Msukuma akwama polisi, mamia wamiminika mahakamani kumsubiri

Bongo movie, huwezi kupoteza muda kwa kile anachokifanya msukuma.. Huyu ni mpigaji na mkurupukaji/ mpenda sifa, somewhere wanamtumia kuaminisha jamii hata wao wanakaa jela aka wanaisoma namba lakini ukweli sio huu kifupi wanazuga..

Watanzania muwe makini sana wakati huu kuliku mwingine..
Ivi ile bia ya 'The Kick' bado ipo?
 
Jamaa ni natural crook who bought his way into CCM machinery like many others of his kind. Hata huo utajiri wake ukifuatiliwa umetokana na uhalifu wa hali ya juu.
Ni kweli. Kuna siku aliongea star TV.. Mtu aliyeweza kujaza (ngano/sukari)iliyokwisha muda wake kwenye viroba vipya na akauza akapiga hela ndefu.. Kwa kukiri huko ingekuwa ni nchi za wenzetu angeshakamatwa kuhojiwa. Lkn pia alisema alikuwa anatorosha gold kwa njia za magendo kwenda Kenya...na alikuwa anaongea kama mambo mazuri... Bangi ni sheeda
 
Pelekeni maigizo huko mnafanya hivyo ili ionekane sio wabunge wa upinzani tu wanaonewa too bad mmekosea timing tayari imani imeshajengeka kwa wananchi kwamba wabunge wa upinzani wanaonewa
 
katika hili niko pamoja na polis.. msukuma angalau aswekwe ndani wiki nzima. kwa hili amekosea sana. iwejewenyekiti wa chama kilichoko anaanzisha vurugu?
 
Mamia ya wananchi, viongozi wa CCM na matajiri wakubwa wa mji wa Geita wamemiminika katika viunga vya mahakama ya hakimu mkazi Geita wakisubiri kupandishwa mahakamani kwa Mbunge wa Geita Vijijini, Joesph Msukuma na madiwani kumi wanaoshikiliwa na jeshi la polisi kwa kusababisha vurugu zilizotokea Septemba 14 mwaka huu.

Walianza kufika mahakamani majira ya saa nane mchana wa leo Jumatatu baada ya taarifa kuanza kuenea kuwa watapandishwa mahakamani lakini hadi kufika majira ya saa 9:20 alasiri Katibu wa CCM Mkoa wa Geita, Adam Ngalawa akatangaza kuwa viongozi hao hawatafikishwa tena mahakamani kutokana na muda wa Mahakama kumalizika.

“Tulikua tunawasubiri wenzetu tuwawekee dhamana lakini nimepigiwa simu sasa hivi kuwa hawataletwa tena mahakamani kwa kuwa muda wa Mahakama umekwisha na taarifa nilizopokea tumeambiwa wataletwa kesho,”amesema Ngalawa.

Wakizungumza baada ya kauli ya katibu kuwa viongozi hawataletwa mahakamani baadhi ya wafuasi Ikorongo Otto na Masanja Malembeka wamesema kwa sasa hofu imetanda kwa wananchi kwa kuwa huo haukuwa utamaduni uliozoeleka wa kuona viongozi wanakamatwa wakiwa wanadai mali zao.

Awali akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake Kamanda wa Polisi mkoani Geita, Mponjoli Mwabulambo amesema wote wanaoshikiliwa bado wako ndani na watafikishwa mahakamanil leo hata kama muda wa mahakama utakuwa umekwisha watamuomba hakimu.

Amesema dhamana za watuhumiwa ziko wazi kwa kua ni haki ya mtuhumiwa lakini akasema dhamana hiyo inategemea na mazingira ya tukio.

Kamanda amesema bado zoezi la kuwakamata madiwani waliokimbia linaendelea na kuwakata wasiwe wakimbizi badala yake warudi kwenye familia zao kwa kuwa kosa la jinai halina mwisho na lazima watakamatwa kwa uvunjifu wa sheria.

Chanzo: Mwananchi
Kwa sasa tunahangaika na LISU msihamishe Goli
 
Aliwahi mwambia waziri Magembe kuwa atamroga kwa ile ishu ya wafugaji ,nadhani kwa ishu alonayo sasa ndo sehemu muafaka ya kuonyeshea ndumba zake tuzione awaloge wote walomweka ndani wakati alikuwa anatetea wananchi wake.
 
Kumbe hii serikali ni ya kweli yaani kama msumeno vile.
Wangekuwa chadem ungesikia kesho wataongea na vyombo vya habari.
 
Huyu Msukuma mmojawapo ya wabunge wa CCM ambayo wana kiherehere sana mwache akae huko mahabusu apate akili.
 
Back
Top Bottom