Mswada wa sheria ya kuunda Baraza la Usalama wa Taifa wakataliwa!


Sisimizi

Sisimizi

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2009
Messages
490
Likes
14
Points
35
Sisimizi

Sisimizi

JF-Expert Member
Joined Nov 10, 2009
490 14 35
Katika hali ya kufurahisha sana, muda mfupi uliopita Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limeridhia kwa kauli moja (100%) kuchomolewa kwa mswada wa usalama wa kuunda Baraza la Usalama wa Taifa uliowasilishwa na Mh Simba.

Hali Mh Simba akiwa amepigwa bumbuazi, ameurejesha muswada ukajadiliwe upya kweneye kamati.

Wakati akiwasilisha hoja yake, alimsifu Mwanasheria Mkuu wa serikali kwa namna alivyowezesha kukamilishwa kwa mswaada uliopigwa chini.

Ninahoji uwezo wa mwanasheria mkuu wa serikali. Naona hayupo makini kabisa.

Habari Leo

WABUNGE wameukataa muswada wa Baraza la Usalama wa Taifa wa mwaka 2009 kwa madai kuwa sheria ambayo ingetungwa ingemnyang'anya Rais wa Tanzania mamlaka ya kuamua mambo yanayohusu ulinzi na usalama wa nchi.

Wabunge hao wamedai kuwa, kama wangeukubali muswada huo, nchi isingekuwa na siri za masuala ya ulinzi na usalama kuwa watu wengi wangehusika kutoa uamuzi wa mambo hayo nyeti.

Wamesema, ulinzi ni amri, si suala la kupigiwa kura hivyo Rais wa Tanzania aachiwe mamlaka ya kuamua masuala ya ulinzi na usalama wa taifa.

Wabunge wamesema, baraza hilo si chombo cha mjadala na kupiga kura, ni cha kuamua.

Wametoa msimano huo bungeni wakati wanajadili Muswada wa Baraza la Usalama wa Taifa wa mwaka 2009 uliowasilishwa jana.

Msimamo huo wa wabunge ulimlazimisha Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Utawala Bora, Sophia Simba, aombe kuundoa na kuurudisha kwenye Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala, Bunge limekubali.

Kiongozi wa shughuli za upinzani bungeni, Hamad Rashid Mohamed, amesema, sheria ambayo ingetungwa kutokana na muswada huo ingeweza kusababisha Rais wa Tanzania apinduliwe.

Mohamed amesema, hakuna sehemu yoyote duniani inayopiga kura kuhusu masuala ya ulinzi hivyo muswada huo haufai.

"Suala la ulinzi ni time, ukichelewa dakika mbili umekosea" amesema Hamad wakati anazungumza na waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.

"Na ulinzi bwana ni amri...hakuna sehemu duniani ulinzi unapigiwa kura" amesema Hamad na kudai kuwa Baraza la Usalama wa Taifa lililopendekezwa kwenye muswada huo ni kubwa kuliko Baraza la Mawaziri.

Mbunge wa Ilemela, Anthony Diallo, amekataa kuunga mkono muswada huo huo kwa madai kuwa, Baraza la Usalama wa Taifa litakuwa kubwa sana, na utakuwa mzigo kwa walipa kodi na Serikali.

Diallo amelieleza Bunge kuwa, kitaalamu, watu saba hadi tisa tu ndiyo wanaoweza kutunza siri za Serikali, wakizidi utakuwa ni sawa na mkutano wa hadhara.

Amewaeleza waandishi wa habari nje ya ukumbi wa Bunge kuwa, muswada huo unahitaji kuboreshwa kwa kuwa unamnyang'anya Rais wa Tanzania madaraka yake.

Mbunge wa Bumbuli, William Shellukindo, amesema, Baraza la Usalama wa Taifa si kongamano au sehemu ya kujadiliana, ni mahali pa uamuzi.

Shellukindo amesema bungeni kuwa, Rais wa Tanzania ni Amiri Jeshi Mkuu, aachiwe madaraka yake ya kuamua kuhusu masuala ya ulinzi na usalama wa taifa.

Mbunge huyo amehoji, wakati Rais wa kwanza wa Tanzania , Julius Nyerere alipoamua taifa liingie vitani Kagera, kongamano gani lilikaa?

Mbunge wa Mtera, John Malecela amesema, muswada huo umewasilishwa bungeni wakati usio muafaka, ukarekebishwe, upelekwe bungeni wakati unaostahili.

