Game Theory
JF-Expert Member
- Sep 5, 2006
- 8,546
- 843
Kama mtakumbuka kile kipindi cha MALENGA wetu huyu mzee alikuwa hana mfano kwa kutoa narratives za kiswahili
sina la kusema zaidi ya Inna Lillah wa Inna Illahi Rajuun.Duh ninayo CD yenye nyimbo za Egyptia hapa na huyu mzee alikuwa kipenzi wa Egyptia kama mimi....ama kweli waswahili sasa hivi tunadondoka kama majani vile
Hawa ndio wazee ambao tulitakiwa tuwa hudumie lakini wapi!
sina la kusema zaidi ya Inna Lillah wa Inna Illahi Rajuun.Duh ninayo CD yenye nyimbo za Egyptia hapa na huyu mzee alikuwa kipenzi wa Egyptia kama mimi....ama kweli waswahili sasa hivi tunadondoka kama majani vile
Hawa ndio wazee ambao tulitakiwa tuwa hudumie lakini wapi!
bingwa wa kiswahili hamisi akida hatunaye tena
MTAALAMU wa Kiswahili nchini, Hamis Akida amefariki dunia na kuzikwa Dar es Salaam jana. Mzee Akida alifia nyumbani kwake Mkwajuni katika Manispaa ya Kinondoni. Alikuwa na umri wa miaka 94.
Ofisa Uhusiano wa Baraza la Kiswahili Tanzania (BAKITA), Mohamed Mwinyi aliliambia HabariLeo kuwa Akida alikuwa kiungo kikubwa cha lugha hiyo.
Alisema kutokana na mchango wake katika lugha hiyo, mwaka 1999 Baraza liliamua kumtunuku Nishani ya Utetezi wa Kiswahili.
Miongoni mwa michango yake ni pamoja na kutunga Kamusi ndogo ya Kiingereza kwa kushirikiana na Profesa Abdallah Safari, kusahihisha lugha, kutafsiri miswada mbalimbali na uandishi wa makala mbalimbali.
Kwa mujibu wa wasifu wa Akida uliopatikana Bakwata, alizaliwa Novemba 22, 1914 mkoani Tanga. Miongoni mwa nafasi alizowahi kushikilia ni pamoja na ile ya Mchunguzi au Mtafiti Mwandamizi wa Taasisi ya Uchunguzi wa Kiswahili (TUKI).
Alianza masomo mwaka 1923 kwa kusoma Kiarabu na kisha alianza shule ya msingi mwaka 1925 hadi 1932 alipomaliza. Kati ya mwaka 1933 na 1934, alikuwa katika Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Tabora.
Alijiunga na Shirika la Posta na Mawasiliano ya Anga mkoani Tanga, mwaka 1935. Mwaka 1939 alihamishiwa Dar es Salaam ambako pamoja na mambo mengine aliyoyafanya, anakumbukwa kwa kuwa mchezaji mzuri wa mpira wa miguu na pia mwamuzi. Wasifu unaonyesha pia kuwa aliwahi kujiunga na Klabu ya Old Boys Sunderland (Simba) na baadaye alijiunga na klabu ya Yanga.
Alikuwa pia mpenzi wa muziki wa taarabu na aliwahi kuwa kiongozi wa The Egyptian Musical Club wakati wa harakati za kupigania Uhuru wa Tanganyika.