Mswada mpya wa Sheria kuwakinga hata wapinzani watakaposhika hatamu

Duplicate_90

JF-Expert Member
Mar 29, 2020
272
308
Mswada wa sheria unaopelekwa bungeni kumkinga Rais, Jaji Mkuu, Spika na Naibu dhidi ya kushtakiwa wakiwa madarakani, unaweza kuwa na manufaa hata kwa wapinzani endapo watashinda uchaguzi na kuunda serikali.

Kwa upande wangu binafsi sina shida sana na hilo ila nina maswali kama matatu hivi.

1. Ni kwanini ni rahisi sana kupeleka miswada ya kuwakinga watu na sio wa kudai tume huru ya uchaguzi?
2. Hawaoni kufanya hivo kutawapa watawala wetu kiburi cha kuendelea kuvunja katiba ya nchi na kutumia madaraka yao vibaya?
3. Je, Bunge la jmt linaweza kutunga na kupitisha sheria inayokinzana na katiba ya nchi?

Naomba kuwasilisha!
 
Hakuna kitu kibaya kama unapokuwa na nchi ambayo sheria zake zinatungwa ili kuendana na tabia au mapungufu binafsi ya viongozi walioko madarakani. Huu mchezo wa kila mtazamo wa kiongozi aliye madarakani wakati huo, kutunga sheria zinazoendana na tabia zake binafsi tutakuwa tutengeneza nchi ya ajabu sana. Mchezo huu naona ni kama kupima upepo kabla ya kuchezea katiba, ili kumuongezea rais aliye madarakani muda wa kukaa madarakani zaidi ya miaka 10.
 
Apo ndyo mtajua kuwa beberu ni CCM.

Baada ya uchaguzi 2020. Bunge litakuwa halina upinzani kabisa nawahakikishieni. Uchaguzi utavurugwa ilimradi wapinzani ( CHDMA) wasiingie bungeni.

Baada ya hapo mswaada wa Rais magufuli kutawala mpaka atakapotaka kutoka yeye utafata. Utatinga bungeni na utapata support 100% kutoka kwa wabunge wa mabeberu.
 
Mswada wa sheria unaopelekwa bungeni kumkinga Rais, Jaji Mkuu, Spika na Naibu dhidi ya kushtakiwa wakiwa madarakani, unaweza kuwa na manufaa hata kwa wapinzani endapo watashinda uchaguzi na kuunda serikali.

Kwa upande wangu binafsi sina shida sana na hilo ila nina maswali kama matatu hivi.

1. Ni kwanini ni rahisi sana kupeleka miswada ya kuwakinga watu na sio wa kudai tume huru ya uchaguzi?
2. Hawaoni kufanya hivo kutawapa watawala wetu kiburi cha kuendelea kuvunja katiba ya nchi na kutumia madaraka yao vibaya?
3. Je, Bunge la jmt linaweza kutunga na kupitisha sheria inayokinzana na katiba ya nchi?

Naomba kuwasilisha!
Kuna uovu wanajiandaa kuutenda muda shahidi wenye kusifia watashtuka wanalia
 
Hakuna kitu kibaya kama unapokuwa na nchi ambayo sheria zake zinatungwa ili kuendana na tabia au mapungufu binafsi ya viongozi walioko madarakani. Huu mchezo wa kila mtazamo wa kiongozi aliye madarakani wakati huo, kutunga sheria zinazoendana na tabia zake binafsi tutakuwa tutengeneza nchi ya ajabu sana. Mchezo huu naona ni kama kupima upepo kabla ya kuchezea katiba, ili kumuongezea rais aliye madarakani muda wa kukaa madarakani zaidi ya miaka 10.
Bunge la awamu ya tano ndiyo limeongoza kutunga sheria mbovu kuliko bunge lolote lile katika taifa hili.

Ni bunge ambalo kwa matendo yake limewasaliti wananchi ambao ndiyo lilipaswa kuwa sauti yao badala yake limekuwa bunge la serikali.

Limefanya kazi ya kuipongeza serikali na kuamua kwa wazi wazi kujifutia hata uhuru mdogo lililonao wakati huo huo likishiriki kubariki serikali kupambana na raia walioiweka madarakani wenyewe.

Kama watanzania wangekuwa serious ilipaswa kwenda kuufunga ule ukumbi wa bunge na kuwafukuza hao wabunge wa serikali ili tupate fursa ya kuchagua wawakilishi halisi wa wananchi.
 
Why is magufuli doing all these?

Cha kushangaza hataki katiba ya wananchi, lakini anabadilisha vifungu vya sheria kwenye katiba ili vimlinde yeye mwenyewe, na kundi lake analolitumia kupindisha sheria za nchi. Kibaya kabisa anasema tena bila hofu kwamba hakuahidi katiba! Huu ni ushahidi tosha kuwa anafanya ukatili, na sasa ana mashaka akitoka madarakani atakutana na mkono wa sheria. Kama mtu anafanya mambo mazuri, hizo kinga anatafuta za nini?
 
Mswada wa sheria unaopelekwa bungeni kumkinga Rais, Jaji Mkuu, Spika na Naibu dhidi ya kushtakiwa wakiwa madarakani, unaweza kuwa na manufaa hata kwa wapinzani endapo watashinda uchaguzi na kuunda serikali.

Kwa upande wangu binafsi sina shida sana na hilo ila nina maswali kama matatu hivi.

1. Ni kwanini ni rahisi sana kupeleka miswada ya kuwakinga watu na sio wa kudai tume huru ya uchaguzi?
2. Hawaoni kufanya hivo kutawapa watawala wetu kiburi cha kuendelea kuvunja katiba ya nchi na kutumia madaraka yao vibaya?
3. Je, Bunge la jmt linaweza kutunga na kupitisha sheria inayokinzana na katiba ya nchi?

Naomba kuwasilisha!

Mi najua wakiingia wapinzai wataviondoa hivyo vifungu, na wataweka wazi mtu yeyote atakuwa na haki ya kumshitaki raisi hata kama atakuwa madarakani, na mahakama ndio itakayo hukumu kama hajakosea,
Kwa uwazi najua hili litafanyika tu
Kwa sababu ndicho wanachopigania.
 
Mswada wa sheria unaopelekwa bungeni kumkinga Rais, Jaji Mkuu, Spika na Naibu dhidi ya kushtakiwa wakiwa madarakani, unaweza kuwa na manufaa hata kwa wapinzani endapo watashinda uchaguzi na kuunda serikali.

Kwa upande wangu binafsi sina shida sana na hilo ila nina maswali kama matatu hivi.

1. Ni kwanini ni rahisi sana kupeleka miswada ya kuwakinga watu na sio wa kudai tume huru ya uchaguzi?
2. Hawaoni kufanya hivo kutawapa watawala wetu kiburi cha kuendelea kuvunja katiba ya nchi na kutumia madaraka yao vibaya?
3. Je, Bunge la jmt linaweza kutunga na kupitisha sheria inayokinzana na katiba ya nchi?

Naomba kuwasilisha!
Hiyo Sheria haifai kabisa iwe kwa yeyote atakae ingia madarakani
 
Back
Top Bottom