Malecela ametaka Rais aachiwe madaraka ya kuamua kuhusu masuala ya ulinzi wa nchi na ameuliza, ni wapi Rais aliyechaguliwa anakuwa na kamati kubwa ya kumshauri kuhusu masuala ya vita.

Mbunge wa Kongwa, Job Ndugai amesema, muswada huo una kasoro, haukutazamwa vizuri hivyo urekebishwe.

Mbunge wa Karatu, Dk Wilbroad Slaa amesema, muundo wa Baraza la Usalama wa Taifa ni lazima uwe mzuri, hivyo wahusika waangalie nchi nyingine wanafanya nini.

Msemaji Mkuu wa kambi ya Upinzani katika Wizara ya Utawala Bora, Shoka Hamis Juma, ameupinga muswada huo kwa madai kuwa kuwa si sahihi kuwa na sheria tatu za usalama wa taifa.

Kambi hiyo imetaka iwepo sheria moja tu ya usalama wa taifa kwa kuwa zikiwa nyingi zitatoa mianya ya kufanyika makosa.
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,898
Likes
8,105
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,898 8,105 280
hiyo inasikitisha; wadau wenyewe wa usalama wa taifa hata kuulizwa hatujaulizwa licha ya kuwa ndio wakosoaji wa kwanza na wakubwa? Wangeuleta hapa uchambuliwe na mabingwa waliojazana hapa badala ya kuufanya ni siri yao..
 
nguvumali

nguvumali

JF Bronze Member
Joined
Sep 3, 2009
Messages
4,891
Likes
198
Points
160
nguvumali

nguvumali

JF Bronze Member
Joined Sep 3, 2009
4,891 198 160
Hunahaja ya kuhoji utendaji wake, maana ni dalili nyingine kuwa mfumo wetu wakuteuana unawalakini. UTEUZI WA MTU MAKINI UTAKUA UTEUZI WA WATU MAKINI....mUSWADA wenyewe unawasilishwa na waziri kama Simba, kweli kua uyaone.
 
Chimunguru

Chimunguru

JF-Expert Member
Joined
May 3, 2009
Messages
10,369
Likes
1,295
Points
280
Chimunguru

Chimunguru

JF-Expert Member
Joined May 3, 2009
10,369 1,295 280
Mkuu nimeona hiyo, naona wabunge wa ccm wanalala mbele kutoa maoni kwa tbc, dk kigoda kapata kigugumizi anajidai kashtukizwa
 
nguvumali

nguvumali

JF Bronze Member
Joined
Sep 3, 2009
Messages
4,891
Likes
198
Points
160
nguvumali

nguvumali

JF Bronze Member
Joined Sep 3, 2009
4,891 198 160
hiyo inasikitisha; wadau wenyewe wa usalama wa taifa hata kuulizwa hatujaulizwa licha ya kuwa ndio wakosoaji wa kwanza na wakubwa? Wangeuleta hapa uchambuliwe na mabingwa waliojazana hapa badala ya kuufanya ni siri yao..
Serikali inafanya siri yasiopaswa kuwa siri ....
 
nguvumali

nguvumali

JF Bronze Member
Joined
Sep 3, 2009
Messages
4,891
Likes
198
Points
160
nguvumali

nguvumali

JF Bronze Member
Joined Sep 3, 2009
4,891 198 160
Mkuu nimeona hiyo, naona wabunge wa ccm wanalala mbele kutoa maoni kwa tbc, dk kigoda kapata kigugumizi anajidai kashtukizwa
wamejaa unafiki, uzandiki, wanaogopa hata kutoa maoni yao , kweli nnchi hii inatatizo la kimfumo, bado watu wanaishi kama wapo karne ya kumi na saba. uelewa wao kuwa wapo bungeni kwa maslahi ya umma, wala si kwa maslahi ya chama wala serikali, kweli na ije ile sheria ya uhuru wa mgombea na binafsi labda itaongeza uwezo wetu wakujiamini.
 
