Msukuma Mahamani

X-PASTER

JF-Expert Member
Feb 12, 2007
11,620
1,787
Kuna jamaa mmoja mkoani Mwanza, alikamatwa kwa kosa la kuwa na silaha aina ya gobore kinyume cha sheria. Siku ya mahakama kabla ya kesi yake kuanza, kulikuwa na kesi nyingine ya wizi wa ng'ombe.

Mshtakiwa wa kesi ya ng'ombe ktk utetezi wake alijitetea kuwa yule ng'ombe alikuwa amemrithi toka kwa baba yake na alimpata tangia akiwa ndama.

Hakimu na wazee wa baraza baada ya kuridhika na utetezi, Mshtakiwa akaonekana kuwa hana kesi ya kujibu na akaachiwa huru kuendelea kumiliki ng'ombe wake....

Jamaa yangu Maganga kwa kuwa alikuwa mahakamani na alisikiliza ile kesi ya wizi wa ng'ombe, akaona kuwa na yeye bora aige kile alichokisikia kwenye kesi ya wizi wa ng'ombe.

Kesi yake ilikuwa kama hivi:

Msoma Mashtaka: Bwana Maganga unashtakiwa kwa kosa la kumiliki, bunduki aina ya Gobore kinyume cha sheria.

Hakimu: Mshtakiwa unaweza kujitetea?

Maganga: Bwana Mheshimiwa hakimu, kwa kweli huu ni uwonevu na wivu tu, Hili ligobore nililipataga kwa Babu yangu mzaa Babu yake na Babu yangu, Yaani tangia likiwa kibastora kidogo hakiyamungu, nimelitunza mpaka leo limekuwa limebarehe na kuwa Ligobore likubwa kabisaaa... Bwana mheshimiwa hili ni la kwangu kabisa, tangia likiwa dogo.

Hakimu: Kwa kuwa umeitunza tangia ikiwa bastora ndogo, kwa hali hiyo umeihakikishia mahakama kuwa hilo gobore ni la kwako.

Maganga: Ndio Bwana Hakimu. Ni la kwangu kabisa bila shaka

Hakimu: Na kwa kosa hilo la kuwa na bunduki yenye kukuwa na kuongezeka ukubwa. Nakuukumu kifungo cha miaka mitano jela na kazi ngumu, ili hiwe ni fundisho kwa wengine.

Na kwa kuiepusha hilo ligobore lako lisifikie kuwa RPG, Mahakama inaitaifisha kwa manufaa ya umma...

Kooooooooooooorrrrtiiiiiiiiii....!
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom