Msururu wa viongozi wa merekani kuja tanzania..........!!

sinafungu

JF-Expert Member
Feb 13, 2010
1,524
863
heri hao wazungu watupuuze huenda tutakuwa salama.(HAYATI MWL J K NYERERE)
huyu mzee alikuwa anaona mbali sana. sasa ndo napata tafsiri ya maneno yake. kulikoni ndg zangu safari haziwaishi hao mabeberu wanyonyaji kukimbili NCHINI mwetu....? BUSHI alituletea vyandarua sasa OBAMA ndo analeta shuka.........? jamani mwenye kufahamu faida mbali na hasara ya kuja hao watu atuondoe wasiwasi (wengine hadi leo kigamboni tupotupo tu)
 
Nafikiri humuoni rais wako anovyokwenda kwa watu ndio?
Hivyo na kwakwe watakuja tu
 
Bado ipo siku tutaambiwa tuhamie somalia kwa kuwa nchi hii si yetu tena
 
Tanzania imekuwa kama mgodi usiokuwa na mwenyewe mawazo ya viongozi wetu wameyapeleka kwa rangi nyeupe na kusahau kuwainua wazawa eti uwekezaji hawajiulizi hapo uingereza na mataifa mengi yaliyoedelea ni nani mgeni alienda kuwekeza huko kama sio nchi yenyewe kujiwekeza kupitia wananchi wake wenyewe takwimu zinaonesha asilimia 90 ya uchumi wa nchi hii unamilikiwa na watu kutoka nje na wala sio wazawa, ukiona mzawa aliefanikiwa ni mchuuzi wa bidhaa za nchi nyingine na si mzalishaji wengi waliobaki ni waangalizi tu wa investments za watu kutoka nje ambazo zinaendeshwa kwa rasilimali zao yani mgeni anakuwa smart kuliko mzawa yani ukiangalia nchi hii inavyoendeshwa ni kama bado tupo kwenye critical colonialism still hapa ndipo nnapo msalute Mugabe!!
 
heri hao wazungu watupuuze huenda tutakuwa salama.(HAYATI MWL J K NYERERE)
huyu mzee alikuwa anaona mbali sana. sasa ndo napata tafsiri ya maneno yake. kulikoni ndg zangu safari haziwaishi hao mabeberu wanyonyaji kukimbili NCHINI mwetu....? BUSHI alituletea vyandarua sasa OBAMA ndo analeta shuka.........? jamani mwenye kufahamu faida mbali na hasara ya kuja hao watu atuondoe wasiwasi (wengine hadi leo kigamboni tupotupo tu)

Nyerere alikuwa anawakimbilia wao. Kikwete anawafanya watukimbilie sisi.

Nakumbuka baada ya kukumbwa na uhaba wa chakula wakati wa Nyerere walituletea unga wa mahindi wa manjano (Yanga) kwi kwi kwi teh teh teh! Na kabla ya hapo alipokwenda kuonana na Kenedy tukaletewa maziwa ya uji mashuleni.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom