Mswada mpya wa Sheria kuwakinga hata wapinzani watakaposhika hatamu

Sioni shida sana, maana muda ukifika maadiko yataandikwa upya kukidhi uhitaji wa wananchi.
Cha maana tuombe afya na uhai tuyashuhudie niliyoandika hapo juu.
Kumbuka kila zama na kitabu chake by Alhaj Ali Hassan Mwinyi.
 
Mi najua wakiingia wapinzai wataviondoa hivyo vifungu, na wataweka wazi mtu yeyote atakuwa na haki ya kumshitaki raisi hata kama atakuwa madarakani, na mahakama ndio itakayo hukumu kama hajakosea,
Kwa uwazi najua hili litafanyika tu
Kwa sababu ndicho wanachopigania.

Uko sahihi, na hali hiyo ili ifikiwe hamna budi machafuko kutokea, maana kwa njia ya box la kura sioni hilo likitokea.
 
Apo ndyo mtajua kuwa beberu ni CCM.

Baada ya uchaguzi 2020. Bunge litakuwa halina upinzani kabisa nawahakikishieni. Uchaguzi utavurugwa ilimradi wapinzani ( CHDMA) wasiingie bungeni.

Baada ya hapo mswaada wa Rais magufuli kutawala mpaka atakapotaka kutoka yeye utafata. Utatinga bungeni na utapata support 100% kutoka kwa wabunge wa mabeberu.

Hii kuhakikisha wapinzani hawarudi bungeni ni ili hilo litimie. Na hata wanaccm watakaopitishwa, ni wale watakaounga mkono Magufuli kukaa madarakani zaidi ya miaka 10.
 
Uko sahihi, na hali hiyo ili ifikiwe hamna budi machafuko kutokea, maana kwa njia ya box la kura sioni hilo likitokea.

Kwenye machafuko hapo labda uwe umezeeka umekufa ila kwa vizazi vijavyo,
Na kama mmejipanga kwa hii 2020 na huyo Lisu mtachapwa sana.
 
Sioni shida sana, maana muda ukifika maadiko yataandikwa upya kukidhi uhitaji wa wananchi.
Cha maana tuombe afya na uhai tuyashuhudie niliyoandika hapo juu.
Kumbuka kila zama na kitabu chake by Alhaj Ali Hassan Mwinyi.
Na mshindi wa wakati huo ndio ataamua jinsi gani ya kudili na hawa wahuni wa kipindi hiki.
 
Mswada wa sheria unaopelekwa bungeni kumkinga Rais, Jaji Mkuu, Spika na Naibu dhidi ya kushtakiwa wakiwa madarakani, unaweza kuwa na manufaa hata kwa wapinzani endapo watashinda uchaguzi na kuunda serikali.

Kwa upande wangu binafsi sina shida sana na hilo ila nina maswali kama matatu hivi.

1. Ni kwanini ni rahisi sana kupeleka miswada ya kuwakinga watu na sio wa kudai tume huru ya uchaguzi?
2. Hawaoni kufanya hivo kutawapa watawala wetu kiburi cha kuendelea kuvunja katiba ya nchi na kutumia madaraka yao vibaya?
3. Je, Bunge la jmt linaweza kutunga na kupitisha sheria inayokinzana na katiba ya nchi?

Naomba kuwasilisha!
Ndugu, kwa Tz. ya sasa kila kitu chenye mwelekeo wa kulinda maslahi ya watawala ni halali. Hii haiwalindi wapinzani kwa sababu ndoto ya kushika madaraka kwao ndani ya mazingira ya sasa haitatimia. Katiba ya nchi haiheshimiki tena hadi mahakamani!
 
jiwe anajiandaa ili awe tayari kuua watakaopinga matokeo hapo october hasa wapinzani wake kisiasa!!!!Tujiandae kwa kupotea na kuuawa wengi kuelekea uchaguzi mkuu!!!
 
Bunge la awamu ya tano ndiyo limeongoza kutunga sheria mbovu kuliko bunge lolote lile katika taifa hili.

Ni bunge ambalo kwa matendo yake limewasaliti wananchi ambao ndiyo lilipaswa kuwa sauti yao badala yake limekuwa bunge la serikali.

Limefanya kazi ya kuipongeza serikali na kuamua kwa wazi wazi kujifutia hata uhuru mdogo lililonao wakati huo huo likishiriki kubariki serikali kupambana na raia walioiweka madarakani wenyewe.

Kama watanzania wangekuwa serious ilipaswa kwenda kuufunga ule ukumbi wa bunge na kuwafukuza hao wabunge wa serikali ili tupate fursa ya kuchagua wawakilishi halisi wa wananchi.
Dawa ni kudai tume huru ya uchaguzi na kanuni zilizosawa kwa wote. La sivyo hakuna litakalobadilika!
 
Dawa ni kudai tume huru ya uchaguzi na kanuni zilizosawa kwa wote. La sivyo hakuna litakalobadilika!
Dawa ni katiba mpya kwanza mengine ni mambo madogo.

Lakini kabla ya hapo lazima wananchi tutambue pia juhudi za kutafuta katiba mpya haupaswi kuwa kazi ya vyama vya siasa pekee.
 
Kwenye machafuko hapo labda uwe umezeeka umekufa ila kwa vizazi vijavyo,
Na kama mmejipanga kwa hii 2020 na huyo Lisu mtachapwa sana.

Hilo lakuchwapa sana wala halina mjadala maana hatuna silaha. Ila hilo hilo ndio litaloweka kila kitu sawa. Usidhani dunia imelala mpaka mfanye mtakacho. Na hilo la kutupiga ndio hasa tunalolitaka, maana litafungua ukurasa mpya na huenda ukawa mwisho wenu. Huenda mkatamba kwa muda fulani lakini mtaishia jela wote. Ukiona mnaowasujudia wanapeleka mswaada wa kutoshitakiwa, basi ujue wamenusa ajali itakayotokea mbeleni.
 
Hilo lakuchwapa sana wala halina mjadala maana hatuna silaha. Ila hilo hilo ndio litaloweka kila kitu sawa. Usidhani dunia imelala mpaka mfanye mtakacho. Na hilo la kutupiga ndio hasa tunalolitaka, maana litafungua ukurasa mpya na huenda ukawa mwisho wenu. Huenda mkatamba kwa muda fulani lakini mtaishia jela wote. Ukiona mnaowasujudia wanapeleka mswaada wa kutoshitakiwa, basi ujue wamenusa ajali itakayotokea mbeleni.

Unataka ujiringanishe na marekani? 😁😁😁😁😁😁 kama mlikuwa na nguvu 2015 hamkufanya kitu itakuwa sasa hivi? Sanduku la kura tu linawatupa nje, hao unaowaaminia mbona wamefukuzwa burundi juzi tu.
 
Yaani wanatunga sheria ya;

1. Kumlinda Rais asishitakiwe akiwa na akitoka madarakani?.....Katiba inasemaje kwani?

2. Kumlinda Jaji Mkuu asishitakiwe akiwa ama akitoka madarakani? How? Katiba inasemaje?

3. Kumlinda Spika na naibu Spika wasishitakiwe wakiwa ama wakitoka madarakani? How? Katiba inasemaje kuwahusu?

å Na kwa ujumla wake tusemeje hasa? Je, si kwamba jambo hili si la KISHERIA bali ni la KIKATIBA?

å I thought wangepeleka mswaada wa marekebisho ya Katiba kwa sababu as far as I know hawa watu wote wako kwa mujibu wa katiba....

å Na katiba iko very clear kuanzia upatikanaji wao, majukumu yao na ulinzi wao kikatiba wakiwa madarakani na hata wakitoka...

å Na kwanini viongozi wa serikali kwa sasa wanaamua kujitungia sheria za kujilinda na kwa upande wa pili wakitunga sheria za kukandamiza uhuru wa RAIA katika mambo mbalimbali?

å Wamenusa nini huko mbeleni hawa watu? Au wanataka kufanya nini huko mbeleni kiasi ambacho wameona kabla ya kufanya hayo/hicho wajilinde kwa sheria kwanza??

å Na je, wana uhakika gani kuwa wakifanya uhuni au unyama sheria hizi zitaweza kuwalinda milele?

å Kama wakija wengine na wakitaka kuwashughulikia hakika tunawahakikishia kuwa watashughulikiwa tu....!!

å Ni rahisi tu, kwa sababu kwa kutumia njia hii hii wanayotumia wao kutunga sheria hizi za kujilinda, akija anayetaka kuwashughulikia anaweza kufuta hizi sheria na akatunga zingine ili ziruhusu watakaokuwa wameshika mpini wawashughulikie....

å Ulinzi kamili na wa uhakika katika maisha ya binadamu ki KUWA WAKWELI ndani ya nafsi zetu, KUWA NA KIASI, KUVUMILIANA na kama watu ama viongozi wenye dhamana na mamlaka ya maamuzi kuishi maisha ya KUTENDA HAKI!!....

å Haya wafanyayo hayatawasidia sasa wala kesho na hata milele kwa sababu adhabu ya dhambi yoyote ni lazima ihukumiwe tu....!!
 
Unataka ujiringanishe na marekani? 😁😁😁😁😁😁 kama mlikuwa na nguvu 2015 hamkufanya kitu itakuwa sasa hivi? Sanduku la kura tu linawatupa nje, hao unaowaaminia mbona wamefukuzwa burundi juzi tu.

Kwa taarifa yako Burundi heshima ilipatikana wakati Nkurunziza alipoanza kutaka kukaa madarakani muda wa ziada. Huoni kakubali yaishe? Na sasa hivi hapo Burundi wanaheshimiana maana ukurasa mpya umefunguliwa.
 
Watakuwa wamesahau vipengele vya kuwalinda viongozi wa tume ya uchaguzi, na IGP kweli? Au wameamua kuanza na hiyo!
 
Mtazamo wangu: Hii naiona kama kuendeleza zoezi la kujaza upepo kwenye puto. Ikifika elastic limit litapasuka tutake tusitake. Sayansi ndivyo inavyosema, so Mimi. Ya Floyd wa marekani nayo ni wingi wa upepo ktk vifua vya watu, si vinginevyo!
 
Why is magufuli doing all these?
His doing all these to save the country from "THEM". Those who are ready to sell our freedom/humanity to the mabeberu. People like Lissu who thinks people who speak English better should rule us by all means!
 
Eti wanatunga sheria kuwa badala ya kumshitaki spika, naibu spika au Jaji mkuu, mtu ukamshitaki mwanasheria mkuu wa serikali.
Sasa mwanasheria mkuu si ni wa mhimili wa serikali, yeye anahusika na nini kwenye mhimili wa Mahakama na Bunge?

Hii kitu inazidi kukoroga mihimili, na kuifanya mihimili mingine iwakilishwe na mhimili wa serikali, Huu muswada ni ujinga wa hali ya juu!

Kama ni Mwigulu amehusika kudraft muswada huu, basi hii ni kazi yake ya mwanzoni mwanzoni ambayo ni ya hovyo kupita kiasi!
 
Duh
Mpaka kizazi hiki cha mambumbu kiishe ndipo akili zitashika hatamu
 
Back
Top Bottom