Hatua za mijadala ya Muswada katika Bunge

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,467
113,567
Miswada hupitia hatua zifuatazo
82.-(1) Muswada wa Sheria wa Serikali utawasilishwa Bungeni na Waziri au Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

(2) Muswada Binafsi wa Sheria unaweza kuwasilishwa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati yoyote ya Kudumu ya Bunge au Mbunge yeyote ambaye si Waziri.

83.-(1) Muswada wowote wa Sheria ambao umetangazwa kwenye Gazeti, unaweza kuwasilishwa Bungeni kufuatana na Orodha ya Shughuli ili Kusomwa Mara ya Kwanza na katika hatua hiyo Katibu atasoma jina refu la Muswada wa Sheria unaohusika bila hoja yoyote kutolewa kwa ajili hiyo.
Utaratibu kuhusu Miswada Binafsi
Uwasilishaji wa Muswada

(2) Hakutakuwa na mjadala wowote wakati wa Muswada wa Sheria Kusomwa Mara ya Kwanza.
84.-(1) Spika atapeleka Muswada wa Sheria kwenye Kamati inayohusika na Kamati itaanza kuujadili Muswada huo mapema iwezekanavyo.

(2) Kamati iliyopelekewa Muswada itatoa matangazo au itatoa barua ya mwaliko kumwalika mtu yeyote afike kutoa maoni yake mbele ya Kamati hiyo kwa lengo la kuisaidia katika uchambuzi wa Muswada huo.

(3) Bila ya kuathiri masharti ya Ibara ya 99 ya Katiba, Kamati iliyopelekewa Muswada itakuwa na uwezo wa kufanya marekebisho katika Muswada wa Sheria kwa kumshauri Waziri au Mbunge anayehusika na Muswada huo kufanya mabadiliko, vilevile Serikali itakuwa na uwezo wa kuishauri Kamati ya Kudumu ya Bunge kuhusu kufanya marekebisho au mabadiliko juu ya Muswada Binafsi.

(4) Kabla Muswada wa Sheria uliofanyiwa mabadiliko haujawasilishwa Bungeni kwa ajili ya Kusomwa Mara ya Pili, utapelekwa kwenye Kamati inayohusika kwa madhumuni ya kuzingatia mabadiliko hayo.

85.-(1) Kamati iliyopelekewa Muswada wa Sheria itakapokamilisha kuujadili Muswada huo Mwenyekiti wa Kamati atamjulisha Spika kwa maandishi kwamba, Kamati imemaliza kujadili Muswada husika.

(2) Spika ataagiza Muswada huo uwekwe kwenye Orodha ya Shughuli kwa ajili ya kusomwa Mara ya Pili.

86.-(1) Siku ambayo Muswada wa Sheria uliokwisha kujadiliwa na Kamati umepangwa kwenye Orodha ya Shughuli, Waziri, Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mwenyekiti wa Kamati au Mbunge mwenye Muswada husika atawasilisha hoja kwamba Muswada wa Sheria ambao atautaja kwa jina Kusomwa Mara ya Pili.

(2) Hoja ya Muswada wa Sheria Kusomwa Mara ya Pili itakuwa kama ifuatavyo:“Kwamba, Muswada wa Sheria uitwao….. sasa usomwe mara ya pili.” Au kadri itakavyokuwa; “Kwamba, Muswada uitwao ……………… kama
Muswada kupelekwa kwenye Kamati
Taarifa ya Kamati
Muswada Kusomwa Mara ya Pili

87.-(1) Endapo Muswada ulikwishasomwa mara ya Pili na haukuwa na mabadiliko,

(10) Kamati ya Bunge Zima itajadili na kupitisha au kufanya mabadiliko na kupitisha Muswada wa Sheria Ibara moja baada ya Ibara nyingine, isipokuwa kwamba, Mwenyekiti, akiona inafaa, anaweza kuihoji Kamati itoe uamuzi wake kwa sehemu moja yenye Ibara kadhaa au Ibara zote zilizomo katika sehemu moja ya Muswada.
89.-(1) Baada ya Kamati ya Bunge Zima kukamilisha kazi ya kupitia Muswada wa Sheria, Bunge litarejea na Mtoa hoja atatoa taarifa Bungeni kwa maneno yafuatayo:

“Kamati ya Bunge Zima imeupitia Muswada wa Sheria, Ibara kwa Ibara na kuukubali bila mabadiliko, naomba kutoa hoja.” au kama kuna mabadiliko yaliyofanywa kwa maneno yafuatayo: “Kamati ya Bunge Zima imeupitia Muswada wa Sheria, Ibara kwa Ibara na imeukubali pamoja na marekebisho yaliyofanyika, naomba kutoa hoja” na kisha atatoa hoja:
“Kwamba, Muswada wa Sheria wa …………sasa ukubaliwe”. au kama kuna mabadiliko yaliyofanywa katika Muswada kwa maneno yafuatayo:
Taarifa baada ya Muswada Kusomwa Mara ya Pili
“Kwamba, Muswada wa Sheria wa …. Kama ulivyorekebishwa au kubadilishwa katika Kamati ya Bunge zima, sasa ukubaliwe.”

(2) Hoja ya kupitisha Muswada wa Sheria wa mabadiliko ya Katiba itaamuliwa kwa mujibu wa Ibara ya 98 ya Katiba. Kwa sababu hiyo, kura zitapigwa kwa kuita jina la Mbunge mmoja mmoja katika hatua ya Muswada huo Kusomwa Mara ya Pili.

90.- Mtoa hoja anayewasilisha Muswada wa Sheria anaweza kuuondoa Muswada wakati wowote kabla ya Bunge kuhojiwa kutoa uamuzi wake, baada ya kutoa taarifa kwa Spika.
91.- Baada ya Muswada wa Sheria Kusomwa Mara ya Tatu, utahesabika kuwa umepitishwa na Bunge.

P.
 
Nimependa ufahamu sahihi wa hili jambo. Japo ni nadra mswaada kutoka serikalini ukapata marekebisho yoyote ya maana huko bungeni kutokana na ushabiki wa kisiasa uliotamalaki.
 
Back
Top Bottom