KWELI Msumbiji: Magaidi wamevamia Msafara wa Wanajeshi wa Tanzania na Lesotho

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Zipo taarifa zinadai kuwa Jeshi la Tanzania katika wilaya ya Nangade, Cabo Delgado waliingia kwenye mtego wa Magaidi katika kijiji cha Vondanhar, eneo la Palma. Aidha inadaiwa Jeshi la Tanzania lilikuwa likisafiri kwa magari ya kivita sambamba na jeshi la Msumbiji. Magari matatu ya jeshi la Tanzania yamechomwa moto na baadhi ya Silaha kuharibiwa.

Taarifa iliyotolewa na kikundi cha Kigaidi cha IS, imedai wamekamata baadhi ya Silaha ikiwemo Chinese Type 81-1 assault rifle pamoja na 12.7x108mm Type 54 HMG ya kwenye gari.

Zaidi inaelezwa kuwa haya ni magari ya JWTZ yapo chini ya himaya ya magaidi.

1669096815282.png

1669096826864.png
 
Tunachokijua
Msumbiji ilianza kupokea mashambulio ya kigaidi tangu Oktoba 17, 2017. Baadhi ya vyanzo vinaonesha Mashambulizi hayo yalikuwa na nia ya kupinga utamaduni wa magharibi, hata hivyo baadhi yameonesha nyuma ya mashambulizi hayo kuna suala la kiuchumi kwa kuwa mashambulizi yalianza miaka kadhaa baada ya kugundulika kwa gesi na rubi katika Jimbo la Cabo Delgado.

Jimbo la Cabo Delgabo ni jimbo la kaskazini mwa Msumbiji ambalo linapakana na mkoa wa Mtwara ulio kusini mwa Tanzania. Kwa sababu hiyo usalama wa Cabo Delgado ulionesha kuwa ni usalama wa Tanzania. Novemba 15, 2021, Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan alitoa sababu ya kutoa majeshi ya Tanzania kwenda kusaidia kulinda amani nchini Msumbiji.

Majeshi ya Tanzania yaliingia nchini Msumbiji kwa makubaliano ya Mpango wa Jumuiya ya Nchi za kusini mwa Afrika (SADC) ambapo jumla ya nchi sita ziliazimia kutoa jumla ya askari 3000 kulinda amani eneo hilo, Tanzania ikiwa ni moja wa nchi hizo, nchi nyingine zikiwa ni Malawi, Afrika Kusini, Angola, Botswana na Zimbabwe.

Kuvamiwa na Maagaidi
Taarifa za askari wa Tanzania walioko Msumbiji kuvamiwa zilitufikia Novemba 19, 2022. Chanzo chetu cha uhakika kimefuatilia na kubaini kuwa uvamizi huu ulitokea tarehe 15 Novemba 2022 lakini hayo magari hayapo mikononi kwa Magaidi kama ilivyoripotiwa.

Aidha, Kutokana na unyeti wa jambo hili, hatutaweka taarifa za kina zaidi.
15 Reactions
Reply
Back
Top Bottom