saidoo25
JF-Expert Member
- Jul 4, 2022
- 602
- 1,407
Kuna taarifa zinaenea sana mitandaoni zikimhusisha Mbunge wa Geita Vijijini, Joseph Kasheku Musukuma na Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mashimba Ndaki kufadhili vitendo vya uvuvi haramu ili waweze kutajirika kupitia uvuvi haramu na kusababisha kuadimika kwa samaki na dagaa Ziwa Victoria na kuchochea ugumu wa maisha kwa wananchi.
Msukuma anadaiwa kuendesha makundi makubwa ya wavuvi haramu na kuwahakikishia kuwa hawatakamatwa kwa kuwahadaa kuwa Rais Samia amekataza wananchi wasikamatwe waachwe wavue wanavyotaka kama sehemu yake ya kufungua nchi na kukuza biashara.
Msukuma anatuhumiwa kutumia jina la Rais vibaya kwa kushirikiana na Waziri Mashimba Ndaki ambaye jana Rais Samia ametangaza kukosa imani nae kutokana na usimamizi mbovu wa wizara yake.
Mashimba naye mara kadhaa amekuwa akilalamikiwa kuhusiana na kushamiri kwa uvuvi haramu Ziwa Victoria na hadi Gazeti la Raia Mwema liliwahi kuripoti juu ya Hatari ya kwisha kabisa kwa samaki katika Ziwa Victoria lakini Waziri huyo anadaiwa kuwaagiza maafisa wake wasimkamate mtu yoyote kwa kuwa Rais amekataa wananchi wasionewe.
Mbunge wa Viti Maalum, Mariam Ditopile akichangia bajeti ya Wizara ya Mifugo na Uvuvi kwa mwaka 2022/2023 Bungeni alieleza bayana hali ni mbaya ya kukosekana kwa samaki Ziwa Victoria na kutishia viwanda kufungwa lakini Waziri hakusikiliza ushauri huo na kuendelea kuwaagiza maafisa wake wasimkamate mtu yoyote.