Sisimizi

Sisimizi

JF-Expert Member
Joined
Nov 10, 2009
Messages
490
Likes
14
Points
35
Sisimizi

Sisimizi

JF-Expert Member
Joined Nov 10, 2009
490 14 35
hiyo inasikitisha; wadau wenyewe wa usalama wa taifa hata kuulizwa hatujaulizwa licha ya kuwa ndio wakosoaji wa kwanza na wakubwa? Wangeuleta hapa uchambuliwe na mabingwa waliojazana hapa badala ya kuufanya ni siri yao..
kweli Kamanda. Ninakuunga mkono 100%. Wangeuachia hapa JF tuudadavue.
 
ngoshwe

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Messages
4,119
Likes
66
Points
145
ngoshwe

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined Mar 31, 2009
4,119 66 145
Katika hali ya kufurahisha sana, muda mfupi uliopita Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, limeridhia kwa kauli moja (100%) kuchomolewa kwa mswada wa usalama wa taifa uliowasilishwa na Mh Simba.

Hali Mh Simba akiwa amepigwa bumbuazi, ameurejesha muswada ukajadiliwe upya kweneye kamati.

Wakati akiwasilisha hoja yake, alimsifu Mwanasheria Mkuu wa serikali kwa namna alivyowezesha kukamilishwa kwa mswaada uliopigwa chini.

Ninahoji uwezo wa mwanasheria mkuu wa serikali. Naona hayupo makini kabisa.
Shida ni nini mpaka umerejeshwa kwenye Kamati??, tatizo ni la AG au M/Kiti wa Kamati husika ya kisekta labda hakukuwa na extensive Public Hearing ambapo kimsingi ni kwenye ngazi ya Kamati??...
 
W

WildCard

JF-Expert Member
Joined
Apr 22, 2008
Messages
7,495
Likes
104
Points
160
W

WildCard

JF-Expert Member
Joined Apr 22, 2008
7,495 104 160
Taaluma ya SHERIA hapa nchini ina walakin. Mama Simba ni mwanasheria, AG wetu ndio usiseme, kamati ile ya Bunge ya Katiba na Sheria imesheheni wanasheria,....tatizo liko wapi kwa mswada nyeti kama huu wa Baraza la Usalama la Taifa? Mimi siwashangai. Walimshtaki Zombe na wenzake kumbe sio walioua!
 
nguvumali

nguvumali

JF Bronze Member
Joined
Sep 3, 2009
Messages
4,891
Likes
198
Points
160
nguvumali

nguvumali

JF Bronze Member
Joined Sep 3, 2009
4,891 198 160
Taaluma ya SHERIA hapa nchini ina walakin. Mama Simba ni mwanasheria, AG wetu ndio usiseme, kamati ile ya Bunge ya Katiba na Sheria imesheheni wanasheria,....tatizo liko wapi kwa mswada nyeti kama huu wa Baraza la Usalama la Taifa? Walimshtaki Zombe na wenzake kumbe sio walioua!
Sikwamba hawajui nini wanafanya, ila yapo maslahi ya kikundi kidogo cha watu ndani ya nnchi hii ndio kinaangaliwa ....wanasiasa hawajali maslahi ya kundi kubwa...wanasahau kama ipo siku nao watakuja kuwa raia wakawaida wataostahili kulindwa nasheia wanazozitunga leo.
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,898
Likes
8,105
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,898 8,105 280
Inabidi tuutafute huo mswada maana mambo ya kuuziwa nyoka kwenye kiroba hatutaki tena hasa tunakoelekea kwenye uchaguzi mkuu.
 
nguvumali

nguvumali

JF Bronze Member
Joined
Sep 3, 2009
Messages
4,891
Likes
198
Points
160
nguvumali

nguvumali

JF Bronze Member
Joined Sep 3, 2009
4,891 198 160
kuna kitu nimesahau kidogo...hivi waziri akiwasilisha muswada wa sheria fulani nakala sizinagawiwa kwa wabunge, ama ?
 
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined
Mar 10, 2006
Messages
31,898
Likes
8,105
Points
280
Mzee Mwanakijiji

Mzee Mwanakijiji

Platinum Member
Joined Mar 10, 2006
31,898 8,105 280
kusiwe na shaka tutaupata tu. Labda waagize nakala zote zichomwe moto na kompyuta iwe vaporized!
 
