anayeishi au anayetoka kwenye jamii ya watu wa mwambao. Baada ya kuongea na huyu mtu, niligundua kuwa hata mzungu na watu wa bara wanaweza kuwa waswahili!

  Kinachomfanya mtu awe mswahili kumbe ni "hulka" - kubwa mbili zikiwa (1) kuongea zaidi ya matendo na (2) kujifanya kujua kila kitu.

  Kwa mtizamo huu, Tanzania tuna waswahili kibao, Tutafika kweli?

  ========================
  ========================
  =============================
  =========================
   
 2. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #2
  Sep 1, 2010
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  :confused2:
   
 3. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #3
  Jan 18, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,519
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Wanajf naomba tu share changamoto niliokutana nayo. Leo asubuhi nikiwa kwenye daladala naelekea mjini kati. Baada ya kuwaza na kuwazua, karibu yangu alisimama mtoto wa kike I think she is at 7 or 8 aliyekuwa amevaa sare za shule.

  Kwa kuhisi kuwa yuko embarased kutokana na foleni, nikaamua kum keep bize kwa kumpa recognition kwa kumuuliza maswali ya kitoto ya hapa na pale ali mradi tu tufike bila ya uchovu. Unaishi wapi, Unaitwa nani, unasoma shule gani na darasa la ngapi. Nikamuuliza huku nikiwa sina uhakika kama nitajibiwa vizuri swali langu. Nilishtushwa na uwezo mkubwa wa kujieleza baada ya kujibu kwa ufasaha maswali yangu ya mpigo. Du!! Nikajiona Chief mzima napigwa TKO kutokana na jibu la mtoto kwani wahenga walisema kuwa jibu likisadifu swali, ni kama kiu iliyokatwa kwa maji safi ya kisima cha chemchem.

  Mtu mzima sikutaka kushindwa kirahisi.nikamuuliza swali lingine ambalo niliamini kuwa litamsumbua kutokana na umri wake. " Umesema unaishi Kimara, Wewe ni kabila gani?" Huku nikitegemea jibu la "Mimi ni Mchaga" kutokana na maeneo mengi ya Kimara kugeuzwa kuwa mashamba ya Migomba kutokana na kukaliwa na Wachaga wengi, nilishangaa kusikia jibu alilolitoa yule mtoto. Kwa kujiamini alijibu "Mimi ni Mswahili" Huku nikiwa siamini masikio yalichosikia, nikamuuliza tena. "Umesema wewe ni kabila gani?" Akijibu kwa msisitizo na kujiamini, alisema "Mimi ni Mswahili" Nikajiona Chief mzima leo ninalo.

  Nikajitutumua na kuuliza tena. "Kwa nini unasema wewe ni Mswahili. Kwani baba yako ni kabila gani." Kwa kujiamini akajibu. "Baba yangu ni Mhehe na Mama yangu ni Msukuma. Na kwa kuwa wazazi wangu ni makabila tofauti, mimi ni Mswahili kwa kuwa sifuati mila yoyote wala situmii lugha yoyote ya wazazi wangu zaidi ya Kiswahili".

  Ghafla nikasikia sauti ya Konda, "Akiba wa kushuka". Nikajibu "tupo" bila ya kujali kuwa sikutumwa na mtu yeyote kumjibia. Nikashuka zangu huku nikijiuliza MSWAHILI NI NANI?
   
 4. drphone

  drphone JF-Expert Member

  #4
  Jan 18, 2011
  Joined: Sep 29, 2009
  Messages: 3,563
  Likes Received: 29
  Trophy Points: 145
  mswahili ni mimi na ww
   
 5. E

  Elias Member

  #5
  Jan 18, 2011
  Joined: Jul 11, 2009
  Messages: 20
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Tehe tehe.... kazi kweli kweli @drphone dunia hii co ile ya miaka ile watoto sasa wamegeuka kuwa wakubwa leo hii mtoto wa chini ya miaka 18 anauwezo kuliko hata mzee wa zaidi ya miaka 45 na ndio maana akakujibu yeye ni mswahili.
   
