Mwanahabari Huru
JF-Expert Member
- Mar 9, 2015
- 14,243
- 34,903
HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam imekabidhi timu ya soka ya manispaa hiyo KMC FC kwa wananchi kwa ajili kuisaidia ishiriki michuano ya Ligi Kuu Tanzania bara.
Hatua hiyo inatokana na timu hiyo inayoshiriki Ligi daraja la kwanza kutofanya vizuri kwa miaka mitatu mfululizo tangu inunuliwe.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo na wadau wa soka wa manispaa hiyo, Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni, Boniface Jacob alisema mwenendo mbaya wa timu hiyo imesababisha ishindwe kufika mbali.
Alisema kutokana na mwenendo huo, manispaa hiyo imeamua kuwakutanisha wadau wa soka ili kuwakabidhi timu.
"Awali tulikuwa hatujafanya hivyo ila tumeonelea tuirudishe kwa wananchi ili wapate fursa ya kutoa mchango wao, licha ya kuwa usimamizi wa masuala ya bajeti utakuwa chini ya halmashauri," alisema. Meya Jacob ambaye pia ni alike wa Mwenyekiti wa kikao.hicho, alibainisha kuwa licha ya timu hiyo kugharamiwa kwa kila kitu lakini bado imekuwa haifanyi vizuri. "Tumekosa fursa mbalimbali ikiwemo ya timu yetu kwenda jijini Humburg Ujeruman, endapo tungefanya vizuri ama kupanda daraja kushiriki Ligi Kuu," alisema. Katika mkutano huo ulioudhuliwa na wadau mbalimbali, walieleza kuwa kushuka kwa timu hiyo kunatokana na kutoshirikishwa kwa wananchi muds.mrefu. Mdau wa soka, Ramadhan Kampira alisema kuwa lazima iundwe kamati ya wataalam ili kuisimamia timu hiyo ndani na nje ya uwanja. "Haya yote.yanafanyika lakini tutambue tumechelewa sana, ilatakiwa mipango ianze muda mrefu hatuwezi kufanya usajili ndani ya wiki tatu kisha tuamini tutafika Ligi Kuu," alisema. Mdau mwingine, Idd Mbonde alisema kuwa timu hiyo ilikosa utawala bora wa kuisimamia ndio maana imekuwa ikifanya vibaya. "Kinachotakiwa kufanyika sasa hii timu wakabidhiwe wananchi angalau kwa miaka miwili ili tuhakikishe inafanya vizuri," alisema
Hata hivyo Meya Jacob alimaliza kikao hicho kwa kuunda kamati ya uongozi ya watu 12 wataohakikisha wanasimamia usajili wa wachezaji,katiba na uchaguzi wa uongozi wa kudumu.