Msongomano soko kuu k/koo: Mtoto aaga dunia; serikali ya DSM itenge barabara ya kuingia na Kutokea

R.B

JF-Expert Member
May 10, 2012
6,296
2,573
Kutokana na msongamano mkubwa uliopo soko kuu la kariakoo ; Toka Juma tatu umati mkubwa karikooo ; unaitaji uangalizi wa hali ya juu; Jana mama aliyebeba mtoto alikosa kichanga hicho ; ingawa sababu rasmi haijatajwa kuwa ni hewa au mbinyo.
ushauri serikali ya mkoa Dar es salaam tunaomba itenge barabara ya kuingia na nyingine kutokea
upload_2017-6-23_7-52-13.jpeg
upload_2017-6-23_7-52-28.jpeg
 
Kiukweli hali si hali kwa sasa katikati ya jiji,hasa kipindi hiki kuelekea sikukuu ya Eid.Wanaotafuta mahitaji ni wengi sana
 
Ushauri mzuri mkuu...
Pia pale bora kuhamisha kabisa baadhi ya huduma kwa lazima ili mahitaji mengine yanayosababisha watu kwenda kariakoo wayapate sehemu nyingine.
watu wengi wanaenda kwa sababu ya unafuu wa bei za vitu, unafuu huu ukihamishiwa mahala pengine utapunguza msongamano.

4.jpg
 
Mimi nadhani wangeweka maduka yanayofanya kazi usiku tu, yani mengine yafunguliwe mchana mengine usiku, labda msongamano ungepungua.
ila wazo lako la barabara ni zuri japo msongamano unaletwa na hao machinga wanaomwaga vitu vyao chini, barabara finyu mtu kaweka nguo chini, magari yapite hapo, watu wapite hapo na ole wako ukanyage bidhaa unanunua, lol.
 
LAWAMA LAZIMA ; UKIZINGATIA MWAKA JANA MAANDALIZI YA SHEREHE YA IDD MAMA MJAMZITO ALIKUFA K/KOO .
 
Sipati picha pale mtaa wa Kongo kuna hali gani maana ule ndio mtaa pendwa kwa wakina mama na wakina Dada.
 
Mimi nadhani wangeweka maduka yanayofanya kazi usiku tu, yani mengine yafunguliwe mchana mengine usiku, labda msongamano ungepungua.
ila wazo lako la barabara ni zuri japo msongamano unaletwa na hao machinga wanaomwaga vitu vyao chini, barabara finyu mtu kaweka nguo chini, magari yapite hapo, watu wapite hapo na ole wako ukanyage bidhaa unanunua, lol.
Unawafahamu vibaka wewe? Uende shopping kkoo usiku utapita vipi jangwani kwa mfano?
 
  • Thanks
Reactions: R.B
culture gal si watu wote huenda kkoo kwa magari wengine hutembea kwa miguu. Acha kufikiri kiulayaulaya. Ukisema kkoo lifanye kazi usiku ni kukaribisha matatizo zaidi. Polisi wetu wenyewe muda wote wanahangaika na UKAWA watalinda usalama saa ngapi?
 
Kama wewe kwako ni shida kwa wengine inawezekana, na hiyo jangwani unauliza kwa miguu au kwa gari??

Hata wafanyabiashara wa Malawi ,Congo.,Zambia sijui kama wanaweza kwenda usiku Kariakoo kwa kuhofia usalama wao labda usalama uboreshwe kwanza.
 
Back
Top Bottom