Mswada wa kuuza viungo vya mwili kujadiliwa Bungeni

Humphrey Msoka

JF-Expert Member
Feb 4, 2017
420
322
taasisi ya moyo ya Jakaya Kikwete inajiandaa kupeleka mswada Katika Bunge lijalo kuhusu uuzwaji wa viungo vya binadamu Kama moyo na figo na pia watu kuandika wosia pindi watakapo kufa viungo vyao vitumikaje

maoni yenu kuhusu ili wakuu

je upo Tayari kuuza au kuandika wosia wa viungo vitumike

=========

Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete (JKCI) inaandaa mapendekezo ili kuyapeleka bungeni yaridhiwe na kupitishwa sheria itakayoruhusu mtu kuandika wosia wa viungo vyake kutumika baada ya kufariki dunia.

Sanjari na hilo, kwa sasa inatararajia kuanza upasuaji wa kupandikiza moyo kwa wagonjwa wenye matatizo hayo nchini. Mkurugenzi wa Upasuaji na Daktari Bingwa wa Moyo na Mishipa ya Damu, Dk Bashir Nyangasa ameyasema hayo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizungumza na vyombo vya habari kuhusu malengo ya taasisi hiyo.

“Tuko katika maandalizi ya kuandaa mapendekezo kwa ajili ya kupeleka Bungeni ili Bunge liridhie na kupitisha sheria itakayoruhusu mtu kuandika wosia wa viungo vyake kutumika mara baada ya kufariki ikiwamo moyo na figo,” alisema Dk Nyangasa.

Amesema kuwa umefika wakati kwa Watanzania kujiwekea utaratibu wa kuacha wosia wa kutumika kwa viungo vyao baada ya kufariki kwa ajili ya kuhifadhiwa kwenye benki za viungo ili viweze kutumiwa na watu ambao watavihitaji.

Dk Nyangasa amesema Hospitali ya Apolo Bangalole ya India na nyingine za kimataifa za magonjwa ya moyo kwa sasa zimehamia JKCI kutokana na kuwapo kwa huduma pamoja na vifaa vya kisasa.

Naibu Mkurugenzi wa Huduma za Tiba na Daktari Bingwa wa Magonjwa wa Moyo, Dk Tulizo Shemu amesema mwaka 2016 JKCI ilifanya uchunguzi wa tiba kwa wagonjwa 973 na kati yao 620 walipata matibabu bila kufunua vifua kwa kupitia mishipa ya damu, huku 353 wakifanyiwa upasuaji wa kufungua vifua.

Taasisi hiyo inategemea kuwa na kambi maalumu ya matibabu ya moyo kwa kushirikiana na Open Heart International ya Australia kuanzia kesho.
 
Watanzania walio wengi hatujawa tayari kwa hili...! Ndiyo kilichonijia kichwani..mara baada ya kusoma post ya kwanza ya uzi huu.
 
Tutaviuza viungo vya wapendwa wetu sasa kiwekwe kipengere cha kujitolea bure kiungo ili kuziba mianya ya wapiga deal! :D:D
 
Hii haifai aisee Tanzania hii ya deal kila kona unaweza ukaumwa zako wakakudedisha ili wachukue hayo makitu wawape wenye fweza zao.Akuuu.
 
Back
Top Bottom