Buchanan

Buchanan

JF Diamond Member
Joined
May 19, 2009
Messages
13,211
Likes
385
Points
180
Buchanan

Buchanan

JF Diamond Member
Joined May 19, 2009
13,211 385 180
Jamani fanyeni juu chini mpate huo Muswada pamoja na ule wa fedha za uchaguzi ili tuijadili humu! Wanajifanya hawaitambui JF lakini mambo mengi wanachukuliaga humu! Hapa JF huwa hakiharibiki kitu!
 
ngoshwe

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined
Mar 31, 2009
Messages
4,119
Likes
66
Points
145
ngoshwe

ngoshwe

JF-Expert Member
Joined Mar 31, 2009
4,119 66 145
kuna kitu nimesahau kidogo...hivi waziri akiwasilisha muswada wa sheria fulani nakala sizinagawiwa kwa wabunge, ama ?
Kila taarifa inayowasilishwa Bungeni ikiwa ni pamoja na Miswaada ya sheria ambayo ina mijadala ya wazi nakala zinapaswa kugawiwa kwa wabunge kabla haijawasilishwa.

Vivyo hivyo sharti ni kuwa kabla ya mawasilisho ya Mswaada na Waziri husika kwenye Kamati ya kisekta ("public hearing"), wadau wanapaswa kupewa nakala ili waweze kushiriki kikamilifu kutoa maoni yao katika siku ya mawasilisho. Ofisi ya Katibu wa Bunge ilikuwa inaweka kwenye tovuti ya Bunge nakala za miswaada yote uliopangwa kuwasilishwa Bungeni na pengine kuchapisha kwny magazeti ya kawaida (local Newspapers) mswaada husika kama una maslahi makubwa ya umma kama ilivyokuwa wa PCCB.

Hata hivyo sasa inaonekana jambo hilo halifanyiki kabsa tokea wa mwisho uliowekwa Aprili, 2009 (Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Wakala wa Serikali). Mbaya zaidi, hata ofisi ya Mwanasheria Mkuu huwa haiweki miswaada kwenye tovuti yake ili wadau watoe maoni pale inapobidi kabla ya mswaada kupelekwa Bungeni!.
 
Sura-ya-Kwanza

Sura-ya-Kwanza

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2007
Messages
561
Likes
2
Points
35
Sura-ya-Kwanza

Sura-ya-Kwanza

JF-Expert Member
Joined Nov 17, 2007
561 2 35
Hakuna mahela ya kuchota hapo!
 
Ndahani

Ndahani

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2008
Messages
14,745
Likes
2,035
Points
280
Ndahani

Ndahani

JF-Expert Member
Joined Jun 3, 2008
14,745 2,035 280
Muswada unapelekwa na Sophia Simba huyu huyu mutoto wa mujini anayefahamika? Lazima uwe rejected! Ni magumashi matupu hayo.
 
Bernard Rwebangira

Bernard Rwebangira

R I P
Joined
Feb 15, 2009
Messages
99
Likes
0
Points
0
Bernard Rwebangira

Bernard Rwebangira

R I P
Joined Feb 15, 2009
99 0 0
Muswada ulikuwa na mapungufu kibao mpaka ya nukta, coma, dash ata ya erufi kubwa na ndogo.

Hii ni aibu sana yaani vitu ka hivyo bado watu hawakuuona? palikuwa na haraka gani kuleta kitu chenye mapungufu kibao?
 
O

Omumura

JF-Expert Member
Joined
Aug 20, 2009
Messages
476
Likes
3
Points
35
O

Omumura

JF-Expert Member
Joined Aug 20, 2009
476 3 35
Hayo ndo mambo ya sophia simba, muswaada anausoma baada ya kutoka kitchen party unategemea nini sasa!!!mwaka huu mambo yapo.
 
nguvumali

nguvumali

JF Bronze Member
Joined
Sep 3, 2009
Messages
4,891
Likes
198
Points
160
nguvumali

nguvumali

JF Bronze Member
Joined Sep 3, 2009
4,891 198 160
Muswada ulikuwa na mapungufu kibao mpaka ya nukta, coma, dash ata ya erufi kubwa na ndogo.

Hii ni aibu sana yaani vitu ka hivyo bado watu hawakuuona? palikuwa na haraka gani kuleta kitu chenye mapungufu kibao?
iNGAWA sijausoma mswada huo lakini nahisi haraka yote ni kukimbilia kwenye uchaguzi mkuu, nahisi kuna majitu ya ajabu katika kuminya uhuru wetu wakushiriki kuwaondoa ccm madarakani, najua .
 

Forum statistics

Threads 1,250,456
Members 481,359
Posts 29,734,236