 6. boma2000

  boma2000 JF-Expert Member

  #6
  Jan 19, 2011
  Joined: Oct 18, 2009
  Messages: 3,283
  Likes Received: 155
  Trophy Points: 160
  alikuwa sahihi 110% kwa jibu la kabila
   
 7. N

  Nonda JF-Expert Member

  #7
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu,

  kwa kusoma thread nyingi hapa JF, mswahili ni mvaa "baragashia".
  kwa kihistoria, kiasili, mswahili ni mtu wa pwani ya Afrika mashariki, mtu wa mwambao na lugha yake ni kiswahili.Kiswahili huwa ndio lugha mama kwake, hana lugha nyengine. *Anaweza kusoma lugha nyengine shule au mitaani.
  Kwa tafsiri ya kileo, mswahili ndiyo kama huyo aliyekupa jibu lililokuchangamsha.

  kwa hiyo wapo waswahili wa asili na waswahili wa kujipa na waswahili wa kuja!
   
 8. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #8
  Jan 19, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,519
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Kivipi?
   
 9. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #9
  Jan 19, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,519
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Kwa jibu la yule mtoto, it means tafsiri unayoeleza imeshapitwa na wakati.
   
 10. afrodenzi

  afrodenzi Platinum Member

  #10
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 18,135
  Likes Received: 2,398
  Trophy Points: 280
  HAHAHAHHAHA LOL watoto bwana...

  You know wewe ni mswahili kama unafanya hizi vitu


  1. You talk too much.

  2. You sleep at the airport just to wait and catch a glimpse of Drogba with the Ivory coast team.

  3. To board a bus in the evening you climb through the window to get a seat even when the bus is just half full.


  4. You greet someone in more than 10 different ways before... getting to the point on what you wanted to say.
   
 11. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #11
  Jan 19, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,519
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  No thank u. I disagree with u. Do u mean,also those fisadis are also waswahili?
   
 12. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #12
  Jan 19, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  Ni Dr++
   
 13. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #13
  Jan 19, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,519
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Usitutoe kwenye ajenda kwa kuingiza utoto
   
 14. father

  father Member

  #14
  Jan 19, 2011
  Joined: Jan 17, 2011
  Messages: 30
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Baba wa Taifa alituasa tusiulizane makabila, wewe kwa nini ulitaka kujua kabila la mtoto?

  Anyway, nafikiri jibu sahihi linategemea na mazingira ambayo hilo swali linaulizwa. mfano ukiwa nje ya nchi kama zambia, mswahili atakuwa ni mtu anayeongea kiswahili kama lugha yake ya asili siyo ya kujifunza shule

  Ukiwa Tanzania mikoa ya nyanda za juu kusini au kanda ya ziwa, mswahili ataelezewa kuwa ni mtu wa pwani
  Ukiwa maeneo ya pwani kama DSM mswahili atatambuliwa kwa tabia zake nafikiri zinafahamika
   
 15. Saint Ivuga

  Saint Ivuga JF-Expert Member

  #15
  Jan 19, 2011
  Joined: Aug 21, 2008
  Messages: 39,449
  Likes Received: 19,820
  Trophy Points: 280
  ungemlipia nauli ningekungea thanks
   
 16. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #16
  Jan 19, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280


  Ungekua na jibu usingeweka hii thread hapa...Najua ukweli ni mchungu mara zote
   
 17. Horseshoe Arch

  Horseshoe Arch JF-Expert Member

  #17
  Jan 19, 2011
  Joined: Aug 10, 2009
  Messages: 11,230
  Likes Received: 4,951
  Trophy Points: 280
  local_26.jpg
   
 18. C

  ChiefmTz JF-Expert Member

  #18
  Jan 19, 2011
  Joined: Apr 15, 2008
  Messages: 2,519
  Likes Received: 292
  Trophy Points: 180
  Sijataka kuliweka wazi hilo kwa kuwa sio issu kwani hujui nilimpa zawadi gani.
   
 19. N

  Nonda JF-Expert Member

  #19
  Jan 19, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu,
  Nimekupa tafsiri, maana tatu, maelezo ya aina tatu ya nani mswahili..rudia kuisoma post yangu.
   
 20. Gaijin

  Gaijin JF-Expert Member

  #20
  Jan 19, 2011
  Joined: Aug 21, 2007
  Messages: 11,850
  Likes Received: 57
  Trophy Points: 0
  Tabia za Waswahili ni zipi..... Hebu tueleze
   
Loading...