Msosi wa lugha huu hapa, najua wengi mlikuwa na njaa sana

Amafita

Member
Jul 22, 2019
65
125
Asalam Alaykum (Amani iwe nanyi)

Yafuatayo ni baadhi ya maneno ya Kiswahili ambayo huwa hayatumiki sana na kupelekea kutokujulikana na watu wengi katika jamii zetu hivyo kupunguza kama sio kuua matumizi ya maneno hayo.

Swahili - English
Kimemeshi - Charger
Kitenzambali - Remote
Karakara - Passion Fruit
Bukunyika - Kangaroo
Kivungulio - Greenhouse
Kambarau - Lift
Kichokonoo - Toothpick
Kadiwia/ Mkamimo - Simcard
Kipakatalishi - Laptop
 

Amafita

Member
Jul 22, 2019
65
125
Course work je ?
Naamini Kiswahili ni lugha ambayo haijajitosheleza kwa maana kwamba bado kuna maneno ya lugha za kimataifa ambayo huwezi pata neno mbadala la Kiswahili.

Sijui kuhusu course work hivyo kama unafahamu neno hilo kwa Kiswahili, nitashukuru sana utalimwaga hapa
 

Amafita

Member
Jul 22, 2019
65
125
Daaah kiswahili kisikie hvo hvo.. ndio maana mm ukiniuliza aina za Maneno hua sielewi kabisa.. sijui nomino,vishazi , viwakilishi nk.
Ila ukaniuliza kuhusu part of speech nakujibu ata kama nimesinzia.
Kiswahili ni kigumu kushinda Kiingereza
 
  • Thanks
Reactions: THT

Mtundu wa Tech

JF-Expert Member
Aug 19, 2019
351
250
mkuu utanivunja mbavu zangu aisee
Daaah kiswahili kisikie hivyo hivyo. Ndiyo maana mimi ukiniuliza aina za Maneno huwa sielewi kabisa. Sijui nomino, vishazi, viwakilishi nk.

Ila ukaniuliza kuhusu part of speech nakujibu hata kama nimesinzia.
 

Amafita

Member
Jul 22, 2019
65
125
Inawezekana maana vitu vingi ni kiarabu
Ila ni vizuri tungetunga na sisi majina tofauti
Ni rahisi kuwa na majina yetu kwa vitu ambavyo havikuletwa na watu wa mataifa mengine. Kwa mfano matembele, kisamvu, ng'ombe, nyumba, kinu n.k havikuletwa na ukoloni ndio maana majina yake yalikiwepo tangu zamani lakn baiskeli, simu, televisheni, penseli, rula n.k hatukuwa navyo ndio maana tumetohoa kutoka lugha za wenzetu.

Na ikumbukwe pia hakuna lugha duniani inayojitegemea yenyewe au kujitosheleza hivyo maneno mengine bila kujali yalikuwepo au hayakuwepo lazima yataingiliana au kufanana na ya lugha nyingine.
 

black sniper

JF-Expert Member
Dec 10, 2013
16,212
2,000
Amafita,

Kweli kabisa lakini katika lugha nyingi kiswahili tumechagua wenyewe kuwa hivyo kwa kuiga maneno ya watu waliokuja kwetu na kueneza lugha yao. Kwa mfano waarabu na wahindi. Ila waarabu ndio zaidi maana mpaka walivyovikuta kwetu wakayataja kwa lugha yao na sisi tukaiga na kuendeleza lugha yao.

Hapa tu kuna maneno kama manne au matano ambayo ni ya kiarabu
Mataifa mengine hawana vitu vingi kama chakula au wanyama lakini wametumia maneno unique ambayo wao tu ndio wanatumia
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom